Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-07 15:54:37    
Katika kipindi cha mpango wa 10 wa miaka mitano, sekta ya nishati ya China yapata maendeleo kwenye pande 6

cri

Kwenye mkutano wa 19 wa Halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, naibu waziri mkuu wa China Bw. Zeng Peiyan alipotoa hotuba kuhusu hali ya nishati na usalama wa nishati nchini China alisema, katika kipindi cha mpango wa 10 wa miaka mitano kidhahiri, hatua ya maendeleo ya nishati yaliharakishwa, ujenzi wa sekta ya nishati ulipata mafanikio mapya katika pande 6.

Kwanza, uwezo wa utoaji nishati umeinuliwa siku hadi siku. Baada ya jududi za miaka mingi, China imeanzisha kimsingi utaratibu wa utoaji nishati ambao makaa ya mawe ni nishati muhimu, kiini chake ni nishati ya umeme, mafuta na gesi asilia, nishati mpya na nishati zinazoweza kutumika tena zinapata maendeleo kwa pamoja. Mwaka 2004 uzalishaji wa jumla wa nishati ulikuwa kigezo cha makaa ya mawe tani bilioni 1.85. China ilikuwa nchi ya pili inayozalisha nishati kwa wingi duniani. Mfumo wa usafirishaji wa nishati umeanzishwa kimsingi.

Pili, utaratibu wa matumizi ya nishati umeboreshwa. Mwaka 2004, matumizi ya nishati yalifikia makaa ya mawe tani bilioni 1.97 kutokana na kigezo cha nishati kwa upimaji, na China ilikuwa nchi ya pili inayotumia nishati kwa wingi duniani. Miongoni mwa nishati zilizotumiwa, kiasi cha makaa ya mawe kilipungua kuwa asilimia 67.7 kutoka asilimia 76.2 ya mwaka 1990. Na matumizi ya nishati zisizoleta uchafuzi kwa mazingira yaliongezeka. Uzalishaji wa nishati ya nyuklia ulifikia kilowati milioni 6.94, na maendeleo ya nishati za upepo, jua na uwezo wa viumbe yametiliwa maanani.

Kiwango cha teknolojia na vifaa na zana katika shughuli za nishati kimeinuliwa hatua kwa hatua. Mfumo kamili wa teknolojia wa viwanda vya mafuta na gesi umeanzishwa hatua kwa hatua. Teknolojia kadhaa zikiwemo teknolojia ya uchimbaji kwenye sehemu zenye utatanisha wa kijiografia na teknolojia ya kuinua uwezo wa uchimbaji wa mafuta zimefikia hali ya juu duniani. Na China imejenga migodi mingi ya makaa ya mawe yenye teknolojia ya kiwango cha juu duniani.

Kazi za kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira zimepata maendeleo. Kuhesabiwa kwa bei zisizobadilika, matumizi ya nishati yalipungua kwa makaa ya mawe tani 5 kutokana na kigezo cha nishati kwa upimaji kila ikipata pato la yuan elfu 10 katika mwaka 2004 kutoka tani 16.6 ya mwaka 1990, ambayo yalipungua kwa asilimia 4 kwa mwaka. Kazi ya kubana matumizi ya nishati yameanzishwa katika jamii nzima, na kazi ya kuhifadhi mazingira imeimarishwa.

Mageuzi ya utaratibu wa nishati yamesukumwa mbele kwa hatua madhubuti, na soko la nishati limepata maendeleo hatua kwa hatua. China imeanzisha utaratibu wa nishati ambao mashirika yanajiendesha, kuna ushindani mwafaka kwenye soko, na serikali inasimamia kwa ujumla. Uzalishaji na mauzo ya makaa ya mawe hayadhibitiwi na serikali moja kwa moja, bei inaamuliwa kimsingi kwenye soko. Mageuzi ya utaratibu wa sekta ya umeme yamepata maendeleo makubwa, na ufanisi wa uendeshaji wa shughuli za mafuta na gesi umeinuliwa.

Kazi ya utungaji wa sheria kuhusu nishati imeimarishwa. Katika kipindi cha mpango wa 9 wa miaka mitano, bunge la umma la China na halimashauri ya kudumu ya bunge la umma la China iliongoza kutunga sheria ya nishati ya umeme, sheria ya makaa ya mawe na sheria ya kubana matumizi ya nishati, ambazo zimetoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nishati na kubana matumizi ya nishati. Sheria ya nishati zinazoweza kutumika tena ilitolewa mwaka 2005. Baraza la serikali la China pia lilitunga au kurekebisha kanuni kadhaa za nishati. Utungaji na utekelezaji wa sheria na kanuni hizo umeonesha kuwa ujenzi wa utaratibu wa sheria za nishati umepiga hatua kubwa.

Bw. Zeng Peiyan alisema, mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya nishati nchini China yamechangia maendeleo ya haraka ya uchumi na jamii. Tunapoona mafanikio hayo, pia tumeona kuwa, baada ya China kutekeleza mpango wa 10 wa miaka mitano, hasa katika miaka mitatu iliyopita, kutokana na maendeleo ya uchumi, matatizo yaliyotokea katika miaka mingi iliyopita kwenye sekta ya nishati yalikuwa wazi zaidi, na hali ya utoaji wa nishati iliyo nyuma imezuia maendeleo ya uchumi na jamii. Tutashughulikia kwa makini na kuchukua hatua za mseto ili kutatua matatizo hayo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-07