Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-20 18:28:33    
Iran na Syria zashirikiana kukabiliana na shinikizo la Marekani

cri

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 19 alifika Damascus, mji mkuu wa Syria kwa ziara ya siku mbili . Hii ni mara ya kwanza kwa rais Ahmadinejad kuitembelea Syria tangu achaguliwe kuwa rais wa Syria, na huu pia ni mkutano wa pili wa wakuu wa Iran na Syria katika muda usiofikia nusu mwaka. Waandishi wa habari wameona kuwa, nchi hizi mbili zinaimarisha mshikamano na kusaidiana chini ya shinikizo kubwa la Marekani na nchi za magharibi.

Tokea miaka ya 70 ya karne iliyopita Iran na Syria zilianza kuimarisha siku hadi siku uhusiano kati yao, baadaye uhusiano huo ukaendelea kuwa wa shirikisho la kimkakati. Sababu kubwa ni kutokana na nchi hizo mbili zote kuilaani vikali sera ya Marekani ya umwamba na upanuzi katika sehemu ya mashariki ya kati, na kuhusu mchakato wa amani ya mashariki ya kati, nchi hizo mbili siku zote zinashikilia msimamo imara wa kupinga Marekani. Hivi sasa Iran na Syria zinakabiliwa na shinikizo kubwa la nchi za magharibi zinazoongozwa na Marekani kutokana na suala la nyuklia la Iran na tukio la kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, hivyo nchi hizo mbili zinaimarisha ushirikiano kati yao ili kukabiliana kwa pamoja na shinikizo la nje, ambapo pia zina matakwa halisi ya dharura zaidi ya kubadlisha hali ya kuwepo kwa nchi hizo mbili.

Hali ya Iraq ni suala muhimu zaidi kuliko mengine katika mazungumzo ya marais wa nchi hizo mbili. Syria na Iran zote ni nchi jirani za Iraq, baada ya vita vya Iraq, askari zaidi ya laki moja wa jeshi la Marekani wameingia kwenye sehemu ya kiini cha mashariki ya kati, na kuwa tishio la moja kwa moja dhidi ya usalama wa Syria na Iran. Na baada ya vita vya Iraq, baada ya siku chache tu, Marekani iliongeza shinikizo dhidi ya Syria na Iran, na kuzilaani nchi hizo mbili kuunga mkono ugaidi, kuendeleza silaha kali na kuharibu utulivu wa Iraq, hata Marekani ilitishia kutumia nguvu dhidi yao.

Kuhusu lawama kutoka Marekani, rais Bashar al Assad wa Syria na rais Ahmadinejad wa Iran tarehe 19 baada ya mazungumo, walisema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, nchi hizo mbili zinaunga mkono Iraq juu ya mchakato wake wa kisiasa na juhudi zake zote kwa kutimiza utulivu. Walidhihirisha hasa kuwa utulivu wa Iraq ni sharti la kwanza la utulivu wa hali ya kikanda, hali isiyo ya usalama kutokana na mashambulizi ya kimabavu yaliyotokea bila kusita itaweza tu kuchukuliwa kuwa kisingizio cha nchi za nje kwa kudumisha ukaliaji wao nchini Iraq. Majeshi ya nchi za nje yatakapoondoka Iraq, ndipo serikali ya Iraq itakapoweza kupambana kwa nguvu na ugaidi na kutimiza usalama wa Iraq. Vyombo vya habari vinaona kuwa, msimamo huo ulioelezwa na marais hao wawili ni sawasawa na msimamo ule wa nchi hizo mbili katika kupinga kuwepo kwa jeshi la Marekani katika sehemu ya mashariki ya kati.

Kuhusu suala la mashariki ya kati, marais hao wawili wameahidi kuunga mkono haki halali ya wananchi wa Palestina ya kuanzisha nchi yenye uhuru ambayo mji mkuu wake ni Jerusalem. Nchi hizo mbili zikiwa nchi zenye msimamo imara kuhusu suala la amani ya mashariki ya kati, zinaendelea kusisitiza kuwa mapambano ni mbinu pekee ya wananchi wa Palestina katika kurudisha haki halali na kukomesha ukaliaji wa Israel kwenye ardhi takatifu ya kiislamu. Na kuhusu suala la nyuklia la Iran na uhusiano wenye hali wasiwasi kati ya Syria na Lebanon, Iran na Syria, kila upande umeahidi kuunga mkono upande mwingine. Rais Bashar wa Syria amesisitiza kupinga kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na Syria inaunga mkono haki ya Iran ya kutumia kiamani nishati ya nyuklia, na kukubali kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo.