Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-24 16:07:36    
Sekta ya huduma ya China

cri

Sekta ya huduma ni nguvu muhimu inayochangia maendeleo ya uchumi nchini China kwa hivi sasa. Katika baadhi ya nchi zilizoendelea nyongeza ya thamani ya sekta ya huduma imezidi 60% ya pato la taifa. Katika miaka ya karibuni, sekta ya huduma imeendelezwa kwa haraka ikiwa ni pamoja na migahawa, uuzaji vitu kwa rejareja au usambazaji bidhaa, utalii na mambo ya fedha.

Hivi karibuni moja ya mambo yanayomfurahisha zaidi bibi Li Hui, ambaye anafanya kazi mjini Shenzhen, mji ulioko sehemu ya kusini nchini China, ni kuona huduma ya kuagiza chakula na vitoweo kwenye Internet, kisha anajiburudisha kwa chakula anacholetewa na mikahawa nyumbani.

"Katika siku za mapumziko, sitaki kupika chakula mwenyewe, vilevile sitaki kula chakula mikahawani, nilisikia kuna huduma ya kuagiza chakula kwenye mtandao wa internet, basi nikajaribu kutafuta, niligundua kuwa nikiandika majina ya vitoweo, ninaweza kupewa majina ya mikahawa husika, kumbe ni jambo rahisi hivyo."

Bibi Li Hui alisema, hapo zamani alijua tu kupiga simu kuagiza chakula, ingawa aliweza kupata chakula, lakini halikuwa jambo rahisi. Kuagiza chakula kwenye Internet ni tofauti sana, si kama tu anaweza kupata anuani za mikahawa, bali pia anaweza kupata habari kamili kuhusu orodha ya vyakula na vitoweo, bei zake na kiasi cha upunguzaji wa bei, baada ya kufikiri, anaweza kuchagua chakula anachopenda na kuletewa nyumbani.

Hivi sasa nchini China kuna mambo mengi ambayo mtu anaweza kuhudumiwa vizuri na sekta ya huduma. Kwa mfano, mtu akitaka kusafiri, anataka kununua tikiti za ndege au za treni, anaweza kuletewa tikiti hizo baada ya kupiga simu au kutoa habari zinazotakiwa kwenye mtandao wa Internet. Aidha kuna mashirika maalumu yanayotoa huduma nzuri kwa uagizaji bidhaa, ombi la kutafuta mwalimu anayefundisha nyumbani, utafutaji wa msaidizi wa kazi za nyumbani na kulipa fedha za maji na umeme.

Pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha pato la wachina, watu wanataka jamii kutoa huduma za aina nyingi zinazohusu mavazi, chakula, makazi na usafiri, ambazo kwa upande mwingine utoaji huduma unahimiza maendeleo ya sekta ya huduma nchini. Maendeleo ya sekta ya huduma si kama tu yanarahisisha maisha ya wachina, bali pia yanahimiza maendeleo ya shughuli za uzalishaji za viwanda na ya uendeshaji wa shughuli huduma. Kwa mfano kuanzishwa kwa aina mpya ya huduma ambayo ni pamoja na uendeshaji shughuli za matawi ya kampuni na maduka, usambazaji bidhaa na biashara ya elektroniki nchini China kunahimiza kupungua kwa gharama za uzalishaji wa viwanda, mashirika ya biashara kuongeza ufanisi wa kazi na mashirika ya fedha kuboresha utoaji huduma.

Kampuni ya Swain Mdogo nchini China inashughulikia zaidi uzalishaji wa mashine za kufulia nguo, kila mwaka inazalisha kiasi cha mashine milioni 4 za kufulia nguo. Hapo zamani bidhaa ilizokuwa inazalisha zilisafirishwa kwa sehemu mbalimbali kwa magari yake yenyewe, njia ambayo iliongeza gharama za uzalishaji na kupunguza faida inayopata.

