Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-20 20:30:10    
Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wenye lengo la kunufaishana na kupata maendeleo ya pamoja kati ya China na Afrika

cri
Ofisa wa Wizara ya Biashara ya China tarehe 10 alisema, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika siku zote unafanyika kwa msingi wa kunufaishana na kupata maendeleo ya pamoja. Madhumuni ya China ya kuanzisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati na Afrika ulio wa usawa, kuaminiana, na kunufaishana ni kupata maendeleo ya pamoja ya kiuchumi na wananchi wa Afrika.

Mkurugenzi wa Ofisi ya uchunguzi kuhusu mambo ya Afrika katika Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bibi He Wenping alisema, vyombo vya habari vya nchi za magharibi vilisema China inafanya "Ukoloni mambo leo" barani Afrika, hii imepotosha ukweli wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika. Nchi za magharibi zilinyang'anya maliasili kwa muda mrefu barani Afrika, lakini China siku zote inasisitiza kutafuta maendeleo ya pamoja na nchi za Afrika. Bibi He alitoa mfano kwamba, nchi inayozalisha mafuta kwa wingi barani Afrika Nigeria haina zana yoyote ya kusafisha mafuta baada ya nchi za magharibi kunyang'anya maliasili nchini humo kwa miaka mingi. Kinyume chake, China imetoa misaada kuanzisha viwanda vingi vikubwa barani Afrika, na kutoa misaada ya teknolojia na fedha zinazohitajika katika nchi za Afrika.

Takwimu kutoka forodha ya China zinaonesha kuwa, katika miaka mitano iliyopita, thamani ya biashara kati ya China na Afrika imeongezeka hadi kufikia dola za kimarekani zaidi ya bilioni 37 kwa mwaka kutoka dola bilioni 10, na mitambo ya umeme, bidhaa za teknolojia mpya za hali ya juu zimepata maendeleo ya kasi zaidi, na kuchukua karibu nusu ya thamani ya jumla ya bidhaa za China zinazouzwa barani Afrika. Mwaka 2006 China itaendelea kuongeza uuzaji wa bidhaa zenye thamani kubwa barani Afrika.

Katika miaka ya hivi karibuni, thamani ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Afika kuja nchini China imekuwa ikizidi ile ya bidhaa zinazouzwa barani Afrika, hii imeziwezesha nchi za Afrika kupata fedha nyingi za kigeni. Ili kusaidia bidhaa za Afrika ziingie katika soko la China, kuanzia tarehe 1 Januari mwaka 2005, China imetoa sera ya kusamehe ushuru wa aina 190 za bidhaa za nchi 28 za Afrika zilizoko nyuma kiuchumi zinazouzwa nchini China, na uuzaji wa bidhaa nyingi za nchi za Afrika nchini China umepata faida kutokana na sera hiyo. Mwaka jana thamani ya bidhaa za nchi za Afrika zinazouzwa nchini China iliongezeka kwa zaidi ya mara moja.

Ofisa wa Wizara ya Biashara alisema, bidhaa za China zenye sifa bora na bei nafuu zimevunja hodhi ya uuzaji wa bidhaa za nchi za magharibi barani Afrika, kuingiza aina nyingi za bidhaa barani Afrika na kuinua kiwango ya maisha cha waafrika. Ongezeko la thamani ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Afrika linachagia uwiano wa biashara kati ya China na Afrika, na kusaidia nchi za Afrika kupata ongezeko la mapato, na kutoa mchango kwa uchumi wa Afrika. Mashirika ya China yaliyoanzishwa barani Afrika yametoa nafasi nyingi za ajira na kuongeza mapato ya ushuru ya nchi yaliyoko, kuleta teknolojia na wataalamu na kuinua uwezo wa uzalishaji wa nchi hizo, na kuhimiza China na nchi mbalimbali za Afrika zipate maendeleo ya pamoja.

Mashirika ya China yanayowekeza vitega uchumi barani Afrika yamepata maendeleo makubwa kutokana na uhamasishaji wa serikali ya China. Katika miezi 10 ya mwanzo ya mwaka jana, thamani ya uwekezaji wa mashirika ya China katika nchi mbalimbali za Afrika ilifikia dola za kimarekani milioni 175, kiasi ambacho kinachukua moja ya kumi (1/10) ya thamani ya jumla ya uwekezaji wa China barani Afrika katika miaka mingi iliyopita. Mashirika hayo yanashughulikia biashara, uzalishaji na utengenezaji, uendelezaji wa maliasili, mawasiliano na uchukuzi, kilimo na utengenezaji wa mazao ya kilimo.

