Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-01-25 20:22:58    
Mapishi ya samaki ya Lu yenye ladha ya sukari na pilipili hoho

cri

Mahitaji

Samaki mmoja, kitunguu moja, pilipili hoho moja, pilipili mboga moja, sosi yenye ladha ya sukari na wanga ya pilipili hoho vijiko viwili, wanga kijiko moja, chumvi nusu kijiko, pilipili manga 1/3 kijiko, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, na mafuta gramu 300.

Njia

1. ondoa gamba la samaki ya Lu na ondoa matumbo, mkata vipande mbili kwa kisu, kata pilipili hoho, pilipili mboga na kitunguu kuwa vipande vipande.

2. weka samaki ndani ya bakuli moja, tia mvinyo wa kupikia, chumvi na pilipili manga korogakoroga. Baada ya dakika 10 tia wanga kwenye pande mbili za samaki.

3. washa moto na tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe na joto la nyuzi 70, tia samaki mkaange mpaka awe rangi ya hudhurungi iliyopauka.

4. washa moto tena tia vipande vya kitunguu, pilipili hoho, pilipili manga, korogakoroga, mimina sosi yenye ladha ya sukari na pilipili hoho, korogakoroga. Uipakue na mimina kwenye samaki. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.