Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-23 21:35:02    
Mambo kuhusu visa ya utalii nchini China

cri

Ikiwa ni hatua ya kwanza kwa wewe kutembelea China, unapaswa kuishughulikia visa ya utalii. Wageni wanapaswa kuomba visa kwenye ofisi ya ubalozi ya China katika nchi za nje. Watalii zaidi ya 9 wakitaka kuitembelea China wanaweza kuomba visa ya utalii ya kikundi. Kwa wageni wanaotembelea mikoa maalumu ya kiuchumi ya Shenzhen, Zhuhai na Xiamen wanaweza kuomba visa ya utalii moja kwa moja kwa ofisi za forodha za mikoa hiyo. Wageni wale wanaotembelea mkoa wa Hainan kwa muda usiozidi siku 15, wanaweza kuomba visa kwenye ofisi za forodha za miji ya Haikou na Sanya. Wageni wanaotembelea Shenzhen kwa muda usiozidi saa 72 kutoka Hong Kong, hawana haja ya kuomba visa. Wageni waliopata visa wanatakiwa kuingia China kupitia forodha zilizofunguliwa kwa wageni au forodha walizoelezwa baada ya kushughulikiwa na wafanyakazi wa forodha.

Watalii wa kigeni wenye pasipoti na visa ya utalii wanaweza kufanya matembezi katika sehemu zilizosofungua mlango kwa nchi za nje, serikali ya China inalinda maslahi halali za wageni walioko nchini, lakini hawaruhusiwi kufanya shughuli zisizolingana na hali yao, zikiwa ni pamoja na ajira, kueneza dini na kufanya mahojiano na watu bila kibali, la sivyo watachukuliwa hatua. Aidha, wanapokuwa nchini China wanapaswa kuheshimu sheria na mila za China.

Watalii wanaweza kufanya matembezi nchini China katika muda waliopewa. Endapo wanataka kuendelea kufanya matembezi baada ya kupita muda wao, wanaweza kuziomba idara za usalama za karibu kurefusha muda wa matembezi. Baada ya kumaliza matembezi wanatakiwa kuondoka China kupitia forodha za kimataifa zilizofunguliwa kwa wageni.

Mambo unayopaswa kujua wakati unapopita kwenye forodha ya China

Mgeni anapopita kwenye forodha ya China anatakiwa kufuata maagizo husika ya forodha ya China, ili kufanikisha matembezi yako na kupita kwenye forodha bila matatizo, anatakiwa kufahamu mambo yafuatayo:

Mtalii anaondoka China akichukua au kusafirisha vitu vinavyo orodheshwa hapo chini, anatakiwa kuieleza forodha:

Vitu vinavyotozwa ushuru, na kiasi cha vitu vinavyoingia nchini bila kulipa ushuru

Vitu vinavyotumiwa na wasafiri wenyewe safarini pamoja na vitu ambavyo haviko katika eneo la vitu vinavyotumiwa na wasafiri wenyewe safarini, lakini bado vinahesabiwa kuwa ni vitu wanavyohitaji safarini;

Vitu vinavyopigwa marufuku kuingia au kutoka China pamoja na kiasi cha vitu vinavyoruhusiwa kuingia na kutoka China vikiwa ni pamoja na vitu vya kale, sarafu, dhahabu, fedha pamoja na vitu vilivyotengenezwa kwa madini hayo, maandishi yaliyochapishwa, na kaseti za audio na video;

Bidhaa, sampuli za bidhaa na vitu ambavyo haviko katika eneo la mizigo ya watalii.