Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-09 20:14:21    
Kutalii msituni katika Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani

cri

Wakati wa Mwezi Oktoba, hali ya hewa imeanza kuwa baridi na majani mbugani imeanza kunyauka, watalii wanaokwenda kutalii mbuga za majani katika mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China walikuwa wanaanza kupungua. Lakini wakati huo msitu usiokuwa na mpaka na wenye rangi tofauti za majani unawavutia watalii wengi mkoani humo.

Tokea likizo la siku ya taifa tarehe mosi Oktoba, mandhari ya milima Da Xing An Ling yenye msitu mkubwa inawavutia watalii wengi. Licha ya kuwa watalii hao wanaweza kutembelea na kufurahia msitu wa misandali pia wanaweza kuchuma matunda mwituni na kuhisi maisha katika mazingira ya kiasili. Kama wakati unatosha, wanaweza kupata malazi kwenye vibanda vya mbao na kusikiliza sauti ya majani kuchakacha katika usiku. Mtalii mmoja kutoka sehemu ya kusini ya China alimwambia mwandishi wa habari akisema, huko ni dunia nyingine kabisa kama bustani ya peponi.

Naibu mkurugenzi wa Idara ya Utalii ya mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China Bw. Ma Yongsheng alisema, ingawa utalii kwenye msitu wa mkoa huo ulichelewa kufunguliwa, lakini unastawi haraka. Hivi sasa katika mkoa huo kuna bustani za misitu 20 zenye maeneo hekta milioni moja. Kwa makadirio, mwaka huu watalii watafikia milioni tano na mapato yatafikia yuan milioni 400.

Bwana huyo pia alieleza kuwa utalii katika mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China una njia nne, nazo ni utalii kwenye msitu wa milima ya Da Xing An Ling, utalii kwenye msitu wa mlima wa Yan Shan, utalii kwenye misitu ya milima ya Da Qing Shan na Ula na utalii kwenye msitu wa mlima wa He Lan.

Majani mekundu yawavutia watalii katika Ziwa Qiandaohu

Majira ya Autumn yanapofika kuanzia mwezi Oktoba, mandhari kwenye sehemu ya ghuba Hongye ya Ziwa Qiandaohu mjini Hangzhou imekuwa inavutia watalii wengi kwa kuwa huko majani yamebadilika kuwa mekundu kila mahali.

Sehemu ya Ghuba Hongye ya Ziwa Qiandaohu ilifunguliwa rasmi kwa watalii kuanzia tarehe 16 Septemba mwaka 2005 iko katika sehemu ya kiini cha Ziwa Qiandaohu, maana ya kichina ya Qiandaohu ni ziwa la visiwa elfu moja. Sehemu ya Ghuba Hongye iko kati ya visiwa vya Jinxian na penisula ya Xiaojinshan, na inakaribia sana na visiwa vya Wulong, Longshan na Shenlong ambapo zote ni sehemu zenye mandhari nzuri.

Sehemu hiyo ina urefu wa kilomita 3.5 na pembezoni mwake ni milima mingi mirefu, mandhari yanabadilika kufuatana na majira tofauti ya mwaka. Kila ifikapo majira ya Autumn, majani ya miti yanakuwa mekundu kama moto, mandhari kama hiyo inawafurahisha na kuwavutia watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali.

Kwa mujibu wa hali ya maumbile, mandhari ya sehemu ya ghuba ya Hongye kwenye Ziwa Qiandaohu imekuwa nzuri siku hadi siku kutokana na kujengwa kwa uwanja ndani ya msitu, njia ya kutembea katika mazingira ya kimaumbile, mikahawa ya chai ndani ya misitu, makazi ya ndege na bustani ya maua na gati la kuvusha kwa mashua, sehemu ya kuvua samaki kwa mshipi na kuchuma matunda katika bustani.

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-09