Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-13 19:01:28    
Vivutio vya utalii vya Beijing

cri

Beijing ni mji mkuu wa China, na ni kitovu cha siasa na utamaduni nchini China. Beijing iko katika sehemu ya kaskazini ya ardhi ya tambarare ya kaskazini ya China. Kijiografia, Beijing, Rome ya Italia, Madrid ya Hispania ziko katika latitudo moja. Hali ya hewa ya Beijing ni yenye upepo wa kimajira wa bara, siku za majira ya baridi na joto ni nyingi, siku za majira ya kichipuka na kupukutika ni kidogo na kukosa mvua. Wastani wa hali-joto ni nyuzi 11.8 sentigredi kwa mwaka.

Beijing ina historia ndefu sana ya kuanzia miaka 3,000 iliyopita. Katika kipindi cha mwaka 770 hadi mwaka 221 K.K, sehemu ya Beijing ilikuwa mji mkuu wa nchi ndogo za himaya ya ufalme, katika enzi za Qin na Han pamoja na kipindi cha Nchi Tatu, Beijing ilikuwa mmoja wa mji muhimu katika sehemu ya kaskazini ya China. Beijing ilianza kuwa mji mkuu wa nchi tangu enzi ya Jin, ikifuatiwa na enzi za Yuan, Ming na Qing, ambapo kulikuwa na wafalme 34 waliotawala dola kutokea Beijing.

Baada ya kuasisiwa China mpya, hususan katika miaka zaidi 20 iliyopita baada ya kuanza kutekeleza sera za mageuzi na ufunguaji mlango, sura ya Beijing ilikuwa na mabadiliko makubwa. Majengo ya kisasa yalijengwa kila mahali na uhusiano na nchi za nje ulikuzwa kwa mfululizo. Hivi sasa, Beijing, inapiga hatua kubwa kuingia kwenye kundi la miji mikubwa duniani. Beijing, ambayo mabaki ya historia yameungana vizuri na sura ya kisasa, inavutia watu wa sehemu mbalimbali. Katika miaka ya karibuni, Beijing kila mwaka imekuwa inapokea mamilioni ya watalii kutoka nchi za nje na milioni ya makumi ya watalii wa nchini.

Historia ndefu iliiachia Beijing vitu vingi vya kale pamoja na utamaduni murua wa jadi. Ikiwa unapenda vitu na mabaki ya utamaduni, unaweza kwenda kuona Ukuta Mkuu, kutembelea makasri makubwa, au kutembelea bustani za kifalme ambazo ni pamoja na Summer Palace, Beihai, Xiangshan na Tiantan. Mandhari nzuri na majengo makubwa ya huko yatafanya wewe kutoka kuondoka. Ikiwa unataka kufahamu utamaduni na mambo kuhusu watu mashuhuri wa China, unaweza kutembelea maskani mengi ya watu mashuhuri au kwenda kusikiliza Beijing opera. Ikiwa unataka kujua hali ya maendeleo ya maeneo mbalimbali ya siasa, uchumi, sayansi na teknolojia na kijeshi, unaweza kwenda kutembelea majumba ya makumbusho zaidi ya mia moja yaliyoko mjini Beijing. Ukitaka kujiburudisha kwa mandhari nzuri ya kimaumbile ya Beijing, unaweza kwenda kuangalia milima na mito iliyoko katika sehemu ya mzunguko wa Beijing.

Hivi sasa, sehemu za mandhari ya ngazi ya 4A zilizoko hapa Beijing ni pamoja na Tiantan, makaburi 13 ya enzi ya Ming, Summer Palace, Jumba la wanyama wa baharini la Beijing, Ukuta Mkuu wa Badaling, Mlima wa Jing, Bustan ya Beihai, bustani ya makabila ya China, Jumba la sayansi na teknolojia la China, bustani ya wanyama la Beijing na Bustani ya mimea ya Beijing.

Kasri la Kifalme Mjini Beijing

Kasri la Kifalme mjini Beijing ni mfano wa majengo ya kifalme nchini China. Kasri hilo kwa Kiingereza linaitwa "Forbidden City", ni kasri lililokaliwa na wafalme wa Enzi za Ming (1368-1644) na Qing (1616-1911), wafalme 24 waliwahi kuishi katika kasri hilo. Eneo la kasri hilo ni mita za mraba laki 7.2, kuna vyumba 9999, uzio wa kasri hilo ni ukuta mwekundu wenye kimo cha mita kadhaa, urefu wa ukuta huo ni mita 3400, nje ya uzio huo kuna mto uliochimbwa kwa ajili ya kulinda kasri hilo. Aidha kwa ukubwa wa kasri hilo, mtindo wake, na ufahari wake, kasri kama hilo halipatikani katika sehemu nyingine duniani.

Kasri la Kifalme mjini Beijing limegawanyika katika sehemu mbili, majengo katika sehemu ya mbele ni sehemu kwa ajili ya wafalme kufanya sherehe kubwa na kutoa amri, majengo kwenye sehemu hiyo ni ukumbi wa Taihe, Zhonghe, na Baohe. Majengo hayo yalijengwa juu ya jukwaa lenye urefu wa mita 8, kwa mbali yanaonekana kama kasri la peponi. Majengo katika sehemu ya nyuma ni makazi ya wafalme na masuria. Majengo katika sehemu hiyo ni mengi yakiwa ni pamoja na bustani, vyumba vya kusomea na bustani yenye majabali ya ajabu, na kila jengo lina ua wake.

Kutokana na enzi na enzi katika historia ndefu, majengo ya kale yaliyobaki kikamilifu ni machache. Licha ya Kasri la Kifalme mjini Beijing, pia kuna kasri la kifalme katika mji wa Shenyang, na magofu ya makasri ya Enzi ya Han (206-220 K.K.) na Enzi ya Tang (618-907) katika mji wa Xi'an.

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-13