Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-02 17:39:20    
Kupanda basi kutembelea nchini China

cri

Leo tunapenda kuwafahamisha njia mbili za kupanda basi kutembelea nchini China, njia hizo mbili ni kutoka Beijing hadi Shanghai, na kutoka Beijing hadi Xian, ambazo zinapendwa na watalii wengi kutoka nchi za nje.

Naibu msimamizi mkuu wa idara ya maendeleo ya soko katika shirika kuu la utalii wa kimataifa la China Bwana Guo Wenbin alituambia:

Kupanda basi kufanya matembezi nchini China, kunatokana na hali nzuri ya ujenzi wa barabara nchini China katika miaka ya hivi karibuni. Hivi sasa nchini China barabara nyingi zinaungana. Shirika letu limeweka njia mbili za matembezi, ya kwanza ni kupanda basi kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Shanghai, njiani itapita Tianjin, Mlima Taishan, maskani ya Confucius Qufu, Xuzhou, Suzhou, mwishoni kufika Shanghai, kwa jumla safari hiyo inahitaji siku 12.

     

Njia nyingine ni kupanda basi kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Xian, njiani basi linapita Baoding, Handan, kufika Anyang, Zhengzhou, Luoyang, Sanmenxia, mwisho kufika Xian, safari hii inahitaji siku 9.

Bwana Guo alisema hivi sasa katika miji na sehemu zenye vivutio zilizoko kando ya barabara zenye mwendo kasi nchini China, miundo mbinu ya kuwapokea watalii inaboreshwa siku hadi siku, hivyo kupanda basi kutembelea miji mbalimbali na sehemu zenye vivutio nchini China hakuna taabu. Watalii wanaopanda basi kila siku wanakaa ndani ya basi kwa saa 4 hivi, toka mji mmoja hadi mji mwingine, shirika la utalii huwapanga watalii kukaa katika mji huo kwa siku moja au siku mbili, ili kwenda huku na huko kufanya utalii.

Mwongozaji wa watalii wa shirika kuu la utalii wa kimataifa la China Bi.Gao Feifei alituambia, kupanda basi kutembelea nchini China kunapendwa sana na watalii kutoka nchi za nje. Kwani watalii wanaona kuwa wakipanda basi kutembelea nchini China wanaweza kuangalia vizuri mandhari ya sehemu zilizoko kando ya barabara, furaha waliyo nayo haiwezekani kupatika katika safari yao kwa kupanda ndege. Hasa katika njia zilizowekwa na shirika la utalii wa kimataifa la China za kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Shanghai, na kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Xian, wanasema njiani wanaweza kuangalia mandhari ya sehemu nyingi na kuona vitu vingi.

Bi. Gao Feifei amekuwa mwongozaji wa watalii wa njia ya kupanda basi kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Shanghai katika miaka miwili ya hivi karibuni, alitufahamisha vivutio vya safari ya kupanda basi kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Shanghai, alisema:

Watalii wana hamu ya kutazama majengo ya kale na utamaduni wa kale wa China. Mjini Beijing wanapenda kwenda Jumba la kale la kifalme na Ukuta mkuu; huko Qufu mkoani Shandong wanapenda kutembelea Hekalu la Confucius, Msitu wa Confucius, aidha kutembelea makaburi ya kale ya Enzi ya Han huko Xuzhou, na mwisho wakafika Shanghai, Shanghai ni mji mkubwa unaojulikana duniani, watalii wanaweza kununua vitu huko Shanghai, pia wanaweza kupata fursa ya kuonja vyakula vitamu mbalimbali, hayo yote yanapendwa na watalii.

  

Katika hali ya kawaida, watalii wengi kutoka nchi za nje wanaweza kuchagua Beijing na Shanghai kuwa lengo lao la utalii, na kupanda ndege kwenda kwenye miji hiyo miwili mikubwa, njiani hawawezi kupata nafasi ya kutembelea Qufu na Xuzhou. Lakini kwa kweli Qufu na Xuzhou ni sehemu mbili zinazostahili kutembelewa na watu. Qufu ni maskani ya Confucius, mwanafikra maarufu wa China wa zama za zaidi ya miaka 2000 iliyopita, mjini Qufu kuna mabaki mengi kuhusu Confucius, kama vile Hekalu la Confucius ambalo lilijengwa kutokana na makazi ya Confucius, Msitu wa Confucius ambao ni sehemu ya makazi ya jadi ya ukoo wa Confucius na makaburi ya ukoo wa Confucius. Na mjini Xuzhou, kuna makaburi mengi ya kale, kwa mfano kuna makaburi zaidi ya matano ya familia moja moja ambayo yalijengwa miaka 1900 iliyopita. Mwongozaji Bi.Gao Feifei alisema, kila mara alipowaongoza wageni kwenda kutazama mahekalu ya kale na makaburi ya kale, wageni huwa na hamu kubwa na kufurahishwa sana.

