Serikali ya China hivi karibuni ilitoa rasmi "Waraka wa sera za China kwa Afrika", hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya China kutoa waraka wa sera za China kwa Afrika. Waraka huo umekumbusha mchakato wa urafiki kati ya China na Afrika, kufafanua maoni ya China juu ya hadhi na umuhimu wa Afrika duniani, na kupanga mpango kabambe kuhusu urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta za siasa, uchumi, utamaduni na jamii. Mwandishi wetu wa habari amewahoji mabalozi wa Kenya na Tanzania walioko China, mabalozi hao wamesifu sana waraka huo.
Balozi wa Tanzania nchini China Bwana Charles Asilia Sanga alisema:
Tukikumbusha historia, urafiki kati ya China na Afrika ulianzia zaidi ya miaka 600 iliyopita ambapo kikosi cha merikebu ya China iliyoongozwa na Zheng He ilipofika barani Afrika. Na wakati nchi za Afrika zilipojipatia uhuru, serikali ya China na wananchi wake walitoa msaada mkubwa sana kwa Afrika, na katika ujenzi na maendeleo ya Afrika, China imetoa tena misaada mingi kwa Afrika, Reli ya TAZARA ni mfano mmoja, kutokana na maana hii, kutolewa kwa Waraka wa sera za China kwa Afrika si jambo la ajabu kwao, na waraka huo umefafanua vilivyo mambo yaliyofanywa na yanayofanyika sasa na pande mbili China na Afrika.
Balozi wa Kenya nchini China Bibi Ruth Sereti Solitei anaona kuwa, waraka huo umeonesha nia ya dhati ya China ya kutumai kushirikiana na Afrika katika kutimiza ustawi wa pamoja, alisema:
China ni rafiki wa dhati wa Afrika, kutolewa kwa Waraka wa sera za China kwa Afrika kumeimarisha zaidi urafiki kati ya China na Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, mawasiliano kati ya viongozi wakuu wa China na Kenya yamekuwa barabara siku hadi siku, na maingiliano kati ya nchi hizo mbili yameongezeka zaidi katika sekta za utamaduni na elimu. Katika miaka mitatu iliyopita, kwa kupitia semina mbalimbali zilizofanyika nchini China, China imeisaidia Kenya kutoa mafunzo ya ujuzi mbalimbali kwa watu wapatao zaidi ya 3000.
Waraka wa sera za China kwa Afrika umedhihirisha kuwa, kanuni na lengo la jumla la sera za China kwa Afrika ni: kuwa na urafiki wa dhati, kutendeana kwa usawa, kunufaishana na kupata ustawi wa pamoja; kuungana na kushirikiana; kufundishana na kutafuta maendeleo kwa pamoja. Balozi wa Tanzania nchini China Bwana Sanga alipotaja hayo alisema, kanuni na lengo hilo la jumla linagusa hisia zake, akisema:
Kama waraka huo ulivyosema, uhusiano kati ya China na Afrika ni wa kunufaishana na kusaidiana. Uhusiano huo umeonekana katika msaada mkubwa wa serikali ya China kwa nchi za Afrika, pia umeonekana katika uungaji mkono wa siku zote wa nchi za Afrika kwa China katika mambo ya kimataifa.
Mwezi Desemba mwaka huu, mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na mkutano wa tatu wa mawaziri wa baraza hilo itafanyika hapa Beijing, ambapo viongozi wa China na nchi za Afrika watakutana Beijing na kupanga kwa pamoja ushirikiano kati ya China na Afrika katika siku za mbele. Balozi Sanga alisema:
|