Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-01 21:07:35    
Umoja wa Mataifa watoa ripoti ikionesha kuwa uchumi wa Afrika utaendelea kuongezeka kwa utulivu

cri

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa kuhusu makadirio ya hali ya uchumi duniani katika mwaka 2006 inaonesha kuwa, katika mwaka jana uchumi wa Afrika unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5.1, na unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 5.5 katika mwaka 2006.

Ripoti hiyo imesema, hali ya miaka 10 iliyopita imeonesha kuwa, uchumi wa Afrika umeendelea kuongezeka kwa utulivu. Ingawa nchi kadhaa za Afrika zilikumbwa na maafa ya ukame na wadudu na mavuno ya chakula yaliathiriwa, lakini hali ya jumla ya kilimo ya Afrika ilikuwa nzuri katika mwaka 2005. mageuzi ya miundo ya uchumi katika nchi nyingi za Afrika yameendelea kupata mafanikio. Hali hiyo imehimiza maendeleo ya uchumi. Kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Burundi na Liberia na kusainiwa kwa mkataba wa amani ya Sudan kumeweka mazingira mazuri kwa maendeleo ya uchumi wa nchi hizo.

Mazingira mazuri ya kimataifa pia yanasaidia ongezeko la uchumi wa Afrika. Kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta ya kimataifa na bei ya malighafi katika biashara ya kimataifa kumesukuma mbele ongezeko la mapato ya biashara ya mauzo kwa nje na maendeleo ya uchumi wa nchi za Afrika. Kuongezeka kwa uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, na misaada ya kiserikali kwa ajili ya maendeleo, na kupunguzwa na kusamehewa kwa madeni ya nje pia kutasaidia maendeleo ya uchumi wa Afrika.

Ongezeko la uchumi wa nchi nyingi zilizoko sehemu ya kusini mwa Sahara linakadiriwa kufikia asilimia 3 hadi 7 katika mwaka 2006. mwaka jana, uchumi wa Afrika ya Kusini ulikua kwa asilimia 5. chanzo kikubwa cha ongezeko la uchumi ni ongezeko la matumizi ya familia lililosababishwa na ongezeko la mapato halisi.

Rais Ben Ali wa Tunisia tarehe 30 alisisitiza kuwa, amani ya dunia itapatikana kupitia mazunguzmo, uvumilivu na maelewano.

Kwenye kongamano la kimataifa kuhusu ustaarabu na utamaduni wa binadamu rais Ben Ali alitoa hotuba akisema kuwa, binadamu pamoja na utamaduni na ustaarabu wake vyote haviwezi kutofautiana kuwa vya uzuri na ubaya, kwa kuwa utamaduni na ustaarabu wote ni urithi wa pamoja wa binadamu.

Rais Ben Ali aliainisha kuwa, "hivi sasa mazungumzo kati yetu na pande nyingine husika hayajafanyika katika hali yenye usawa, kwa kuwa sura ya waarabu na waislamu imeathiriwa vibaya kutokana na kuelewa kwa makosa utamaduni na ustarabu wake." Alisema, ili kuanzisha mazungumzo na pande mbalimbali husika kwa uwiano na ufanisi, pande mbalimbali zinapaswa kushirikiana katika kuimarisha kazi ya Umoja wa Mataifa, kujenga na kusukuma mbele utaratibu wa ushirikiano na maelewano, kujitahidi kuondoa vyanzo vya hali ya wasiwasi na migogoro, kupunguza umaskini na magonjwa, kuzuia pengo la maendeleo kati nchi mbalimbali lisipanulike zaidi, na kuondoa mazingira yoyote yanayoweza kusababisha chuki, mabavu na ugaidi.