Mwaka 2005 ni mwaka wa 60 tangu kuzaliwa kwa Umoja wa Mataifa. Mwaka huu Umoja wa Mataifa umepiga hatua zenye taabu katika mageuzi yake chini ya matarajio mbalimbali na mikwaruzano mikali ya nchi mbalimbali duniani.
Katika miaka 60 iliyopita, Umoja wa Mataifa umefanya kazi muhimu isiyoweza kuchukuliwa na jumuiya nyingine kwa ajili ya kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya binadamu. Lakini mwaka hadi mwaka, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameongezeka siku hadi siku, lakini ufanisi wake umekuwa ukipungua hatua kwa hatua, hata ada za uanachama ni vigumu kupatikana, na kashfa kuhusu mpango wa mafuta kwa chakula ilidhuru vibaya zaidi sura ya Umoja wa Mataifa. Baada ya kumalizika kwa vita vya baridi, masuala ya usalama yasiyo ya jadi kama vile ugaidi, uhalifu wa jumuiya za kimataifa, hali ya mazingira inayozidi kuwa mbaya na maafa ya kiviumbe, yote hayo yanatishia moja kwa moja amani na usalama wa dunia, Umoja wa Mataifa umeonekana hauna uwezo mkubwa katika kushughulikia masuala hayo. Hali mbaya zaidi ni kuwa, katika mambo ya kimataifa Marekani hutekeleza mkakati wake wa upande mmoja na kuchukua hatua zake bila kukubaliwa na Umoja wa Mataifa, hali hiyo imeufanya Umoja wa Mataifa ujitumbuize katika hali zenye taabu kubwa zaidi. Wakati huo huo, nchi kadha wa kadha zinazoendelea zinaukosoa Umoja wa Mataifa kutotilia maanani vya kutosha suala la maendeleo, na kutokuwa na uwezo na nguvu katika kupunguza migogoro ya kikanda na kuzuia vita visitokee.
Kutokana na kukabiliwa na changamoto, Umoja wa Mataifa hauna la kufanya ila tu kufanya mageuzi ili kujipatia tena nguvu ya uhai na kuonesha umuhimu wake. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Kofi Annan mwezi Machi mwaka huu alipotoa ripoti kwa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa alizitaka nchi mbalimbali duniani zichukue vitendo halisi vya kuhimiza Umoja wa Mataifa upige hatua halisi katika mageuzi yake. Bwana Kofi Anna alisema:
Hivi sasa tunahitaji nchi mbalimbali zitoe taarifa au ahadi, na tunazitaka zichukue vitendo halisi ili taarifa yetu iweze kutekelezwa kihalisi.
Nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeona kuwa Umoja wa Mataifa umefika hali ambayo unapaswa kufanyiwa mageuzi, ama sivyo hautaweza kuonesha umuhimu wake, lakini zina migongano mikubwa kuhusu mwelekeo na kanuni za mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Hivi sasa pande mbalimbali zinazohusika zimefikia maoni ya pamoja kuhusu lazima kupanua baraza la usalama, lakini zina maoni tofauti juu ya namna ya kupanua baraza la usalama.
Undani wa mageuzi ya baraza la usalama ni kugawa tena mamlaka ya kimataifa. Kupiga hatua kubwa katika mageuzi hayo, kutakutana na migongano mikali zaidi. Mtaalamu wa China wa suala la Umoja wa Mataifa ambaye pia ni profesa wa chuo kikuu cha kidiplomasia Bwana Zheng Qirong amedhihirisha kuwa, katika hali ambayo kumekuwepo migongano mikubwa, haipaswi kulazimisha kusukuma mbele mageuzi ya baraza la usalama. Alisema:
Tunapendekeza kujadili ipasavyo na kufanya mashauriano ya kutosha ili kupata njia ya kuondoa migongano. Kulazimisha au kuweka kikomo cha muda wa mageuzi si hatua yenye busara, na kulazimisha kupiga kura hakika kutasababisha ufarakanishaji kwenye Umoja wa Mataifa.
|