Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-11 20:43:15    
Mapishi ya mwani pamoja na doufu

cri

Mahitaji

Mwani gramu 20, doufu gramu 200, mchuzi wa soya vijiko 2, sukari nusu kijiko, kiasi kidogo cha maji, maji ya wanga na mafuta ya ufuta.

Njia

1. osha mwani na uuweke kwenye maji kwa dakika 10. pakue na uukate uwe vipande.

2. kata doufu iwe vipande, na washa moto tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia vipande vya doufu kwenye sufuria na uvikaange mpaka viwe na rangi ya hudhurungi, mimina mchuzi wa soya, korogakoroga, tia vipande vya mwani na mimina maji, baada ya kuchemka, tia sukari na punguza moto kidogo, na uache uendela kuchemka.

3. baada ya dakika 5 mimina maji ya wanga, pakue na mimina

mafuta ya ufuta na acha ichemke kidogo. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.