Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-08 21:15:35    
Mapishi ya kamba-mwakaje pamoja na pilipili yenye ladha ya samaki

cri

Mahitaji:

Kamba-mwakaje gramu 350, pilipili hoho gramu 40, mchuzi wa sosi gramu 10, chumvi gramu 3, sukari gramu 30, siki gramu 30, mvinyo wa kupikia gramu 15, vipande vya tangawizi, vitunguu saumu na vitunguu maji gramu 15, M.S.G gramu 2, unga gramu 50, mayai mawili, supu ya nyama gramu 200, mafuta gramu 500.

Njia:

1. osha kamba-mwakaje, wakaushe kisha waweke kwenye bakuli, tia mvinyo wa kupikia, chumvi, korogakoroga. Koroga mayai pamoja na unga halafu tia kamba-mwakaje kisha korogakoroga.

2. koroga mchuzi wa soya, sukari, siki, mvinyo wa kupikia, M.S.G, supu ya nyama na unga.

3. tia mafuta kwenye sufuria, pasha moto hadi joto la nyuzi 60, tia kamba-mwakaje kwenye sufuria wakaange mpaka wawe na rangi ya hudhurungi iliyopauka.

4. ondoa mafuta madogo, pasha moto tena tia pilipili hoho halafu korogakoroga, tia vipande vya tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu, korogakoroga, tia mchuzi uliokorogwa, tia kamba-mwakaje korogakoroga, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-08