Mwaka 2001, kampuni ya Swain Mdogo ikishirikiana na kampuni moja ya vyombo vya umeme vinavyotumika majumbani kwa watu na kampuni moja ya uchukuzi, zilianzisha kampuni maalumu ya usambazaji bidhaa, ambayo ni ya kwanza nchini China. Kampuni hiyo ya usambazaji licha ya kusaidia kampuni ya Swain Mdogo kubuni mpango wa usambazaji wa bidhaa zake na kufuatilia hali ya bidhaa zake zilizoko njiani, bali pia inawajibika kuthibitisha kiasi cha bidhaa zilizowekwa kwenye stoo na muda wa kuwepo kwenye stoo ili kuongeza bidhaa na kusimamia oda za bidhaa hizo. Kufanya hivyo kwa upande mmoja kumepunguza gharama ya uchukuzi, bali pia kumeongeza ufanisi wa usafirishaji na kuwa na faida kubwa zaidi.

Naibu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Swain Mdogo Bw. Xu Yuan alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, hivi sasa gharama za usafirishaji wa bidhaa imepungua kwa 37%, jambo hilo peke yake litaongeza pato la Yuan milioni makumi kadhaa kwa kampuni, na jambo linalofurahisha zaidi ni kwamba Kampuni ya Swain Mdogo ikiwa ni mmoja wa washiriki wa kampuni ya usambazaji bidhaa inaweza kuwa na pato lingine kutokana na kampuni hiyo ya usambazaji.

"Tukiwa washiriki kila mwaka tunaweza kupata 15% hadi 20% ya faida ya kampuni ya usambazaji. Gharama zetu za uzalishaji zimepungua, na tena tukiwa washiriki wa kampuni ya usambazaji, sisi pia tunapata sehemu ya faida ya kampuni hiyo, ni bora zaidi kuliko kusafirisha bidhaa sisi wenyewe."

Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwezi Septemba mwaka jana, nyongeza ya thamani ya sekta ya usambazaji bidhaa nchini China ilikuwa Yuan zaidi ya bilioni 680, ikiwa ni ongezeko la 14% kuliko mwaka uliotangulia katika kipindi kama hiki, na kuchukua 21% ya nyongeza ya thamani ya sekta ya huduma nchini China.

Hivi karibuni idara ya takwimu ya China ilirekebisha takwimu kuhusu pato la taifa mwaka 2004 kutokana na sensa ya uchumi iliyofanyika kote nchini. Takwimu mpya zinaonesha kuwa pato la China katika mwaka 2004 lilikaribia Yuan trilioni 16, kiasi hicho ni ongezeko la Yuan trilioni 2.3 kuliko takwimu za mwaka zilizotolewa. Kiasi cha 90% ya ongezeko hilo kilitoka kwenye sekta ya huduma, ambayo haikuweza kuhusishwa barabara na njia ya zamani ya takwimu. Hivi sasa kiasi cha nyongeza ya thamani ya sekta ya huduma inachukua 41% ya pato la taifa kutoka 32% ya kabla ya takwimu kurekebishwa.

Mkurugenzi mkuu wa idara ya takwimu ya China Bw. Li Deshui anaona, kupanuka kwa nafasi ya sekta ya huduma kunaonesha kuwa hali ya ongezeko la uchumi wa China ni ya mwafaka zaidi kuliko ilivyooneshwa na takwimu za awali.

"Hapo mwanzoni kulikuwa na tamko duniani kwamba ongezeko la uchumi wa China lilitegemea sekta ya viwanda, hususan sekta ya uzalishaji, tena lilisema, ongezeko hilo lilitegemea usafirishaji bidhaa kwa nchi za nje, hali halisi ya hivi sasa inaonesha kwamba si mwafaka kufanya uamuzi haraka namna hii, matokeo ya sensa iliyofanyika nchini China yanaonesha kuwa sekta ya huduma imetoa mchango mkubwa katika ongezeko la uchumi wa China."

Hata hivyo, kulikuwa na matatizo mengi katika maendeleo ya haraka ya sekta ya huduma. Hususan ni tofauti kubwa katika ubora wa huduma zilizotolewa, wafanyakazi wa sekta hiyo kutokuwa na sifa nzuri, na kubwa zaidi kupata malalamiko mengi katika maeneo ya huduma yanayohusika sana na maisha ya watu. Hivyo China inatakiwa kuharakisha mageuzi ya utaratibu wa sekta ya huduma na ya maeneo yanayohusika, na kuimarisha ushindani wa masoko.

Idhaa ya kiswahili 2006-01-24