Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-12 16:25:28    
Waislamu wa China wapate urahisi kwenda kuhiji huko Makka

cri

Mwezi wa Desemba mwaka 2005 ulikuwa mwezi wa waislamu waishio katika sehemu mbalimbali duniani kwenda Makka, kufanya hija, na kati ya mahujaji milioni moja hivi, walikuwepo waislamu 7000 hivi kutoka China.

Bwana Ma Jingliang ni imam maarufu anayeishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia wa kaskazini magharibi mwa China. Mkoa huo una misikiti zaidi ya 3000, vyuo viwili vya kufundisha misahafu ya kiislamu na shule nyingi za kufundisha lugha ya kiarabu. Imam Ma Jingliang alihitimu kutoka chuo kimoja cha misahafu ya kiislamu. Alisema, idadi ya waislamu wa China wanaokwenda Makka kuhiji inaongezeka mwaka hadi mwaka.

Kila mwaka serikali ya China inawaandaa waislamu kadha wa kadha kwenda kuhiji huko Makka, mwaka 2005 waislamu zaidi ya 1000 waishio katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia walienda Makka kuhiji.

Watu wa makabila 10 nchini China yakiwemo kabila la Wahui, Wawygur, Wahazak, Wasala wanaamini dini ya Kiislamu. Idadi ya jumla ya Wachina wanaoamini dini ya Kiislamu inazidi milioni 20, wanaishi katika sehemu mbalimbali nchini China, na mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia ni mkoa wenye waislamu wengi zaidi kuliko mikoa mingine nchini China. Kwa mujibu wa Koran, waislamu wana nguzo tano muhimu katika maisha yao, na kwenda Makaa kuhiji ni moja ya nguzo muhimu ya dini ya kiislamu. Mkuu wa shirikisho la dini ya kiislamu la mkoa huo Bwana Xie Shenglin alifahamisha:

"Kutokana na maendeleo ya kiuchumi, katika miaka ya karibuni, waislamu wengi zaidi wa China wanatarajia kwenda Makka kuhiji ili kukamilisha nguzo zao za kidini. Na sera huru ya kidini ya China imewapa fursa ya kutimiza matakwa yao."

Mwishoni mwa mwaka 2005, ujumbe wenye mahujaji waislamu zaidi ya 1000 kutoka mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia ulifunga safari ya kwenda Makka kwa ndege maalum. Bi. Fatuma Lin Xianglian mwenye umri wa miaka zaidi ya 40 ni mfanyabiashara hodari anayemiliki kampuni ya nyumba na mkahawa. Alipozungumzia safari yake ya kwenda Makka kuhiji alifurahi sana. Akisema:

"Zamani hatukuweza kuzingatia kwenda Makka kuhiji kutokana na umaskini. Tangu China ifanye mageuzi na kufungua mlango kwa nchi za nje, tumepata maendeleo makubwa ya kiuchumi, hivyo tunaweza kukidhi matakwa yetu."

Bi. Lin alisema gharama za kwenda Makka kuhiji kwa mtu mmoja ni Yuan elfu 30. Waislamu ni hodari wa kufanya biashara, na katika miaka ya karibuni, wanahimizwa kujiendeleza kwa kufanya biashara, hivi sasa waislamu wengi wamekuwa wanaendesha viwanda na kuwa wafanyabiashara maarufu nchini China.

Maendeleo ya kiuchumi na ufuatiliaji wa serikali umewawezesha waislamu wa China waende Makka kuhiji. Tokea mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, shirikisho kuu la dini ya kiislamu la China kila mwaka linaandaa ndege maalum kuwapeleka Makka waislamu wa China. Mkalimani wa Kiarabu na daktari mwislamu walienda pamoja nao ili kuwahakikisha waislamu wa China wasiofahamu lugha ya Kiarabu wanaweza kwenda kuhiji na kuhakikisha usalama wao. Kabla ya waislamu wa China kufunga safari, shirikisho la dini ya kiislamu la China hutuma ujumbe ambao unatangulia kufika nchini Saudi Arabia kupanga makazi, chakula na mawasiliano kwa mahujaji wa China.

Mwaka 2005 serikali ya China kwa mara ya kwanza imefungua njia mpya ya angani ya kwenda nchini Saudi Arabia moja kwa moja kutoka Lanzhou, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia, ili kufupisha safari na kuokoa gharama kwa mahujaji. Mhusika anayeshughulikia mambo ya dini ya mkoa wa Ningxia Bi. Jin Xiaolin alisema:

"Zamani waislamu kutoka mkoa wetu waliokwenda Makka kuhiji walipaswa kufika Beijing kwanza, na kupanda ndege nyingine. Hivi sasa ndege maalum kutoka Lanzhou hadi Saudi Arabia inafanya safari ya moja kwa moja, na kuokoa muda mwingi na gharama kubwa kwa mahujaji."

Idhaa ya kiswahili 2006-01-12