Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-04 18:55:18    
Mapishi ya bilinganya kwa kukaanga

cri

Mahitaji

Bilinganya gramu 200, pilipili mboga gramu 100, kiasi kidogo cha vitunguu maji, tangawizi, chumvi na M.S.G

Njia

1. osha bilinganya ksha likate liwe iwe vipande vipande, na uikate pilipili mboga iwe vipande vidogo.

2. pasha moto na tia mafuta kwenye sufuria, tia bilinganya na korogakoroga kwa dakika 2, halafu tia pilipili mboga kwenye sufuria korogakoroga ili vikauke kasha pakua.

3. pasha moto tena mpaka mafuta yawe na joto la nyuzi 70, tia vipande vya tangawizi, korogakoroga, tia vipande vya bilinganya na pilipili mboga kisha koroga, tia chumvi na M.S.G korogakoroga, tia vitunguu maji korogakoroga, na uiache ichemke kidogo halafu ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.