Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-24 19:41:00    
Sera za kuwasaidia na kuwanufaisha wakulima wa China zahimiza wakulima wazalishe nafaka kwa wingi

cri

Wizara ya kilimo ya China ilidokeza kuwa, wakati wa utekelezaji wa mpango wa 10 wa miaka mitano, China ilitoa sera za kuwasaidia na kuwanufaisha wakulima yaani kupunguza na kusamehe kodi mbili za kilimo na kutoa ruzuku za aina tatu. Kutokana na kuimarishwa kwa nguvu za uhakikisho wa kisera, wakulima wa China wamekuwa na juhudi kubwa za kuzalisha nafaka, na ongezeko la uzalishaji wa nfaka linafufuliwa.

Habari zinasema wakati wa mpango wa 10 wa miaka mitano, China ilitoa sera nne kuhusu kulimo na wakulima. Ya kwanza ni kupunguza na kusamehe kodi za kilimo na kodi za mazao maalumu mbali na kodi ya tumbaku. Takwimu zilizotolewa zilionesha kuwa, mwaka 2004, mapato ya wakulima kote nchini yaliyoongezeka kutokana na kupunguzwa na kufutwa kwa kodi ya kilimo yalifikia Yuan bilioni 30.2; mwaka 2005, mikoa 28 ilitekeleza sera ya kusamehe kodi za kilimo kabla ya wakati uliopangwa, na katika mikoa mingine ya Hebei, Shandong na Yunnan wilaya kadhaa pia ziliacha kutoza kodi za kilimo, na kuwapunguzia wakulima mzigo wa Yuan bilioni 22. Mwaka 2006, China itaacha kabisa kutoza kodi za kilimo, na kodi za kilimo zilizotozwa kwa zaidi ya miaka elfu mbili nchini China zitakuwa historia. Kwa hivyo, wakulima wa China watapunguzwa kodi za Yuan zaidi ya bilioni 50.

Ya pili ni kutoa ruzuku ya kilimo cha moja kw moja kwa mazao ya chakula. Mwaka 2004, serikali ya China ilitenga fedha yuan bilioni 11.6 kutoka mfuko wa fedha unaotumika kwa kukabiliana na msukosuko wa nafaka kwa kutoa ruzuku kwa wakulima wanaozalisha mazao ya chakula. Wakulima milioni 600 walinufaika moja kwa moja kutokana na sera hiyo, ambapo wastani wa pato la kila mkulima umeongezeka kwa yuan 19.3; mwaka 2005 mikoa 29 ilitekeleza utaratibu wa kutoa ruzuku kwa wakulima wanaozalisha nafaka, ruzuku hizo zilifikia yuan bilioni 13.2, hili ni ongezeko la asilimia 13.8 kuliko mwaka 2004.

Ya tatu ni kutoa ruzuku kwa wakulima wa sehemu kadhaa kwa kununua mbegu bora na vyombo vya kilimo. Mwaka 2004 na mwaka 2005, ruzuku za matumizi ya mbegu bora zilifikia Yuan bilioni 2.85 na bilioni 3.8; ruzuku za kununua vyombo vya kilimo zilifikia Yuan milioni 70 na milioni 300.

Ya nne ni kutekeleza sera ya kuwepo kwa kikomo cha bei ndogo kabisa ya kununua nafaka kutoka kwa wakuliam katika sehemu muhimu zinazozalisha nafaka. Mwaka 2004 na mwaka 2005, mpango wa kuwepo kwa kikomo cha bei ndogo kabisa ya kununua mpunga ambapo mpunga kutoka kwa wakulima ulitekelezwa katika mikoa ya Hunan, Jiangxi, Hubei na Anhui, ambapo mpunga unaokua haraka ulinunuliwa na serikali kwa bei ya yuan 0.7 kwa nusu kilo, mpunga wa aina ya indika kwa bei ya yuan 0.72 kwa nusu kilo, mpunga wa aina ya japonica kwa bei ya yuan 0.75 kwa nusu kilo, hata hii inahakikisha mapato ya wakulima wanaozalisha mazao ya chakula.

Ofisa husika wa wizara ya kilimo ya China alisema, kutokana na kuongezeka kwa nguvu ya uungaji mkono wa kisera kwa uzalishaji wa chakula, mapato ya wakulima yanaongezeka, na bei ya nafaka imetulia kwenye kiwango fulani, kwa hivyo inahakikisha zaidi ufanisi wa kilimo cha nafaka, kuhamasisha zaidi wakulima kuzalisha nafaka kwa juhudi, na kuonesha umuhimu kwa ufufuzi wa maendeleo ya uzalishaji wa nafaka.