Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-10 20:03:08    
China yatekeleza mkakati wa kustawisha kituo kikongwe cha viwanda vya sehemu ya kaskazini mashariki

cri

Mkurugenzi wa ofisi ya baraza la serikali la China inayoshughulikia mambo ya kustawisha sehemu za kaskazini mashariki za China Bw. Zhang Baoguo, tarehe 27 Desemba, mwaka 2005 alipotoa hotuba kuhusu hali ya kustawisha kituo kikongwe cha viwanda vya kaskazini mashariki ya China kwenye mkutano wa 19 wa halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China alisema kuwa, katika miaka miwili iliyopita, utekelezaji wa mkakati wa kustawisha kituo kikongwe cha viwanda katika sehemu za kaskazini mashariki za China ulikuwa na mwanzo mpya.

Mwaka 2004 China ilitekeleza sera ya kufuta kodi za kilimo mikoani Heilongjiang na Jilin, na kuongeza ruzuku za uzalishaji wa nafaka za sehemu za kaskazini mashariki za China. Bw. Zhang Baoguo alisema mwaka 2004 serikali kuu ilitenga fedha za Yuan za RMB bilioni 11.59 kwa mikoa mitatu ya kaskazini mashariki kutokana na mageuzi ya kodi za vijijini, kutoa ruzuku za moja kwa moja kwa uzalishaji wa nafaka na ruzuku za mbegu bora kwa mikoa hiyo, na mwaka 2005 ruzuku hizo zilifikia Yuan bilioni 12.25. Alisema, mwaka 2005 mkoa wa Liaoning pia ulitekeleza sera hiyo, na kupunguza mzigo kwa wakulima kwa Yuan za RMB milioni 570. Mikoa ya Heilongjiang na Jinlin ilianzisha kazi za majaribio za kukamilisha mfumo wa utoaji huduma za jamii mijini baada ya mkoa wa Liaoning kufanya hivyo. Hivi sasa kazi hizo kwenye mikoa hiyo miwili zinakaribia kukamilika.

Bw. Zhang Baoguo alisema, serikali kuu imetoa sera mwafaka kwa mashirika ya kitaifa yaliyofilisika. Kutokana na kanuni ya "kuweka mkazo na kutoa kipaumbele kutokana na umuhimu wake, kuweka mpango kutokana na hali ya jumla na kutekeleza hatua kwa hatua", idara husika zitaendelea kuongeza nguvu za kuunga mkono na kutoa sera mwafaka kwa mashirika ya kitaifa ya sehemu za kaskazini mashariki yaliyofilisika, ili baadhi ya mashirika ambayo maliasili zake zimekwisha yaweze kuondolewa kwenye soko bila matatizo, na wafanyakazi wengi waweze kupangwa vizuri, pia zitatoa msaada wa fedha kwa viwanda vya serikali kuu vijitoe kutoka kwa uendeshaji wa serikali ili viwe mashirika ya kijamii. Mwaka 2005, viwanda 22 vya serikali vilivyoko kwenye mikoa mitatu ya sehemu ya kaskazini mashariki ya China vimejitoa kutoka kwa uendeshaji wa serikali, na kuanzisha mashirika ya kijamii, na serikali kuu ilitenga fedha za Yuan milioni 220 kwa kuyasaidia.

Imefahamika kwamba, kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa ya China inafanya juhudi kuunga mkono marekebisho ya miundo ya kituo kikongwe cha viwanda vya kaskazini mashariki, na kutekeleza mradi wa kutenga fedha kutoka dhamana ya taifa ili kufanya marekebisho na ukarabati wa kituo hicho kwa kufuata sera na mpango, na kuunga mkono viwanda vyenye nguvu vya kituo hicho viendelezwe. Hadi kufikia mwezi Novemba mwaka 2005, viwanda vyenye teknolojia ya hali ya juu vya kaskazini mashariki vilianzisha miradi 149, na serikali ilitenga Yuan za RMB milioni 816; na kupitisha kuanzishwa kwa vituo vya utafiti vya miradi ya taifa. Tatu ni kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2004, dhamana ya taifa yenye Yuan za RMB bilioni 4.288 ilitumika katika sekta ya kilimo, misitu na maji za sehemu za kaskazini mashariki, na serikali ilitenga fedha za Yuan za RMB bilioni 4.22 katika ujenzi wa barabara muhimu na barabara za vijijini za sehemu za kaskazini mashariki. Nne ni kuidhinisha miradi mingi mikubwa inayorahisisha marekebisho ya muundo.