Kitengo cha utatuzi wa mgogoro cha Shirika la Biashara Duniani, WTO tarehe 13 kilitoa hukumu ikisema, ni makosa ya kukiuka kanuni za WTO kwa Marekani kutoa ruzuku kwa kampuni zake zinazouza bidhaa kwa nchi za nje kwa njia mpya.
Hukumu hiyo ilitolewa na kikundi cha wataalamu tarehe 30 mwezi Septemba mwaka uliopita ikisema, "sheria kuhusu kampuni zinazosafirisha bidhaa nje" ya Marekani, ambayo inaruhusu kutoa ruzuku kwa kampuni za nchi hiyo zinazosafirisha bidhaa kwa nchi za nje, imekiuka kanuni husika za WTO za kushiriki kwenye ushindani kwa usawa.
Umoja na Ulaya na Marekani zilikuwa na malumbano kuhusu "sheria inayohusu kampuni zinazosafirisha bidhaa nje" toka miaka mingi iliyopita. Mwaka 1971, serikali ya Marekani ilitunga "mpango wa ukusanyaji wa kodi kuhusu kampuni za Marekani zinazosafirisha bidhaa kwa nchi za nje" ili kuhimiza usafirishaji bidhaa kwa nje na kupunguza pengo la biashara, sheria hiyo inatoa nafuu ya kuchelewa bila kikomo kwa ulipaji wa kiasi cha 50% ya kodi kwa faida inayopata kampuni ya Marekani inayosafirisha bidhaa kwa nje. Nchi za Umoja wa Ulaya ziliona kuwa kitendo hicho ni kama kutoa ruzuku kwa njia nyingine kwa kampuni zinazosafirisha bidhaa kwa nchi za nje, zikaishitaki Marekani kwa Jumuiya ya Mkataba wa Forodha na Biashara, ambayo ilitoa hukumu mwaka 1981 ikiona kuwa Marekani imekiuka kanuni za jumuiya hiyo za kupinga kutoa ruzuku na kuitaka serikali ya Marekani kurekebisha sheria hiyo ya ukusanyaji kodi nchini mwake. Katika hali ya namna hiyo, Marekani ililazimika kubuni "sheria kuhusu kampuni zinazouza bidhaa nchi za nje" ili kubadili "mpango wa ukusanyaji kodi kuhusu kampuni za Marekani zinazouza bidhaa nchi za nje"
Umoja wa Ulaya ulichukua msimamo wa kupinga mpango huo wa Marekani mara tu baada ya kutolewa kwake, ukiona kuwa Marekani kusamehe kodi kwa kampuni zake zinazouza bidhaa kwa nchi za nje ni kama kutoa ruzuku kwa kampuni zinazouza bidhaa kwa nchi za nje. Walakini Umoja wa Ulaya haukushitaki Marekani mara moja kwa kufikiria hali ya mazungumzo ya raundi ya Uruguay. Katika kipindi cha kati na mwisho cha miaka ya 90 ya karne iliyopita, nchi za Umoja wa Ulaya zilikuwa na malalamiko mengi juu ya "sheria kuhusu kampuni zinazouza bidhaa nje" ya Marekani. Umoja wa Ulaya unakadiria kuwa, ruzuku zinazopata kampuni za Marekani za kuuza bidhaa kwa nchi za nje zinaongezeka haraka na zimefikia dola za kimarekani kiasi cha bilioni 4 kwa mwaka, hali ambayo inafanya sekta za kemikali, dawa, mitambo, elektroniki na zana za uchukuzi za nchi za Umoja wa Ulaya kukabiliwa na ushindani usio wa haki na kuingia hasara. Mwaka 1997 Umoja wa Ulaya uliishitaki Marekani katika WTO baada ya kushindwa kwa mazungumzo kati yake na Marekani.
Mwezi Oktoba mwaka 1999, WTO ilitoa hukumu ikisema, "sheria kuhusu kampuni zinazouza bidhaa nchi za nje" ya Marekani, inatekeleza utoaji ruzuku usio wa haki. Hapo baadaye Marekani ilikata rufani katika idara ya rufani ya WTO, ambayo mwezi Machi mwaka 2000 ilitoa hukumu ya kuunga mkono hukumu ile ya awali na kuitaka Marekani kubatilisha sheria hiyo kabla ya tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka 2000. Lakini Marekani haikutekeleza hukumu hiyo.
Mwezi Novemba mwaka 2000 Umoja wa Ulaya uliishitaka tena Marekani kwa WTO, likilitaka shirika hilo liiadhibu Marekani kwa kuzitoza bidhaa za Marekani zilizouzwa kwa nchi za nje ushuru wa forodha ya dola za kimarekani bilioni 4.43.
Mwezi Mei mwaka 2003 Umoja wa Ulaya uliitaka Marekani ibatilishe "sheria kuhusu kampuni zinazouza bidhaa nje ya nchi" katika msimu wa fedha wa mwaka 2003, la sivyo Umoja wa Ulaya utachukua hatua za kutoa adhabu tokea tarehe 1 mwezi Januari mwaka 2004.
Kutokana na maagizo husika ya WTO, Marekani ina muda wa miezi mitatu kurekebisha sheria yake husika, na Umoja wa Ulaya una haki ya kutoza ushuru wa adhabu kwa bidhaa za Marekani zinazouzwa kwa nchi za nje.
Idhaa ya Kiswahili 2006-02-14
|