Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-12 14:47:48    
Rais Bush aanza kampeni ya uchaguzi wa bunge wa kipindi cha katikati

cri

Tarehe 10 rais Bush wa Marekani alitoa hotuba kwa mara ya pili mwaka huu mjiji Washington akisema kwamba Marekani itakuwa na mengi zaidi ya "mtihani na mhanga" nchini Iraq, na huku alishutumu Chama cha Demokrasia kukosoa ovyo sera ya serikali kuhusu vita vya Iraq. Wachambuzi wanaona kuwa maneno hayo yanalenga kupata uungaji mkono wa vita vya Iraq kutoka kwa wananchi na kukinyamazisha Chama cha Demokrasia ili kujipatia nafasi nyingi katika uchaguzi wa bunge wa kipindi cha katikati.

Katika siku hiyo, rais Bush alipohutubia Shirikisho la Askari Wasaafu wa Vita Nje ya Marekani alisema, jeshi la Marekani nchini Iraq limefanikiwa siku hadi siku, lakini safari itakuwa ngumu katika mwaka 2006, hii inamaanisha kuwa litakabiliwa na mengi ya "mtihani na mhanga".

Licha ya kueleza mkakati kuhusu vita vya Iraq, rais Bush alisema mengi kukihujumu Chama cha Demokrasia. Alisema anafurahia yale yaliyosemwa kwa nia nzuri, lakini yale yaliyokosoa serikali kwa kusema kuwa vita vilianzishwa "kwa ajili ya mafuta, kwa ajili ya Israel, na kupotosha fikra za watu wa Marekani" ni maneno ya ovyo. Rais Bush alisisitiza kuwa maneno kama hayo yatawapotezea askari wa Marekani nchini Iraq ukakamavu na kusaidia ujeuri wa vikundi vyenye silaha dhidi ya Marekani na kuwapatia mfano mbaya watu wa Iraq wanaojitahidi kujenga "serikali ya kidemokrasia".

Vyombo vya habari vinaona kuwa hotuba hiyo ya rais Bush ilitolewa wakati ambapo serikali na Chama cha Republican kimekosa uungaji mkono siku hadi siku, lengo la hotuba hiyo ni kuhamisha ufuatiliaji wa wananchi kutoka dhamira ya kuanzisha vita vya Iraq na kupaka matope Chama cha Republican, ili kukiletea hali nzuri Chama cha Demokrasia kinachopoteza uungaji mkono wa raia siku hadi siku katika uchaguzi wa bunge wa kipindi cha katikati.

Kwanza, askari wa Marekani waliouawa wamezidi 2,200, Marekani inashindwa kujikwamua kutoka Iraq na kiasi cha uungaji mkono wa raia wa Marekani kinashuka siku hadi siku. Uchunguzi wa maoni ya raia uliofanywa wiki iliyopita unasema kwamba asilimia 39 tu ya raia wa Marekani wanaunga mkono sera ya Marekani kuhusu vita vya Iraq, na asilimia hiyo ilikuwa 41 katika mwezi uliopita.

Pili, pamoja na tukio la kusikiliza kisirisiri maongezi ya watu, Chama cha Republican cha rais Bush kinashutumiwa mara nyingi, na chama hicho pengine kitapoteza nafasi ya uongozi katika bunge baada ya miezi kumi. Uchunguzi wa maoni ya raia uliofanyika hivi karibu unaonesha kuwa asilimi 49 ya watu walioulizwa wanatumai kuwa Chama cha Demokrasia kipate nafasi ya uongozi katika bunge, na asilimia 36 tu ya watu walioulizwa wanaunga mkono Chama cha Republican. Kama Chama cha Demokrasia kikishinda katika uchaguzi wa bunge wa kipindi cha katikati, rais Bush atakabiliwa na changamoto kubwa katika bunge. Kwa hiyo mwaka huu ulipoanza tu rais Busha ameanza kupambana na Chama cha Demokrasia.

Chama cha Demokrasia mara kilijibu hotuba ya rais Bush, kikishutumu serikali ya Bush haitaki kusikiliza sauti inayopinga sera yake ingawa inajipamba kwa demokrasia. Mbunge wa Chama cha Demokrasia katika jimbo la Massachusetts Bw. Edward Kennedy alisema, "Kuhusu vita vya Iraq watu waliosema ukweli wanaachishwa kazi au kupuuzwa, lakini watu waliosetiri ukweli na kudhibiti habari wanasifiwa na kuthaminiwa." Bw. Kennedy aliongeza kuwa anakubali moja kwa moja usemi wa Bush "viongozi wanapaswa kuwa wakweli mbele ya vita vya Iraq".

Wachambuzi wanaona kuwa kadiri uchaguzi wa bunge wa kipindi cha katikati unavyokaribia, mvutano unakuwa mkubwa siku hadi siku kati ya vyama vya demokrasia na republican kuhusu vita vya Iraq: Chama cha Demokrasi kitashikilia sera ya vita vya Iraq na kuikosoa serikali ya Bush, na Chama cha Republican kitashikilia "mapambano dhidi ya ugaidi" kudhihaki Chama cha Demokrasia kushindwa kuwa na dawa yoyote ila tu kupiga kelele.

Idhaa ya kiswahili 2006-01-12