Kampuni ya almasi ambayo ni kampuni binafsi ya China inaziuzia nchi za Afrika vyerehani viwandani zenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 kwa mwaka, na kuanzisha ofisi katika nchi nyingi barani Afrika. Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Ruan Xiaoming alisema, kampuni hiyo inaheshimu mila na desturi, kanuni na sheria za nchi za Afrika, na kufanya utafiti na uvumbuzi juu ya aina mpya za bidhaa na teknolojia kutokana na mahitaji ya sehemu mbalimbali barani Afrika, na kuajiri wenyeji wengi wa huko. Hivi sasa kampuni hiyo imekuwa na wafanyakazi 50 wa Afrika, na kampuni hiyo ina mpango wa kuhamishia kiwanda cha kutengeneza bidhaa barani Afrika kutoka China.

Kama Bw. Ruan alivyofanya, wafanyabiashara wengi wa China wanapenda kwa dhati kugawana faida na nchi wenyeji za Afrika, na kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika unaopata faida za pamoja. Bw. Liu Jianjun wa mkoa wa Hebei, China aliongoza wataalamu wa kilimo wa China kuanzisha mradi wa ushirikiano wa kilimo nchini Mali. Kutokana na mradi huo, hali ya nchi hiyo ya kutegemea nchi za nje katika sekta ya mboga ilikomeshwa, bei ya mboga ilipungua kwa zaidi ya nusu, na kuwaletea wananchi wa maslahi.

Mjumbe wa uratibu wa Umoja wa Mataifa nchini China Bw. Ma Heli alisema, ingawa mashirika ya China yameingia katika soko la Afrika kwa muda mfupi, lakini China na nchi za Afrika zina sifa ya pamoja ya kuthamini urafiki, na huo ni umaalum wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika.

Ili kuweka mazingira mazuri ya sera na sheria kwa uwekezaji wa mashirika ya China barani Afrika, serikali ya China imesaini Makubaliano ya kuhimiza na kuhakikisha uwekezaji na nchi 28 za Afrika, kuanzisha kamati ya pamoja ya uchumi na biashara na nchi 35 za Afrika, na kusaini Makubaliano ya kukwepa kutoza kodi mara mbili na nchi 8 za Afrika. Mwaka huu China itasaini makubaliano kama hayo na nchi nyingi zaidi za Afrika. Hivi sasa nchi 16 za Afrika zimeanza kupokea watalii kutoka China, na idadi ya wachina wanaofanya utalii barani Afrika imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, na kutoa fursa nyingi zaidi za biashara kwa nchi za Afrika.

Mwezi Septemba mwaka jana, rais Hu Jintao wa China alitoa hatua tano muhimu zenye lengo la kuendeleza uhusiano na nchi zinazoendelea, na nchi za Afrika zimekuwa sehemu muhimu zinazonufaishwa. Ofisa wa Wizara ya Biashara ya China alisema, mwaka huu China itatekeleza hatua hizo kwa vitendo halisi, na kuongeza nguvu kutoa misaada kwa nchi za Afrika, kuimarisha ushirikiano katika sekta ya nguvu kazi, na kuendelea kutekeleza sera ya kusamehe ushuru wa baadhi ya bidhaa za nchi zile za Afrika zilizoko nyuma kiuchumi duniani na zinazouzwa nchini China.

China imeahidi kutoka mafumo ya kitaalam kwa watu elfu 10 wa nchi za Afrika katika muda wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2004 hadi 2006. Katika miaka miwili iliyopita, China imeongeza kwa mara kadhaa fedha zinazotumiwa katika kutoa mafunzo ya utaalamu kwa waafrika, na kuanzisha utaratibu wa uratibu wa ushirikiano wa uendelezaji wa nguvu kazi na nchi za nje, na kuwapokea watu zaidi ya 6000 kutoka Afrika kupata mafunzo nchini China.

Ofisa wa Wizara ya Biashara alisema, ni wajibu wa kimataifa kwa China kuzisaidia nchi za Afrika kuondoa umaskini na kupata usitawi. Na kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika sekta ya uchumi na biashara kumekuwa maoni ya pamoja kati ya China na nchi mbalimbali za Afrika.

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-20