Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-20 21:34:43    
Ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa wa Tanzania kwa msaada wa China kukamilika

cri
Hivi karibuni mtangazaji wetu alipata fursa ya kufanya mahojiano na Bwana Rish Urio mratibu wa ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa wa Tanzania unaojengwa huko Dar es salaam kwa msaada wa serikali ya Jamhuri ya watu wa China, aliyekuwepo ziarani hapa China. Mtangazaji wetu alianza kwa kumwuliza Bwana Urio lengo ziara yake hapa China.

Bw Urio

Tumekuja hapa China kwa ajili ya semina inayohusu mambo ya michezo, hasa inayohusu misaada inayotolewa na serikali ya China inatoa misaada kwa nchi zinazoendelea, ikiwa ni kuhusu usimamizi na uendeshaji wa michezo, hasa utunzaji wa viwanja vya michezo na ujenzi wa viwanja hivyo vya michezo kwa nchi ambazo hazijajenga au nchi zenye nia ya kujenga viwanja hivyo, na namna ya kuendesha shughuli hizo sio tu kwa ajili ya michezo lakini pia kwa ajili ya biashara.

Mtangazaji

Semina hii imezihusisha nchi ngapi, nikiwa na maana ni China na nchi zipi?

Semina hii imehusisha nchi zote duniani, tulikuwa tunategemea tuwe nchi zaidi ya 40, lakini pamoja na China tumekuwa nchi 30, na tumekuwa tukijadili maendeleo ya michezo na maendeleo ya kiuchumi yanayotokana na mambo ya michezo.

Mtangazaji:

Labda ungefafanua kidogo maana ya maendeleo ya michezo na maendeleo ya kiuchumi yanayotokana na mambo ya michezo

Bw Urio

Unajua sasa hivi karibu nchi zote duniani zinatekeleza azimio la umoja wa mataifa linalohusu vipengele nane vya mpango wa maendeleo ya milenia MDG. Moja ya vipengele hivyo vinasisitiza kuendeleza michezo kwa ajili ya afya, na michezo kwa ajili ya ushindani na kupata nishani, lakini pia sasa tutumie michezo kwa ajili ya kuleta faida za kiuchumi. Tumekuwa tukitumia michezo kwa ajili ya watu kushindana tu na kuweza kuleta medali na kwa ajili ya watu binafsi kujinufaisha kwa kushiriki kwenye michezo mbalimbali ya kimataifa kama michezo ya jumuiya ya madola na michezo ya olimpiki, tumekuwa tukileta faida ndogo kwa wale waliokuwa wanaweza kushinda. Lakini sasa tumefikia mahali ambapo sasa tunataka michezo isaidei kuinua uchumi. Sasa hivi tunajenga hili eneo changamani, (yaani uwanja wa Taifa unaojengwa kwa msaada wa serikali ya China), hapo tunaelekea kweli lengo la kufanya michezo iwe kwa burudani kwa mashindano pamoja na kuleta faida za kiuchumi. Kwa sasa tunakazana ili kujiaanda kwa ajili ya mashindano ya mwaka 2010 ya kombe la dunia yatakayofanyika kule Afrika ya kusini, tunategemea kuwa huduma zitakazokuwepo kwenye uwanja huo zinaweza kutolewa kwa wale watakaoshiriki kwenye mashindano hayo ya Kombe la dunia huko Afrika ya kusini ambapo ni muda wa saa tatu tu kwa ndege, hapo tunaweza kupata faida nyingi za kiuchumi. Mbali na hilo tutatumia uwanja huo kutusaidia kufanya kila tunaloweza kutega uchumi kwa kila njia tunayoweza kwa kutumia michezo. Kwa sasa hilo ndio tunalofanya.

(itaendelea)

Idhaa ya Kiswahili 2006-01-20