Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-23 15:03:45    
Mradi wa kuokoa urithi wa utamaduni wa jadi wapata mafanikio makubwa katika uchapishaji

cri

Shirikisho la China la Wasanii wa Sanaa na Fasihi za Wenyeji lilianzisha mradi wa kuokoa urithi wa utamaduni wa jadi kuanzia mwaka 2003. Miaka miwili imepita tangu mradi huo unzishwe, mafanikio makubwa yamepatikana katika uchapishaji.

China ni nchi yenye eneo kubwa na historia ndefu. Miongoni mwa wananchi na kwenye maisha yao ya kila siku kuna utamaduni mkubwa, lakini kadiri jamii inavyoendelea kuwa ya kisasa, urithi wa utamaduni wa jadi unazidi kuwa katika hatari ya kutoweka, na sanaa nyingi zilizo bora zimeanza kunyauka kutokana na kukosa msingi unaofaa. Mwanzoni mwa mwaka 2003 Shirika la China la Wasanii wa Sanaa na Fasihi za Wenyeji lilianzisha mradi wa miaka kumi wa kuokoa utamaduni wa jadi. Kutokana na mpango, mradi huo utashughulikiwa kwa maandishi, kurekodi, kupiga picha na kupiga picha za video kukusanya na kuhifadhi sanaa zinazowakilisha mila na desturi, kusajili na kuchapicha vitabu vya picha zilizochorwa na wenyeji, na kuanzisha ghala la kumbukumbu za mila na desturi kwa maandishi na picha. Hii ni mara ya kwanza kwa mradi kama huo kufanyika nchini China.

Kuanzia mwezi Machi mwaka huu, baadhi ya mafanikio ya mradi huo yameanza kuchapishwa. Naibu katibu mkuu wa Shirikisho la China la Wasanii wa Sanaa na Fasihi za Wenyeji Bw. Xiang Yunju alieleza, "Kwa kutumia sayansi na teknolojia ya juu, kazi kabambe ya kufanya uchunguzi, kurekodi, kuratibu na kuokoa urithi uliokuwa hatarini kutoweka, imeanza kupata mafanikio kwa kuchapisha vitabu.

Shirika la Uchapishaji la Zhonghua lenye miaka 94 linajulikana kwa kuchapisha vitabu vya utamaduni wa jadi. Shirika hilo limechapisha kitabu cha "Picha za Mwaka Mpya za Kuchongwa ? Sehemu ya Yangjiabu" ambacho ni kitabu cha kwanza kabisa katika mradi huo. Picha za kusherehekea mwaka mpya zimekuwa na miaka zaidi ya 300 katika sehemu ya Yangjiabu mkoani Shandong. Picha za huko zinajulikana nchini China na nchi za nje kwa mtindo wake unaovutia na sanaa ya hali ya juu. Kitabu hicho kimepata tuzo ya uchapaji iliyotolewa na Marekani mwaka 2005. Inasemekana kuwa Shirika hilo la uchapishaji limebeba jukumu la kuchapicha seti yenye juzuu 20 za picha za kuchongwa, seti hiyo itagharimu yuan milioni mbili. Mhariri mkuu wa shirika hilo Bw. Li Yan alisema, "Utamaduni miongoni mwa wenyeji ni aina moja ya utamaduni wa jadi, ni wajibu wetu wa lazima kuhariri na kuchapisha. Seti ya juzuu za picha za kuchongwa za China ni mradi mgumu kuanzia kufanya uchunguzi wa kina hadi kuratibu na kuchapisha. Tutachapisha juzuu hizo ambazo daima hazitaonekana zimepitwa na wakati kwa uzuri wake."

Seti ya juzuu za hadithi za jadi iliyochapishwa na Shirika la Hakimiliki na Shirika la China la Wasanii wa Sanaa na Fasihi kwa pamoja imechapishwa kwa juzuu 12 za hadithi simulizi zilizopatikana kutoka wilaya 12 za sehemu ya Dali inayojitawala ya kabila la Wabai mkoni Yunnan, juzuu hizo zina maneno milioni 40. Kutokana na mahali ilipo kijiografia, sehemu ya Dali mkoani Yunnan ni makutano ya utamaduni wa China na utamaduni wa India katika zama za kale na kuufanya utamaduni pekee wa kabila la Wabai. Juzuu hizo za hadithi miongoni mwa wenyeji wa huko zimekusanya mila na desturi kwa kuambatanisha picha za mazingira ya kijiografia, vijiji na shughuli za wenyeji.

Inajulikana kwamba juzuu za "Hadithi Simulizi Nchini China" zimechapishwa kwa wilaya moja juzuu moja. Nchini China jumla kuna wilaya zaidi ya 2800, kazi ya uchapishaji ni ngumu na kubwa. Lakini kwa ajili ya kuokoa urithi wa utamaduni wa jadi shirika hilo litabeba jukumu hilo bina neno. Alisema, "Urithi wa utamaduni wa taifa la China ni hakimiliki ya watu wa makabila yote ya China, kuhifadhi urithi huo ni wajibu wa lazima wa shirika letu, tutajitahidi kuokoa urithi wa utamaduni wa taifa letu bila kulegea."

Shirika la China la Wasanii wa Sanaa na Fasihi za Wenyeji kwa kushirikiana na Shirika la Umma la Uchapishaji la Mkoa wa Heilongjiang yamechapisha vitabu mfululizo vya fasihi simulizi, vikiwa ni pamoja na hadithi, hekaya, picha za kukatwa na vinyago.

Naibu mkurugenzi wa Idara Kuu ya Uchapishaji ya China Bw. Liu Binjie alisema,

"Mradi huu umeshirikisha mashirika ya uchapishaji zaidi ya 40. Mashirika hayo yanasaidia sana uokoaji wa urithi wa utamaduni wetu wa jadi. Mchango mkubwa kwa shirika la uchapishaji ni kuongeza mali katika hazina ya utamaduni wa taifa."

Idhaa ya kiswahili 2006-01-23