Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-01 20:05:49    
Mapishi ya kuchemsha samaki pamoja na pilipili hoho

cri

Mahitaji

Samaki mmoja, vipande vya tangawizi, vitunguu maji, kiasi kidogo cha mvinyo wa kupikia, sukari, chumvi, M.S.G na mboga, kiasi kingi pilipili hoho, pilipili manga na mafuta.

Njia

1. Kata nyama ya samaki iwe vipande vipande, halafu iweke kwenye bakuli moja, tia vipande vya tangawizi, mvinyo wa kupikia, chumvi, sukari, pilipili manga na M.S.G, korogakoroga.

2. Washa moto kisha chemsha maji, halafu tia vipande vya samaki ndani ya maji ya moto kwa dakika 2, vipakue. Weka mboga kwenye bakuli kubwa, kisha weka vipande vya samaki kwenye mboga.

3. Tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya tangawizi, vitunguu maji, pilipili hoho, pilipili manga, mpaka mafuta yachemke, kisha weka vipande vya samaki. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.