Hivi karibuni waislamu wa nchi nyingi duniani wanaendelea kutoa malalamiko kupinga baadhi ya magazeti ya nchi za Ulaya kuchapisha michoro ya katuni za kumdhalilisha mtume Mohamed wa dini ya kiislamu. Shughuli za kutoa malalamiko zimebadilika kuwa vitendo vya kimabavu, ambavyo vimesababisha vifo, majeruhi na hasara ya mali, hivyo jumuiya ya kimataifa inataka pande mbalimbali husika zijizuie ili kuepusha mambo kuharibika zaidi.
Gazeti la Denmark linalojulikana kwa "Jyllands-Posten" mwezi Septemba mwaka jana lilichapisha seti moja ya picha za katuni za kumkashifu mtume Mohamed, ambazo moja ya michoro hiyo ni kuhusu mtume Mohamed aliyeweka bomu kichwani. Mwanzoni mwa mwezi huu, magazeti ya baadhi ya nchi za Ulaya yakidai kuunga mkono uhuru wa kutoa maoni, yalichapisha picha hizo. Vitendo hivyo vimesababisha malalamiko makali kutoka kwa nchi za kiislamu.
Maendeleo ya matukio hayo yanafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Serikali za baadhi ya nchi zikiwemo Marekani na Uingereza zilikosoa picha hizo kufanya makosa juu ya waislamu. Lakini ghadhabu za waislamu zinaendelea kuwa kubwa zaidi. Tarehe 4 baadhi ya walalamikaji walichoma moto ofisi za ubalozi wa Denmark na Norway zilizoko katika Damascus, mji mkuu wa Syria, kwa kufuata, ofisi ya ubalozi wa Denmark iliyoko katika Beirut nchini Lebanon pia ilishambuliwa na maelfu ya waislamu, katika matukio hayo mawili, watu makumi kadhaa walijeruhiwa. Nchini Afghanistan, baadhi ya walalamikaji walipambana na polisi, kwa uchache watu 6 waliuawa na watu wengi walijeruhiwa.
Kutokana na kukabiliwa na hali inayoweza kuwa mbaya zaidi, waziri anayeshughulikia mambo ya dini wa serikali ya Syria alitoa taarifa tarehe 4 huko Damascus, wakieleza masikitiko kuhusu walalamikaji kuchoma moto ofisi za ubalozi wa Denmark na Norway zilizoko nchini Syria. Amesema, watu wana haki ya kutoa malalamiko kuhusu picha zinazomkashifu mtume Mohamed, lakini wanapaswa kufuata njia ya mwafaka wala siyo kwenda kinyume na kanuni za dini ya kiislamu. Waziri mkuu wa Lebanon Bw. Fuad Siniora amesema, vitendo vya kimabavu havina uhusiano wowote na dini ya kiislamu, vitendo vya kuharibu usalama vimeharibu sura ya dini ya kiislamu.
Hapo baadaye katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan alitoa taarifa kwa kupitia msemaji wake ikieleza wasiwasi wake kuhusu matukio ya kimabavu yaliyosababishwa na mgogoro wa katuni. Taarifa hiyo inawataka waislamu wapokee samahani iliyotolewa na gazeti la "Jyllands-Posten" kuhusu uchapishaji wa michoro ya katuni, na inawataka wajizuie, kuonesha moyo wa kusamehe wengine wa dini ya kiislamu na kukomesha mgogoro wa katuni. Katika taarifa hiyo Bw. Annan amezitaka pande mbalimbali zijitahidi kupunguza hali ya wasiwasi iliyoletwa na mgogoro wa katuni na kuepusha kutenda vitendo vinavyozidisha hali ya wasiwasi.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw. Philippe Douste-blazy tarehe 6 alitoa tamko akiwataka watu wajizuie, amesema Ufaransa inapinga kutumia vitendo vya kimabavu kuhusu matukio ya michoro ya katuni.
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Zhaoxing, ambaye hivi sasa anaitembelea Ulaya, tarehe 6 alipokuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Norway Bw. Jonas Gahr Stoere alisema, dini na ustaarabu tofauti unapaswa kuheshimiana, aliongeza kuwa usalama wa ubalozi wa kidiplomasia unatakiwa kulindwa kwa mujibu wa sheria ya kimataifa. Anatarajia pande mbalimbali husika zitajizuia, na kutatua ipasavyo matukio hayo na kuepusha kutokea kwa mgogoro mpya.
Katika siku hiyo, mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kimataifa ya bunge la taifa la Russia Bw. Konstantin Kosachev aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuchapisha michoro ya katuni ya kumkashifu mtume Mohamed kwa magazeti ya baadhi ya nchi za Ulaya, kutaleta mgongano kati ya Ulaya na nchi za kiislamu. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kulaani na kuchukua hatua kuzuia kutokea tena kwa matukio kama hayo. Alitoa wito wa kutaka waislamu kutatua suala hilo kwa njia ya kisiasa wala siyo vitendo vya kimabavu.
Idhaa ya Kiswahili 2006-02-07
|