Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-12 19:43:23    
Kwa nini kundi la Hamas halikutaja maneno kuhusu kuiangamiza Israel kwenye ilani yake ya uchaguzi

cri

Uchaguzi wa kamati ya utungaji wa sheria ya Palestina unatazamiwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu, kundi la upinzani la kiislamu la Palestina Hamas litakaloshiriki kwenye uchaguzi huo hivi karibuni, limetangaza ilani yake ya uchaguzi inayoonesha msimamo wake imara kama kawaida, lakini kwa mara ya kwanza ilani hiyo haikutaja mambo kuhusu "lazima kuiangamiza kabisa Israel". Wachambuzi wameainisha kuwa, kundi la Hamas linaeleekea kufuata hali halisi na kuwa fufutende.

Gazeti la Haaretz la Israel tarehe 11 lililichapisha makala ikisema kuwa, katika ilani yake ingawa kundi la Hamas bado limesema litatimiza ukombozi wa taifa la Palestina kwa njia mbalimbali yakiwemo mapambano ya kijeshi, lakini halikutataja msimamo wake wa kikanuni lililoshikilia siku zote kuhusu kuiangamiza Israel na kurudisha sehemu zote za magharibi ya Mto Jordan. Wachambuzi wameainisha kuwa, katika sera ya kidiplomasia mapendekezo ya kundi la Hamas kwenye ilani yake hayana tofauti kubwa na yale ya kundi kuu la chama cha ukombozi wa taifa la Palestina Fatah.

Mapema ya mwanzoni mwa mwaka jana, kundi la Hamas liliwahi kutunga waraka wa kundi hilo, kwa mara ya kwanza lilitambua mstari wa kusimamisha vita kabla ya vita vya mashariki ya kati mwaka 1967 kuwa ni mstari wa mipaka ya siku za usoni wa nchi ya Palestina, na limeahidi kupenda kuboresha uhusiano na nchi mbalimbali duniani hasa nchi za magharibi. Mwishoni mwa mwaka jana, viongozi wa Hamas walitoa ishara ya fufutende mara kwa mara. Kiongozi wa kundi hilo aliyeko katika sehemu ya kanda ya Gaza Bwana Mahmoud Zahar alipohojiwa na waandishi wa habari wa nchi za magharibi alisema, baada ya uchaguzi wa kamati ya utungaji wa sheria, kundi la Hamas litachukua mikakati yenye unyumbufu zaidi, na haliondoi uwezekano wa kufanya mazungumzo na Israel katika siku za usoni. Aidha viongozi wengine wa Hamas walisema, Hamas huenda itaacha mbinu yake ya kufanya milipuko ya kujiua. Wachambuzi wamedhihirisha kuwa kuna mabadiliko hayo ya Hamas katika sera yake, kundi hilo linafanya marekebisho na mpango mpya juu ya maendeleo yake ili kulingana na hali mpya ya kikanda.

Kwa upande wa Israel baada ya maendeleo ya miaka kumi kadhaa, Israel imeweka msingi imara katika sehemu ya mashariki ya kati, na inatambuliwa na nchi nyingi duniani, na malengo ya kimkakati ya Hamas ya kuiangamiza Israel kwa kweli yamekuwa roshani iliyojengwa angani. Hasa katika migogoro kati ya Palestina na Israel iliyofanyika miaka kadhaa iliyopita, mashambulizi ya kijeshi ya Israel yamedhoofisha vibaya hali halisi ya Hamas, viongozi wengi wakuu akiwemo Ahmed Yassin waliangamizwa mmoja baada ya mwingine, na miundo na nguvu halisi ya kijeshi ya kundi la Hamas pia imeharibiwa vibaya. Katika hali hiyo, kundi la Hamas linapaswa kufanya marekebisho ili kulingana na hali halisi ilivyo.

Katika miaka miwili ya hivi karibuni kundi la Hamas linachukua mikakati yenye unyumbufu hatua kwa hatua kwa kushika njia ya kisiasa, safari hii kundi hilo limeamua kushiriki kwenye uchaguzi wa kamati ya utungaji wa sheria, hii imechukuliwa kuwa hatua muhimu ya kutimiza mabadiliko yake.

Msimamo wa kundi la Hamas unaelekea kuwa wa fufutende pia unahusiana na mabadiliko ya hali ya kisiasa katika jamii ya Palestina. Migogoro ya kimabavu iliyofanyika kwa zaidi ya miaka minne imewawezesha wapalestina wengi watambue kuwa, mazungumzo na majadiliano ndiyo njia ya kimsingi ya kutatua mgogoro kati ya Palestina na Israel.