Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-05 19:59:07    
Russia na Ukraine zafikia makubaliano kuhusu bei ya gesi asilia

cri

Russia na Ukraine tarehe 4 huko Moscow zilisaini makubaliano ya miaka mitano ya utoaji wa gesi asilia, Ukraine imekubali bei iliyowekwa na Russia, na mgogoro kati ya nchi hizo mbili umekomeshwa.

Kutokana na makubaliano yaliyofikiwa siku hiyo kati ya pande hizo mbili, kampuni ya kihisa ya viwanda vya gesi asilia ya Russia itauza gesi asilia ya Russia kwa bei ya dola za kimarekani 230 kwa mita 1000 za ujazo kwa kampuni moja ya "nishati ya Russia na Ukraine", halafu kampuni hiyo itaichanganya gesi hiyo na gesi asilia kutoka nchi za Asia ya kusini za Turkmenistan, Kazakhstan na Uzbekistan, baadaye itauza gesi zilizochanganywa kwa bei ya dola za kimarekani 95 kwa mita 1000 za ujazo kwa Ukraine. Aidha, malipo ya kupita Ukraine wakati Russia kusafirisha gesi asilia kwa nchi za Umoja wa Ulaya yataongezeka kuwa dola za kimarekani 1.6 kutoka 1.09 kwa mita 1000 za ujazo.

Pande mbili Russia na Ukraine zote zimesifu makubaliano kati yao. Rais Vladmir Putin wa Russia siku hiyo alisema, makubaliano hayo yataleta athari yenye juhudi kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, pia yameleta hali ya utulivu kwa kuhakikisha Russia inatoa gesi asilia kwa nchi za Umoja wa Ulaya. Rais Vikort Yushchenko wa Ukraine pia alisema, Ukraine ni rafiki wa kutegemewa na itatekeleza majukumu yake yote ya kusafirisha gesi asilia ya Russia inayouzwa kwa nchi za Ulaya.

Katika siku kadhaa zilizopita Umoja wa Ulaya ulioathiriwa na mgogoro kati ya Russia na Ukraine kuhusu bei ya gesi asilia pia umefurahia Russia na Ukraine kuondoa mgogoro kwa haraka na juhudi. Maofisa wa Umoja wa Ulaya tarehe 4 walitoa taarifa ya pamoja wakisema, Umoja wa Ulaya unakaribisha Russia na Ukraine ziendelee kuwa mtoaji na msafirishaji wa gesi asilia kwa Umoja wa Ulaya.

Wachambuzi wamedhihirisha, kutokana na maslahi ya kiuchumi, jambo hili limeonesha Russia kutimiza lengo la kuuza gesi yake kwa bei ya dola za kimarekani 230 kwa kila mita 1000 ya ujazo. Wakati huo huo Russia pia imeioneshea dunia nguvu yake kubwa katika kufanya "mambo ya kidiplomasia katika sekta ya nishati".

Lakini Russia pia imepata hasara katika tukio hilo. Kwanza kitendo cha Russia cha kusimamisha utoaji wa gesi kilisababisha wimbi la "kuipinga Russia" nchini Ukraine, hii haisaidii sana kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Aidha machoni mwa wawekezaji wa nchi za magharibi na watumiaji wa nishati, Russia imetiliwa mashaka juu ya hali yake ya kutegemeka ikiwa mwenzi wa kiuchumi, hii inaleta athari mbaya kwa sura yake ya nchi kubwa ya nishati; zaidi ya hayo kitendo cha Russia cha kusimamisha utoaji wa gesi huenda kitazifanya nchi nyingi zaidi za shirikisho la Jamhuri huru zikaze nia kujitoa kutoka hali ya kuitegemea Russia katika sekta ya nishati, ambapo huenda itaweza kuyafanya "mambo ya kidiplomasia ya Russia katika sekta ya nishati" yapoteze matokeo yake.

Matokeo ya mgogoro kati ya Russia na Ukraine pia yameleta faida na hasara nusu kwa nusu kwa Ukraine. Ingawa kijuujuu, Ukraine imekubali bei iliyotoa Russia mwanzoni, lakini wachambuzi wa kisiasa wa Russia na Ukraine wameona kuwa, serikali ya Ukraine mwanzoni ilitaka kukubali bei iliyotoa Russia, ilichelewesha kuamua mara kwa mara ni kwa ajili ya kuchochea hisia za wananchi za kuipinga Russia, ili kufanya maandalizi ya kisiasa. Kitendo chake kimeonesha mwelekeo wake wa kuzipendelea nchi za magharibi, ikahurumiwa na kuungwa mkono na nchi za magharibi na nchi nyingine za shirikisho la Jamhuri huru.

Lakini kitendo cha Ukraine cha kuchelewesha kwa makusudi uamuzi wake, kimelaumiwa na Russia na kudhuru sura yake duniani, hii imeleta fursa kwa vyama vya upinzani vya Ukraine kuilaani serikali ya sasa ya Ukraine.