Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-18 19:36:53    
Mapishi ya vipande vya nyama ya ng'ombe na pilipili manga nyeusi

cri

Mahitaji

Vipande vya nyama ya ng'ombe gramu 500, kitunguu gramu 200, pilipili hoho gramu 10, mchuzi wa soya gramu 10, vitunguu saumu gramu 25, ute wa yai moja, wanga 15, pilipili manga nyeeusi gramu 8, mvinyo wa kupikia gramu 5, mafuta ya ufuta gramu 5, sosi ya nyanya gramu 20, chumvi gramu 5, sukari gramu 5, mafuta gramu 500

Njia

1. weka vipande vya nyama ya ng'ombe kwenye bakuli moja pamoja na mchuzi wa soya, mvinyo wa kupikia, ute wa yai, viunge kwa pamoja na uchemshe kwa dakika 30.

2. tia mafuta kwenye sufuria pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia vipande vya nyama ya ng'ombe korogakoroga na kisha vipakue. Tia vipande vya vitunguu na chumvi korogakoroga, vipakue.

3. Pasha moto tena, tia vipande vya pilipili hoho na vitunguu saumu, korogakoroga halafu tia vipande vya nyama ya ng'ombe, vitunguu, pilipili manga nyeusi, mchuzi wa soya, sukari, sosi ya nyanya, korogakoroga, halafu tia mafuta ya ufuta, maji ya wanga, korogakoroga kwa haraka kisha pakua. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.