Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-11 20:33:44    
Mfumo wa huduma za afya wapata maendeleo makubwa nchini China

cri

Habari kutoka Wizara ya Afya ya China zinasema kuwa katika miaka ya karibuni mfumo wa kulinda afya ya umma umepata maendeleo makubwa nchini China.

Tokea mwezi Septemba mwaka 2002 hadi mwishoni mwa mwaka 2005, miradi ya kukinga na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza iliyojengwa na vituo vya kinga na tiba vya ngazi mbalimbali nchini China imekuwa 2,416, na fedha zilizowekezwa katika miradi hiyo ni yuan bilioni 10.5, hivi sasa miradi hiyo karibu yote imekamilishwa. Kadhalika, miradi ya kupmbana na mlipuko wa magonjwa iliyoanzishwa na vituo vya magonjwa ya dharura na hospitali za magonjwa ya kuambukiza imekuwa 2.649, na fedha zilizotumika katika miradi hiyo ni yuan bilioni 16.4, hivi sasa miradi hiyo iko mbioni kujengwa. Pamoja na miradi hiyo mageuzi ya idara za kukinga na kudhibiti magonjwa na idara za usimamizi na utekelezaji wa sheria zinazohusu afya ya umma yamekamilika katika ngazi ya mikoa, na yamekuwa karibu kumalizika katika ngazi ya wilaya. Mfumo unaolingana hali ilivyo ya China katika kukinga na kudhibiti magonjwa kimsingi umekmilika nchini China.

Tokea mwezi Januari mwaka 2004 mfumo wa kutoa taarifa moja kwa moja hali ya magonjwa ya kuambukiza umeanzishwa kote nchini China, mikoa yote 31 ya China bara inaweza kupashana habari kuhusu hali ya magonjwa ya kuambukiza popote yalipotokea nchini China. Kwa kufanya hivyo mgonjwa ya kuambukizwa yakitokea hayatachelewa kujulikana, na habari zenyewe zinaaminika, uwezo wa kukinga na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza yanayohusu umma umeinuka. Wizara ya Afya ya China na mikoa kadhaa imeweka utaratibu wa kutoa taarifa kuhusu magonjwa ya kuambukiza kila baada ya kipindi fulani, utaratibu huo umeridhisha wananchi kufahamu hali ilivyo ya magonjwa ya kuambukiza nchini China na umeimarisha tahadhari dhidi ya magonjwa hayo na kudhibiti magonjwa hayo.

Kuanzishwa kwa mfumo huo wa kulinda afya ya umma kumeleta mafanikio wazi. Uwezo wa kupambana na magonjwa ya dharura umeinuka, na mfumo huo umethibitishwa kuwa ni mfumo mzuri na ulitoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya SARS na homa ya mafua ya ndege, magonjwa ambayo yanahatarisha afya ya umma.

Wakazi wa Beijing wanatazamiwa kuishi miaka 80 kwa wastani ifikapo mwaka 2010

Habari kutoka Shirika la Habari la Xinhua la China tarehe 8 zimesema kuwa kwa wastani umri wa miaka ya kuishi kwa wakazi wa Beijing ulifikia miaka 79.87 mwaka 2004. Mkuu wa idara ya afya ya Beijing siku chache zilizopita alisema kuwa hadi ifikapo mwaka 2010 umri huo unatazamiwa kufikia miaka 80.

Mkuu huyo alisema, katika kipindi cha "mpango wa kumi na moja wa maendeleo ya miaka mitano" Beijing itaanzisha na kukamilisha mifumo mitatu ya huduma za afya, nayo ni kukinga na kuhifadhi afya, kuendeleza maendeleo ya mambo ya afya mjini na vijijini kwa pamoja na kutoa huduma za matibabu, afya na hifadhi ya afya kwa haki na gharama nafuu kwa haraka, na kuifanya hali ya afya ya wakazi wa Beijing itangulie mbele nchini China. Hadi mwaka 2010 kwa wastani umri wa miaka ya kuishi kwa wakazi wa Beijing unatazamiwa kufikia miaka 80, kiasi cha kufa kwa watoto hakitazidi asilielfu sita, na kiasi cha kufa kwa wajawazito na wanaojifungua hakitazidi 15 kwa laki moja. Na tofauti kati ya wakazi wa vijijini na mjini katika malengo hayo matatu itapungua kwa thuthuthi moja katika msingi wa mwaka 2005.

Ili kuhimiza maandalizi ya wataalamu wa kazi mbalimbali za afya, hasa wahudumu wa afya katika sehemu za makazi mjini na vijiji, Idara ya Afya ya Beijing itaanzisha utaratibu wa kupima sifa za wahudumu wa afya, kutathmini uwezo wa kazi na utaratibu wa motisha. Hadi mwaka 2010, wahudumu wa afya waliohitimu vyuo vikuu na kuendelea, watapaswa kufundishwa zaidi katika vituo vya mafunzo vilivyokubaliwa na idara ya afya. Pamoja na hayo, wahudumu wa afya kwa wakazi wanaohudumiwa watapangwa kwa hali inayofaa, kwamba kimsingi kila wakazi 2,000 hadi 3,000 wanapatwa daktari mmoja mwenye uwezo wa magonjwa ya ndani na nje na muuguzi mmoja, na kila wakazi 2,000 wanapatwa mtaalamu mmoja wa kinga na hifadhi ya afya.

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-11