Bi. Gao pia aliona wageni waliopanda basi kufanya utalii nchini China huwa na uchangamfu mkubwa njiani, kila walipopita kwenye sehemu moja iliyoko kanda ya barabara ya mwendo kasi, wageni husifu sana mandhari ya njiani, kama kuna wageni wakitoa ombi, Mwongoza wa utalii humtaka dereva aegeshe gari njiani, ili wageni watoke nje kuangalia na kupiga picha.

Hivi sasa watalii wengi kutoka Marekani na Ulaya wanapenda njia ya kupanda basi kutembelea nchini China. Mtalii kutoka Marekani Bill Milewski amewahi kupanda basi mara tatu kutembelea nchini China. Alituambia:

Kwa sisi wageni kila tukija China kwa utalii ni kwa muda mfupi, hivyo sipendi kupanda ndege, nilipanda basi kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Shanghai, njiani niliweza kupata nafasi ya kuangalia Mlima Taishan na Hekalu la Confucius, hii ni njia bora ya utalii. Njiani nilipotembelea sehemu yenye ustaarabu wa kale, pia niliweza kuona mambo mengi mapya.

Meneja wa ngazi juu wa idara ya mawasiliano na nje katika shirika kuu la utalii wa kimataifa la China Bwana Zhang Shuo alituambia kuwa, wageni wengi kama Bwana Milewski waliochagua njia ya kupanda basi kutembelea nchini China, huwa ni wageni wenye hamu kubwa juu ya ustaarabu wa kale wa China, wageni hao wakipanda basi kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Shanghai, huwa wanaweza kuja China tena kupanda basi kufunga safari kutoka Beijing na kwenda Xian. Bwana Zhang alisema:

Kufuga safari kutoka Beijing na kwenda Xian, njiani watalii wanaweza kuona makaburi mengi ya kale, wakifika Xian hakika watatembelea sehemu yenye sanamu za askari na farasi vya enzi ya Qin, na wakifika Sanmenxia wanaweza kuona vitu vingi vya mabaki ya kale, wageni wote walifurahia matembezi hayo. Aidha huko Yinxu wanaweza kuona maandishi yaliyochongwa kwenye magamba ya kobe, maandishi hayo yaligunduliwa huko Yinxu.

   

Sanamu za askari na farasi alizozitaja Bwana Zhang zinasifiwa kuwa ni "mwujiza mkubwa wa 8 duniani", sanamu hizo zilizikwa kwa kuambatana na mwili wa mfalme Qinshihuang ambaye alikuwa mfalme wa kwanza katika historia ya China. Watu wa vizazi vya hivi sasa waligundua na kufukua sanamu za askari na farasi zenye ukubwa kama walivyo binadamu na farasi, sanamu hizo ziliundwa kama kikosi kimoja cha askari na farasi chini ya ardhi, vikilinda kaburi la mfalme Qinshihuang. Sehemu ya Yinxu iko Anyang mkoani Henan, katika sehemu hiyo yalifukuliwa magamba ya kobe au mifupa ya wanyama ipatayo laki 1.5 ambayo ilichongwa maandishi, maandishi ya kichina yanayotumiwa na wachina hivi sasa ndiyo yalitokana na maandishi hayo yaliyochongwa kwenye magamba ya kobe au mifupa ya wanyama.

Bwana Zhang aliongeza kwa kusema, wameona kuwa watalii kutoka nchi za nje kama Bwana Milewski si kama tu wana hamu kubwa juu ya vitu vya mabaki ya kale vya China, bali pia wana udadisi mwingi juu ya China ya hivi sasa. Shirika la utalii wa kimataifa la China linafanya mpango wa kuanzisha njia nyingi za kupanda basi kutembelea nchini China, ili watalii kutoka nchi za nje watapata fursa ya kuielewa vizuri zaidi kuhusu China.

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-02