Hivi karibuni Iran iliondoa lakiri zilizowekwa kwenye sehemu tatu zenye zana za nyuklia na kuanzisha upya uzalishaji wa nishati ya nyuklia. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tatu za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wanataka shirika la nishati ya atomiki duniani kuitisha mkutano wa dharura kujadili suala la kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la la Umoja wa Mataifa. Katika wakati huo msimamo wa Russia ulianza kubadilika, na kutoa tamko kwa mara ya kwanza hadharani la "si lazima kupinga kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa". Hivi sasa Iran inakabiliwa na shinikizo kubwa duniani. Hivi karibuni Iran ilitekeleza sera tatu za "kukanusha maneno yaliyopotoka", "kupambana ncha kwa ncha" na "kujiwekea njia ya kujiepusha na matokeo mabaya" ili kukabiliana na mabadiliko ya hali. "Kukanusha maneno yaliyopotoka" ni kuwa Iran inasisitiza tena na tena kutenganisha utafiti wa nishati ya nyuklia na usafishaji wa uranium, ikiwa nchi iliyosaini "mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia", Iran ina haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa njia ya amani. Kwa upande mwingine, Iran ilifanya shughuli nyingi za kidiplomasia za kueleza msimamo wa Iran kuhusu suala la nyuklia: waziri wa mambo ya nje Bw. Manouchehr Mottaki alikwenda Moscow kuwa na mazungumzo na rais Putin, wakati naibu waziri wa mambo ya nje alitembelea Beijing na naibu waziri mwingine wa mambo ya nje alifika Korea ya Kusini. "Kupambana ncha kwa ncha" ni kuhusu kujibu mapigo dhidi ya lawama na tishio la nchi za magharibi. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Motaki alisema, endapo Marekani na Umoja wa Ulaya zinachukua hatua ya kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama, Iran itasimamisha ushirikiano na shirika la nishati ya atomiki duniani. Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alisema, Iran kamwe haitaacha haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa njia ya amani, hata kama suala la nyuklia litawasilishwa kwenye baraza la usalama, Iran haitaacha shughuli zilizoanzishwa upya za utafiti wa nishati ya nyuklia. "kujiwekea njia ya kujiepusha na matokeo mabaya" ni kutoziba njia ya mazungumzo katika siku za baadaye wakati Iran inaposhikilia msimamo wake, inataka Umoja wa Ulaya kuwa na "kichwa baridi" na kumfanya katibu mkuu wa Umoja wa Matiafa Bw. Kofi Annan aeleze nia ya Iran ya "kupenda kuendelea na mazungumzo". Mwakilishi wa kwanza wa Iran katika mazungumzo Bw. Ali Larijani alisema, njia pekee ya kutatua suala la nyuklia la Iran ni mazungumzo.
Wachambuzi wanaona kuwa tangu Bw. Ahmadinejad aapishwe kuwa rais wa Iran, Iran ilitekeleza madai yake hatua kwa hatua, na ilipata mafanikio mara kwa mara. Katika muda usiozidi nusu mwaka, Iran imefaulu kuufanya Umoja wa Ulaya utambue ukweli wa Iran kufanya shughuli za kusafishia uranium, na kuilazimisha Marekani kutambua haki yake ya kutumia nishati ya nyuklia kwa njia ya amani. Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka jana, Iran ilikataa rasmi pendekezo la Umoja wa Ulaya la Iran kuacha uzalishaji wa nishati ya nyuklia kwa "manufaa" ya kuwa na ushirikiano wa kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia, na kuanzisha upya shughuli za kubadilisha uranium.
Tarehe 18 mwezi Septemba, Bw. Mahmaoud Ahmadinejad alitamka, Iran kukubali pendekezo la kuwa na ushirikiano na kampuni za serikali au kampuni binafsi za nchi za nje, na kuanzisha mradi wa kusafisha uranium nchini Iran. Tarehe 18 mwezi Januari mwaka huu, kabla ya kurudisha mazungumzo na Umoja wa Ulaya, Iran ilianzisha upya utafiti wa kusafisha uranium tarehe 10. Hivi sasa Iran inasema, kubadilisha na kusafisha uranium. Hivi sasa Iran inasema kuwa utafiti wa kubadilisha na kusafisha uranium haupo katika eneo la mazungumzo, maana ya maneno hayo ni kuwa, mambo yatakayozungumziwa katika mazungumzo ya siku za mbele ni kuhusu suala la uzalishaji wa uranium nzito.
Hivi sasa Umoja wa Ulaya umeamua kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na kubatilisha mazungumzo yaliyopangwa hapo awali yatakayofanyika tarehe 18.
|