Tangu Marekani kueleza mashaka yake kuhusu matumizi ya amani ya mpango wa nyukilia wa Iran, suala hilo limekuwa na utata mwingi sana, licha ya kwamba suala hilo lenyewe ni lenye utata mwingi, mvutano kati ya mataifa makubwa yanayofuatilia maslahi yake umezidisha matatizo ya suala hilo.
Vyombo vya habari vinaona kuwa Marekani ni nchi iliyozusha suala la nyukilia la Iran. Kutokana na maslahi ya kimkakati katika sehemu ya mashariki ya kati, Marekani inachukulia Iran kuwa moja ya nchi muhimu zenye uovu duniani kwa minajiri kuendeleza silaha za nyukilia na kutishia usalama wake., hivyo inajitahidi kwa kila iwezalo kubomoa zana za nyukilia za Iran. Vitendo hivyo vya kimabavu vimechochea hisia za uzalendo za watu wa Iran na hisia za kuipinga Marekani. Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia hivi karibuni iliilaani hali ambayo Marekani inaipendelea Israel na kuiruhusu kuwa na silaha za nyukilia, kwa hiyo suala la nyukilia la Iran haliwezi kutatuliwa bila malalamiko. Mratibu mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki Bw. Mohamed El Baradei aliwahi kusema, utatuzi wa mwisho wa suala la nyukilia la Iran ni kupata ahadi iliyotoa Marekani juu ya usalama wa Iran.
Iran imepata funzo kubwa kutokana na vita kati yake na Iraq, vita vya ghuba na vita vya Afghanistan, na inaona tishio kubwa dhidi ya usalama wake. Kutokana na kukabiliwa na sera za uhasama mkubwa za Marekani, Iran inaona mbinu nzuri na ya uhakika ni kuwa na teknolojia ya nyuklia. Watu wengi nchini Iran wanaona kuwa, kuwa na teknolojia ya nyukilia na kuwa taifa lenye nguvu ni vitu viwili visivyoweza kutengana. Hii ndiyo sababu ya kuungwa mkono hivi karibuni nchini Iran kwa sera zake za kithabiti. Hivi karibuni rais Mohamed Ahmadinejad wa Iran alisema, nchi za magharibi hazitaki kutuuzia hata dawa ya kuokoa uhai wetu, tunaweza kuwaamini kutupatia daima nishati ya nyukilia? Tafsiri ya maneno hayo ni kuwa Iran lazima iwe na uwezo wa kuzalisha nishati yenyewe.
Umoja wa Ulaya una wasiwasi kuwa pindi Iran ikipata teknolojia ya nyukilia, huenda italeta hatari ya kutoa silaha za nyuklia kwa magaidi, hatua ambayo itatishia usalama wake na maslahi yake kwenye mashariki ya kati. Lakini tofauti na Marekani ni kwamba Umoja wa Ulaya una wazo zaidi la kutatua mgogoro wa kimataifa kwa njia za kidiplomasia na amani. Mbali na hayo, sera za Umoja wa Ulaya kuhusu Iran ni kuhusu maslahi yake ya kiuchumi. Iran ni nchi mwanachama muhimu wa OPEC, pindi ikisimamisha usafirishaji wa mafuta ya asili ya petroli kwa nje kutokana na vita, uchumi wa nchi za Umoja wa Ulaya utakuwa wa kwanza kukumbwa na pigo kubwa. Hivyo Umoja wa Ulaya ulijituma kwenda kufanya mazungumzo na Iran. Hata hivi sasa unapotaka baraza za usalama la Umoja wa Mataifa kushughulikia suala la nyukilia la Iran, Umoja wa Ulaya bado haujafa moyo kuhusu uwezakano wa kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw Frank-Walter Steinmeier alisema, pamoja na uingiliaji wa baraza la usalama, suala la nyukilia la Iran litaingia katika kipindi kipya, lakini hii haimaanishi kusimama kwa mazungumzo. Umoja wa Ulaya umeanza kuwa na wazo la kutatua suala hilo kwa muda mrefu na kuhusu ugumu wa utatuzi wa suala hilo.
Iran ni nchi muhimu sana kwa mikakati na maslahi ya kiuchumi ya Russia. Nchi hizo mbili zimekuwa na miradi mingi ya ushirikiano kuhusu nishati ya nyukilia, mambo ya kijeshi na safari ya ndege. Hivyo toka siku nyingi zilizopita, Russia ni kama mtetezi wa Iran. Baada ya kukwama kwa mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Iran, Russia iliingilia kati suala hilo kama msuluhishi na kutaka Iran ihamishie shughuli za kusafisha uranium nchini Russia. Lakini Iran haikukubali kufanya hivyo, badala yake ilianzisha upya utafiti wa nyukilia unaohusika na usafishaji wa uranium, jambo ambalo limeiudhi Russia.
Mgogoro wa nyukilia wa Iran umefika kwenye njia panda. Wachambuzi wanaona kuwa utatuzi wa suala la nyukilia la Iran utapita kwenye njia ndefu, na utatuzi wa amani wa suala hilo pia utakuwa na uwezekano wakati wowote.
|