Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-05 20:25:05    
Profesa wa muziki wa chuo kikuu cha sanaa cha Xinjiang Bw. Sulaman Imin

cri

 

Muda si mrefu uliopita muziki wa jadi wa kabila la Wauygur uitwao "Mukham 12" ulithibitishwa kuwa urithi wa utamaduni simulizi na shirika la elimu, sayansi ya utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. Muziki wa "Mukham 12" ulitungwa na kukamilika baada ya miaka mia kadhaa, ni mchanganyiko wa nyimbo, ngoma na muziki, umesifiwa kuwa mama wa muziki wa kabila la Wauygur. Katika sehemu inayojiendesha ya kabila la Wauygur, mkoani Xinjiang, watu wengi akiwemo Profesa Suleiman Imin wanafanya utafiti kuhusu muziki wa aina hiyo. Licha ya kufanya utafiti wa muziki, Bw. Suleiman pia ametunga muziki mwingi, na kuupiga kwa ala za fidla na piano.

Bwana Sulaman mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 ni profesa wa muziki wa chuo kikuu cha sanaa cha Xinjiang. Muziki mliousikia ni muziki maarufu wa piano uliotungwa na Bw. Suleiman, muziki huo uitwao "Gulailai" umemsifu msichana Gulailai na kueleza upendo kwake. Muziki mwingine uliopigwa kwa ala ya fidla iitwayo "Kumbuka", muziki wa piano uitwao "Nilipokukumbuka" na muziki mwingine unatumiwa katika mafunzo ya vyuo vikuu vya muziki nchini China, baadhi ya wapiga fidla hata wanapiga muziki wake na kufundisha katika nchi za nje zikiwemo Australia na Russia.

Profesa Sulaman alizaliwa katika familia ya mkulima, kipaji chake cha muziki kinatokana na baba yake. Baba yake alikuwa hodari kuimba na kucheza ngoma, alijua kupiga ala nyingi za kikabila. Kutokana na kuathiriwa na baba yake, Bw. Suleiman alipenda sana muziki tokea utotoni mwake.

"Nilipokuwa nasoma katika shule ya msingi, baba yangu alininunulia ala ya Rawap na kunifundisha jinsi ya kuipiga. Baadaye alininunulia fidla. Nilipohitimu shule ya sekondari ya chini, nilikuwa hodari katika kupiga ala ya Rawap, fidla na kuimba."

Rawap ni ala ya jadi ya kabila la Wauygur, na fidla ni ala ya kimagharibi. Mwaka 1961, Bw. Suleiman alipokuwa na umri wa miaka 17 alisoma katika chuo kikuu cha sanaa cha Xinjiang, kutokana na uhodari wake wa kupiga ala hizo mbili. Licha ya kujifunza kupiga fidla, Bw. Suleiman pia alijifunza utungaji muziki. Baada ya kuhitimu masomo, Bw. Sulaman alibaki chuoni na kuwa mwalimu kutokana na masomo yake mazuri. Akisema:

"Nikiwa mwalimu lazima nijielimishe kuhusu somo langu. Nimejifunza mambo mengi kuhusu nyimbo za jadi za nchini China na za nchi za nje, na nimeona kuwa muziki wa jadi wa kabila la Wauygur ukiwemo "Mukham 12" una thamani kubwa zaidi kuliko muziki wa makabila mengine, unastahili kufanyiwa utafiti na kukusanywa, na kuwafahamisha watu wengi zaidi.

Bw. Suleiman alisema kuwa, "Mukham 12" ukiwemo nyimbo na muziki zaidi ya 340, ni mfumo mkubwa wa muziki, muziki huo unaonekana ni muziki kamili ambao unasikika vizuri sana, lakini ni vigumu kujifunza. Ili aweze kufahamu kanuni za muziki huo, Bw. Suleiman alikuwa anasikiliza muziki huo kwa makini usiku mzima, halafu alikuwa anajaribu kuiga kuupiga na kuuimba. Baada ya juhudi za miaka mitano, Bw. Suleiman alifahamu jinsi ya kupiga na kuimba muziki wa Mukham, ambpo hamu yake ya kutunga muziki imeongezeka siku hadi siku.

"Nataka kueleza muziki wa kabila la Wauygur kwa kupiga ala za kimagharibi, ili kuwafahamisha watu wengi zaidi wa nchini China na wa nchi za nje muziki wa kikabila wa Xinjiang. Lakini ni vigumu sana kuunganisha ala za kimagharibi na muziki wa kikabila wa Xinjiang, inahitaji juhudi kubwa."

Bw. Suleiman amefanikiwa kuandika makala nyingi za taaluma. Katika miaka ya 70 ya karne iliyopita, wimbo wa kumkumbuka kiongozi maarufu wa China hayati Zhou Enlai ulioimbwa na kundi la wanawake baada ya kutafsiriwa kwa Kichina ulienea kote nchini China. Baadaye Bw. Suleiman alitumwa kusoma katika chuo kikuu cha muziki cha China kwa miaka miwili. Katika kipindi hicho, alitunga nyimbo na muziki 10, kazi zake zilivutia uangalifu wa fani ya muziki nchini China.

Hadi leo, Bw. Suleiman ametunga muziki zaidi ya 200. Baadhi ya muziki zimepigwa na wapigaji muziki wengi wa nchini China na wa nchi za nje, lengo lake la kuwafahamisha watu wengi duniani muziki wa kikabila wa Xinjiang limetimizwa.

Upendo wa Suleiman kwa muziki wa kikabila wa Xinjiang pia umeonekana katika ufundishaji wake chuoni. Aliona kuwa vijana wa hivi sasa wana fursa nyingi za kupata mambo ya nchi za nje, lakini wakati wa kujifunza mambo ya nje hawapaswi kupuuza vitu vyenye thamani vya taifa la China. Hivyo aliwaelimisha wanafunzi wake kujifunza mambo mazuri kutoka nje na kuacha mabaya. Mwanafunzi wake Bwana Tokan Smagule ambaye sasa amekuwa profesa wa chuo kikuu cha sanaa cha Xinjiang alisema:

"Nakumbuka zaidi ya miaka 20 iliyopita, profesa Suleiman alianza kukusanya na kutunga vitabu vya kiada vya muziki wa makabila madogo madogo. Vitabu hivyo vimetuelimisha kikamilifu kuhusu utamaduni wa muziki wa taifa la China."

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-05