Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-23 20:15:22    
Uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina

cri

Uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina umepangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu, huo ni uchaguzi wa pili wa kamati ya kutunga sheria katika muda wa miaka zaidi ya kumi tangu kusainiwa mkataba wa amani wa Oslo na tangu kuasisiwa mamlaka ya taifa ya Palestina. Je Uchaguzi huo utakuwa na athari kubwa kwa muundo wa kisiasa wa jadi nchini Palestina? Na je uchaguzi huo utaleta athari gani kwa hali ya nchini humo?

Kamati ya utungaji sheria ya Palestina iliasisiwa kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza uliofanyika mwezi Januari mwaka 1996 nchini Palestina, ambayo inalingana na mabunge ya nchi za magharibi. Katika miaka 10 iliyopita, mabadiliko makubwa yalitokea kati ya makundi mbalimbali nchini Palestina, hususan kundi la Hamas lenye siasa kali na kuathiri sana muundo wa kisiasa wa jadi unaoongozwa na Fatah. Matokeo ya upigaji kura za maoni za umma uliofanyika hivi karibuni yanaonesha kuwa, uungaji mkono kwa Fatah ni mkubwa kwa asilimia chache tu kuliko ule kwa Hamas. Baadhi watu wamekadiria, kuna uwezekano wa Hamas kuishinda Fatah kwenye uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria. Kuhusu suala hilo, mwenyekti wa jumuiya ya utafiti wa masuala ya kimataifa nchini Palestina Bw. Abdul Hadi alisema,

"Kuibuka kwa Hamas kutatingisha muundo wa kisiasa wa Palestina, hivi sasa kundi la Fatah linakabiliwa na mgogoro mkubwa. Wazo la kisiasa la Fatah kuhusu mustakabali wa Palestina, jukumu lake la kuongoza watu wa nchi hiyo kutimiza ukombozi wa taifa na heshima ya viongozi wa serikali linakabiliwa na changamoto kali."

Bw. Abdul Hadi anaona, watu wengi wa Palestina wanaliunga mkono Kundi la Hamas, hii haimaanishi kuwa wanaunga mkono siasa yake, lakini kwa kiwango fulani hali mbaya ya ufisadi ya serikali ya Palestina na mwelekeo na sera za Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya kuhusu suala la Hamas kushiriki kwenye uchaguzi mkuu vimewasukuma wapiga kura kwa upande wa Hamas.

Hata hivyo Bw. Abdul Hadi anasema, kuibuka kwa Hamas ni changamoto na pia ni nafasi kwa kundi la Fatah. Amesema Fatah likiwa ni kundi la kisiasa limefanya jitihada kwa zaidi ya miaka 40 kwa ajili ya ukombozi wa Palestina, kundi la Fatah bado lina msingi imara wa umma, wazo lake la kujenga Palestina kwa njia ya amani linaendana na nia ya wapalestina walio wengi. Hivi sasa linatakiwa kukabiliana na athari zinazoletwa na Hamas na kuwa na nguvu mpya ya uhamasa katika kufanya mageuzi ya ndani ya chama chake.

"Wapalestina wanaoliunga mkono kundi la Fatah wameweka matumaini yao juu ya viongozi wapya wakifikiri kuwa, iko siku viongozi wazee wa Fatah wataondoka katika utawala. Wapalestina wengi hawaliamini kundi la Hamas, hasa hawaamini mtindo wa kufanya uamuzi bila kujali serikali ya nchi hiyo."

Kundi la Hamas ambalo limeorodheshwa na Israel na Marekani kuwa ni kundi la kigaidi, siku zote linapinga ukaliaji wa Israel kwa nguvu ya kisilaha, na kuibuka kwake kisiasa kumesababisha wasiwasi mkubwa kwa nchi za magharibi. Israel imewahi kusema, endapo kundi la Hamas litashiriki kwenye serikali ya Palestina baada ya uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria, hiyo itakuwa ni kurudi nyuma kwa hatua kubwa kwenye mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel. Bw. Abdul Hadi amesema, hivi sasa bado ni vigumu kukisia muundo wa serikali ya nchi hiyo ya baada ya uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria, lakini Israel na Marekani huenda zitashindwa kukataa kuwa na mazungumzo na serikali ya Palestina yenye wanachama wa Hamas.

Vyombo vya habari vya huko vinaona kuwa uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria nchini Palestina ni uchaguzi muhimu kuhusu muundo wa kisiasa katika siku za baadaye.