Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-14 17:39:08    
Utoaji na mahitaji ya bidhaa kwenye soko la raslimali za uzalishaji nchini China yaelekea kwa uwiano katika nusu ya kwanza ya mwaka 2006

cri

Kwa mujibu wa makadirio yaliyotolewa na Wizara ya biashara ya China, katika nusu ya kwanza ya mwaka 2006, mahitaji ya vitega uchumi hapa nchini yataendelea kuongezeka, utoaji na mahitaji ya bidhaa za uzalishaji utaelekea kulingana na bei za bidhaa hizo zitapungua kiasi kwa jumla.

Wizara ya biashara ya China hivi karibuni ilifanya uchunguzi juu ya hali ya utoaji na mahitaji ya bidhaa zipatazo 300 za uzalishaji katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa, bidhaa 218 ambazo zinachukua asilimia 72.7 ya bidhaa zote zitakuwa na uwiano wa utoaji na mahitaji, kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 2.4 zaidi kuliko kile cha nusu ya pili ya mwaka jana. Utoaji wa bidhaa 69 utazidi mahitaji, ambazo zinachukua asilimia 23, kiasi hicho kinapungua kwa asilimia 4.6 kuliko kile cha nusu ya pili ya mwaka jana. Na bidhaa nyingine 13 ambazo zinachukua asilimia 4.3 zitahitajika sana katika soko, na idadi hiyo pia inapungua kwa asilimia 61.5 kuliko ile ya nusu ya pili ya mwaka jana.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2006, utoaji wa vifaa vya ujenzi, bidhaa za umeme, magari, metali nyeusi, raslimali za viwanda vyepesi, bidhaa za uzalishaji wa kilimo na bidhaa za kemikali utakuwa mwingi, na soko litahitaji sana bidhaa za nishati, metali za rangi na mbao.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi huo, katika kipindi cha mwezi Januari hadi Juni, uwezo wa uzalishaji katika baadhi ya sekta za viwanda utaongezeka sana, hali hii itapeleka bidhaa zikiwemo metali nyeusi na magari kuzalishwa kwa wingi zaidi kuliko mahitaji ya soko.

Wizara ya biashara ya China imekadiria kuwa, mahitaji ya chuma cha pua yatadumisha ongezeko la kasi katika nusu ya kwanza ya mwaka 2006. Wizara ya biashara ya China imedhihirisha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka jana kutokana na utengenezaji wa magari mapya ya aina mbalimbali uliofanyika karibu kwa wakati mmoja nchini China, hivyo ongezeko la mahitaji kwenye soko lilikuwa tulivu, ambapo ushindani kwenye soko la magari utazidi kuwa mkali zaidi, bei za magari zinaelekea kupungua kwa kiasi fulani katika hali ya utulivu. Wakati huo huo, kutokana na sera iliyotolewa na serikali kuhusu kuhamasisha watu watumie magari madogo yanayotoa hewa chache ambayo bei yake ni ya chini, na tena hayaleti uchafuzi mkubwa kwa mazingira, matumizi ya magari yatakayotumia nishati kubwa na kutoa hewa nyingi yatazuiliwa kwa kiasi fulani.

Mwaka 2005, chini ya uhimizaji wa hatua mbalimbali za serikali ya China kuhusu marekebisho na udhibiti wa uchumi, uchumi wa China ulidumisha maendeleo ya haraka kwa miaka mfululizo. Shughuli zenye msingi dhaifu kama vile shughuli za nishati zimeimarishwa, na uwekezaji wa kupita kiasi kwenye uzalishaji wa bidhaa unaotumia nishati nyingi, na kuleta uchafuzi mkubwa kwa mazingira pamoja na ujenzi wa nyumba wa kupita kiasi umedhibitiwa kwa hatua ya mwanzo, ambapo mahitaji yaliyoongezeka kupita kiasi kwenye soko la raslimali za uzalishaji pia umedhibitiwa, na upungufu wa baadhi ya raslimali za nishati ulilegezwa, na bei za raslimali za uzalishaji zilizopandishwa juu zimepungua kidhahiri.

Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zimeonesha kuwa, thamani ya jumla ya uuzaji wa raslimali za uzalishaji wa bidhaa wa China iliongezeka kwa asilimia 16.2 mwaka 2005, ongezeko hilo lilipungua kwa asilimia 2.8 kuliko lile la mwaka 2004.

Wizara ya biashara ya China iliainisha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka 2006, maendeleo ya uchumi wa China yatadumisha ongezeko lake la haraka, hii italeta nafasi kubwa zaidi kwa maendeleo ya utulivu wa soko la rasilimali za uzalishaji nchini China.

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-14