Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-16 20:24:03    
Jumba la Makumbusho ya Filamu za China Lazinduliwa

cri

  

Wakati China inapoadhimisha miaka mia moja toka ianze kutengeneza filamu, siku chache zilizopita jumba la makumbusho ya filamu za China limezinduliwa mjini Beijing. Wasanii wa nyanja mbalimbali na wapenda filamu wengi walihudhuria uzinduzi huo. Meya wa Beijing, Bw. Wang Qishan kwenye uzinduzi alisema,

"Maendeleo ya filamu za China yanahusiana moja kwa moja na maendeleo ya mji wa Beijing. Mwaka 1905 filamu ya kwanza ya China ilitengenezwa mjini Beijing, tokea hapo historia ya filamu za China ilianza safari yake. Leo miaka mia moja baadaye, jumba la kwanza la makumbusho ya filamu za China limezinduliwa hapa Beijing. Hili ni jambo la maana sana katika historia ya filamu za China. Jumba hili ni jukwaa la maingiliano ya utamaduni wa filamu za China na pia ni mfano wa nyayo za maendeleo ya filamu za China, uzinduzi wa jumba hili umefungua ukurasa mpya wa maendeleo ya filamu za China."

Jumba la makubusho ya filamu za China liko kwenye kiunga cha Beijing upande wa mashariki. Eneo lake ni mita za mraba elfu 40, jumba hilo ni kubwa sana kwa eneo kuliko majumba mengine ya namna hiyo duniani. Sura ya jumba hilo kwa nje ni kama boksi kubwa jeusi likiashiria mashine ya kupigia picha za filamu na sinema. Kwenye uwanja mbele ya jumba hilo zimesimamishwa fremu kumi nyeusi za mraba zilizofungamana, kuta za jumba zimepambwa kwa nyota nyingi zikimaanisha nyota zisizoweza kukosekana katika dunia ya filamu.

Ndani ya jumba hilo kuna kumbi 21, ambazo jumla ya maeneo ni karibu mita za mraba elfu 10. Kumbi hizo zimegawanyika katika kazi tofauti, kwamba licha ya kuonesha maendeleo ya filamu za China pia zina ukumbi wa maingiliano ya utamaduni wa filamu, ukumbi wa kuonesha filamu, ukumbi wa kufanyia utafiti na ukumbi wa burudani. Mkuu wa Idara ya Taifa ya Redio, Filamu na Televisheni Bw. Wang Taihua alisema,

"Jumba la makumbusho ya filamu za China litatoa huduma ya utamaduni wa filamu kwa wote, kwa kufanya shughuli za aina mbalimbali za utamaduni wa filamu za China linaonesha nyayo za maendeleo ya filamu za China, maandishi muhimu na watu mashuhuri katika sanaa ya filamu, na kufumbua maajabu ndani ya filamu, ili kulifanya jumba hilo licha ya kuonesha mafanikio ya filamu za China pia litachangia maendeleo ya filamu na kustawisha maingiliano ya kimataifa ya utamaduni wa filamu."

Katika jumba hilo, zimeoneshwa picha na vitu vya zamani zaidi ya elfu 6 vinavyohusika na filamu zaidi ya 1500, na kuna skrini za kuonesha filamu 260.

Katika ukumbi wa kuonesha maendeleo ya filamu, watazamaji licha ya kuweza kuona jinsi filamu ya kwanza ilivyopigwa, pia wanaweza kuona filamu ya kwanza duniani ilivyopigwa na ndugu wawili Limiere wa Ufaransa mwaka 1895. Ili kuwafahamisha watazamaji jinsi filamu ya kwanza ilivyotokea dniani, mashine ya kupigia filamu ambayo ni ya zamani sana duniani, ambayo pia ni mashine iliyotumiwa na ndugu wawili Lumiere inaoneshwa. Studio ya kutengenezea filamu ya Tianjin ilitoa mashine mbili za zamani ambazo ziliwahi kurekodi hali ya vita vya kupambana na wavamizi wa Japani na sherehe ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

Vitu vya zamani vya kutengenezea filamu, sanamu za nta, sanamu za ufinyanzi na kielelezo cha mazingira yaliyokuwa zamani ya kutengeneza filamu na maonesho ya filamu, na matangazo ya filamu yameonesha kwa pande zote historia ya maendeleo ya filamu za China. Filamu "Mtu Afikapo Umri wa Makamo" iliyopigwa mwaka 1982 ilipooneshwa iliwagusa sana watazamaji. Filamu hiyo pamoja na picha za filamu hiyo pia zimeoneshwa ndani ya jumba hilo. Mwigizaji muhimu wa filamu hiyo Pan Hong alipohojiwa na waandishi wa habari alisema,

"Tunaichukulia kazi ya filamu kuwa ni kazi ya maisha yetu yote, ni fahari yangu kwamba filamu moja kati ya filamu kumi kadhaa nilizochezea inahifadhiwa katika jumba hilo. Filamu sio mali ya mwigizaji binafsi bali ni mali ya jamii, ni mali ya watu wote."

Mwigizaji mashuhuri Wang Tiecheng aliwahi kumwigiza waziri mkuu Zhou Enlai katikia filamu, uigizaji wake umewaachia watazamaji kumbukumbu kubwa. Alisema,

"Jumba la makumbusho ya filamu za China sio limeeleza historia ya miaka mia moja ya filamu za China, lakini limeonesha jinsi mwanzo ulivyokuwa mgumu na watu walioshughulikia filamu walivyokumbwa na shida. Nahakika kwamba kadiri jumba hilo linavyoendelea kuongeza kumbukumbu nyingi ndivyo litakuwa na thamani kubwa zaidi."

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-16