Mkutano wa 6 wa wakuu wa Umoja wa Afrika unatazamiwa kufanyika tarehe 23 huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan. Marais au viongozi wa serikali wa nchi wanachama 53 wote watahudhuria mkutano huo. Wachambuzi wanaona kuwa, kwenye mkutano huo viongozi wa nchi za Afrika watajitahidi kusukuma mbele amani na maendeleo ya bara la Afrika.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni elimu na utamaduni, Umoja wa Afrika unatumai kuendelea kuweka mkazo katika kukuza elimu, kuwaandalia watu wenye ujuzi, na kuweka mazingira mazuri kwa ajili yakuijenga Afrika iwe sehemu yenye amani, ustawi na muungano. Viongozi wa nchi za Afrika wanaona kuwa, katika mpango wa kwanza wa miaka 10 wa elimu ya Afrika uliotekelezwa kati ya mwaka 1996 hadi 2006, nchi mbalimbali za Afrika zimepata maendeleo makubwa katika kuwapatia watu wote haki ya elimu, lakini kutokana na kukabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo ni pamoja na watu wengi wenye ujuzi kuondoka nchini humo na upungufu wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya elimu, suala la elimu la nchi za Afrika bado linakabiliwa na changamoto kubwa. Kwa hivyo mkutano huo wa wakuu unatumai kuhimiza utekelezaji wa mpango wa pili wa miaka 10 wa elimu ya Afrika, ili kutimiza kihalisi lengo la kuwawezesha watu wote wa Afrika wawe na haki ya kupata elimu.
Zaidi ya hayo viongozi wa nchi za Afrika watathibitisha na kupitisha pendekezo lililotolewa na serikali ya Sudan kuhusu kuanzisha shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Afrika litakaloambatana na shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, ili kusukuma mbele maendeleo ya Afrika katika maeneo hayo. Mkurugenzi mkuu wa shirika la UNESCO atahudhuria mkutano huo na kutoa hotuba.
Kwenye mkutano huo, viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika pia watathibitisha ripoti kuhusu kuhimiza mchakato wa utandawazi wa siasa na uchumi wa Afrika na pendekezo la kuanzisha shirikisho la nchi za Afrika lililotolewa na kiongozi wa Libya Bwana Muammar Gaddafi. Mkutano huo pia utajadili uwezekano wa kutoa passpoti ya kidiplomasia ya Afrika, ili kuwahimiza watu wa nchi mbalimbali za bara la Afrika wawasiliane kwa uhuru.
Kwenye mkutano huo, viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika pia watasikiliza na kuthibitisha ripoti iliyokabidhiwa na baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika. Imefahamika kuwa mgogoro wa sehemu ya Darfur ya Sudan, mgogoro kati ya Sudan na Chad na hali ya vurugu ya Cote d'ivoire yatakuwa masuala muhimu ya kujadiliwa kwenye mkutano huo.
Licha ya mijadala hiyo, viongozi wa nchi za Afrika pia watajadili na kuthibitisha mijadala kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa, kuanzisha kituo cha hisa nchini Afrika ya ksuini au Misri, kuanzisha mfuko wa msaada unaolenga kupunguza athari za kiuchumi zilizotokana na kupandwa kwa bei ya mafuta duniani kwa nchi maskini za Afrika na kinga na tiba ya ugonjwa wa Ukimwi.
Wachambuzi wameona kuwa, viongozi wa nchi za Afrika wameanza kufahamu, katika wakati utandawazi wa uchumi duniani unapoendelea siku hadi siku, nchi za Afrika zinapaswa kusukuma mbele mchakato wa utandawazi wa siasa na uchumi wa bara la Afrika, zishirikiane kwa kujikakamavu, kulinda kwa pamoja amani na utulivu wa bara la Afrika, ili nchi za Afrika ziondokane kabisa na vurugu za kivita na umaskini, na kufuata njia ya amani, ustawi na maendeleo.
|