Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-08 21:06:37    
Mkutano kuhusu "mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" wafanyika

cri

Nchi zilizosaini "mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" duniani zitakuwa na mkutano wa kwanza kati ya tarehe 6 hadi 17 mwezi Februari huko Geneva. "Mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" ni mkataba kwa kwanza duniani kuhusu afya ya binadamu, na ni mnara katika njia ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku duniani, ambao una maana kubwa kwa maendeleo ya shirika la afya duniani. Kwa wawakilishi kutoka nchi 110 duniani, namna ya kutekeleza mkataba huo itakuwa ni mada muhimu ya mkutano huo.

Mazungumzo kuhusu "mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" yalianza mwezi Oktoba mwaka 1999. Nchi wanachama 192 wa shirika la afya duniani ziliafikiana kwenye waraka wa mwisho tarehe 21 mwezi Mei mwaka 2003. Baada ya nchi ya 40 kuidhinisha mkataba huo, mkataba ulianza kufanya kazi mnamo tarehe 27 mwezi Februari mwaka 2005. Kutokana na mkataba huo, mkutano wa kwanza wa nchi zilizosaini mkataba ungefanyika ndani ya mwaka mmoja baada ya mkabata huo kufanya kazi.

"Mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" umeweka mfano kwa sheria za kimataifa, mkataba huo una kanuni za jumla, kwa mfano: kuchukua hatua za bei ili kupunguza mahitaji ya tumbaku na hatua za ukusanyaji kodi, kwa upande mwingine mkataba huo umetoa maagizo kamili kuhusu ufungaji na chapa za sigara. Kwa hatua za bei na ukusanyaji kodi, mkataba huo unaheshimu mamlaka ya nchi mbalimbali ukisisitiza, utekelezaji wake usidhuru uamuzi na mamlaka ya kubuni sera ya nchi zilizosaini mkataba. Kuhusu baadhi ya maagizo ya mkataba huo yakiwa ni pamoja kuhusu ufungaji na chapa zake, mkataba huo umesisitiza kuwa maneno ya onyo kuhusu madhara ya sigara ni lazima yaonekana kwenye 30% ya pakiti ya sigara ndani ya miaka mitatu baada ya mkataba huo kuanza kazi; na kupiga marufuku kutoa matangazo ya sigara ndani ya miaka mitano.

Kwenye mkutano huo, wawakilishi wengi walieleza mbinu zilizochukuliwa na nchi zao katika miaka ya karibuni za kudhibiti matumizi ya sigara. Ireland na Hispania zimepiga marufuku uvutaji sigara kwenye sehemu za umma. India imetunga sheria kamili kuhusu upigaji marufuku wa uvutaji sigara. Australia, Brazil, Canada, Singapore na Thailand zimeagiza wazi kuwa kwenye paketi za sigara ni lazima kuchapisha maneno kuhusu madhara ya sigara.

Mwakilishi wa China Bw. Sha Zukang kwenye mkutano huo alisema, udhibiti wa uvutaji sigara umepata maendeleo halisi nchini China. China imetoa sheria kadhaa kuhusu udhibiti wa uvutaji sigara. Katika miaka ya karibuni idara husika za serikali zimechukua hatua kuimarisha nguvu ya udhibiti wa uvutaji sigara; kuanzisha harakati za kutovuta sigara kwenye sehemu za umma, kuanzisha idara zisizo na wavutaji sigara na miji isiyo na matangazo ya sigara. Mbali na hayo, serikali ya China inajitahidi kuandaa michezo ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008 isiyo ya wavuta sigara.

Washiriki wa mkutano wanaona, "mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" ni mkataba wa kikanuni, kutolewa kwake ni mwanzo tu kwa udhibiti wa matumizi ya tumbaku duniani, katika siku za baadaye inapaswa kubuni vifungu kamili na vya nyongeza kuhusu "mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku". Kwa mfano, mkataba huo haukuweka maelezo na maagizo kamili kuhusu biashara ya magendo ya sigara na matangazo ya sigara yanayotoka nchi za nje, hivyo washiriki wengi wa mkutano wanataka kubuni makubaliano mawili kuhusu "biashara haramu ya sigara" na "matangazo ya sigara yanayotoka nchi za nje". Ofisi ya uratibu ya shirika la afya duniani imesema, ubunifu wa makubaliano hayo mawili umewekwa katika agenda ya shirika la afya duniani.

Mratibu mkuu wa shirika la afya duniani, Bw. Lee Jong Wook alisema kwenye mkutano huo, uvutaji sigara ni maafa yanayodhuru afya za watu, tamko hilo linazidi kuungwa mkono na watu wengi. Endapo "mkataba wa kanuni za udhibiti wa tumbaku" utatekelezwa vizuri, basi maisha ya watu zaidi ya milioni 200 yataokolewa kabla ya mwaka 2050. Kutokana na maana hiyo, tunasema "historia ya binadamu itabadilishwa".

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-08