Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-18 16:47:53    
Kusamehe karo za wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kumewapunguzia mzigo yuan bilioni 15 nchini China

cri

Tarehe 27 ofisa wa Wizara ya Fedha ya China alisema, Baraza la Serikali ya China imetangaza kuwa kuanzia mwaka 2006 wanafunzi wa sehemu ya magharibi ya China wanasamehewa karo za shule za msingi na za sekondari, na sera hiyo itaenea hadi sehemu ya katikati na ya mashariki ifikapo mwaka 2007. Hatua hiyo inayowahusu wananchi moja kwa moja, itawapunguzia mzigo wa yuan bilioni 15, kwa wastani kila mwanafunzi wa shule ya sekondari yuan 180 na mwanafunzi wa shule ya msingi 140.

Ofisa huyo alieleza kuwa katika miaka ya karibuni, mageuzi ya kuwapunguzia kodi wakulima yanavyoendelea kwa kina, mfumo wa fedha unavyokamilishwa zaidi na kuongeza mfululizo fedha za elimu katika bajeti kimekuwa chanzo muhimu cha fedha za elimu vijijini. Mwaka 2004 fedha kwa ajili ya elimu vijijini ziliongezeka na kufikia yuan bilioni 132.6 katika bajeti, ikiwa ni ongezeko la yuan bilioni 79.3 kuliko mwaka 1999 mageuzi ya kuwapunguzia kodi wakulima yalipoanza, kwa wastani kila mwaka kuna ongezeko la 20%, wanafunzi maskini waliofaidika wamefikia milioni 34 katika sehemu ya katikati na ya magharibi ya China.

Kadhalika ofisa huyo alisema katika juhudi za kuwapunguzia mzigo wakulima, cha kwanza ni kuondoa karo za shule kwa watoto wao. Kuondoa karo za wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ni hatua muhimu ya serikali kuu ya China kwa kuzingatia hali ya jumla nchini China, na pia ni hatua nyingine muhimu baada ya sheria ya kuondoa kodi za kilimo. Ili kuhakikisha hatua hiyo inatekelezwa, Baraza la Serikali ya China imeamua kuitekeleza sehemu baada ya sehemu na kukamilisha katika muda wa miaka miwili. Mwaka kesho, mikoa ya magharibi pamoja na mikoa mitatu ya katikati inayofaidika na sera sawa na mikoa ya magharibi itaondoa karo za shule za msingi na sekondari, mwaka 2007 elimu vijijini katika sehemu ya katikati na ya mashariki itaondolewa karo hizo.

Wizara ya Fedha ya China inataka katika mwaka 2006 idara zianzishwe ili kuhakikisha hatua hiyo inatekelezwa kwa kanuni za "majukumu yawe wazi kwa kila ngazi, serikali kuu na serikali za mitaa zibebe gharama kwa pamoja, kuongeza fedha katika elimu na kutekeleza hatua hiyo kutoka sehemu hadi sehemu", na idara zote za fedha za ngazi mbalimbali zinatakiwa ziwajibike vilivyo na kutekeleza kwa hatua madhubuti.

Kwanza, lazima zihakikishe wanafunzi wa familia zilizopata dhamana ya maisha ya kiwango cha kichini wanasamehewa karo kwa mujibu wa sera zilizotolewa na serikali.

Pili, ihakikishwe kuwa fedha za msaada kwa shule baada ya kuondoa karo za wanafunzi zifikie mahali panapokusudiwa, ni marufuku kuathiri shughuli za kawaida shuleni.

Tatu, mapato ya shule za msingi na sekondari vijijini lazima yakaguliwe na ni marufuku kuwatoza pesa ovyo wanafunzi. Pamoja na hayo serikaliya China ilifanya kazi ya kuwasamehe wanafunzi gharama za vitabu vya kiada na msaada wa bweni na maisha yao, ili kila mwanafuzi maskini anufaike na elimu ya lazima.

Idhaa ya kiswahili 2006-01-18