Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-15 16:25:36    
Wizara ya elimu ya China yasukuma mbele vyuo vikuu kushiriki kwenye maendeleo ya uchumi wa kikanda

cri

Tarehe 21 mwezi Januari kwenye mkutano wa ushirikiano na mawasiliano ya sayansi na teknolojia kati ya vyuo vikuu vinavyosimamiwa moja kwa moja na wizara ya elimu ya China na mkoa wa Guangdong, naibu waziri wa elimu wa China Bw. Zhao Qinping alisema, ni lazima kwa vyuo vikuu vinavyosimamiwa moja kwa moja na wizara ya elimu, kushiriki kwenye utaratibu wa uvumbuzi wa kikanda wenye uwezo mkubwa wa kupata maendeleo na sifa ya kipekee, na kuwa mhimili na kufanya kazi ya uongozi wa kikanda katika maendeleo ya uchumi na jamii.

Mwezi Septemba mwaka jana, waziri wa elimu Bw. Zhou Ji na mkuu wa mkoa wa Guangdong Bw. Huang Huahua walisaini mkataba wa ushirikiano wa kuinua uwezo wa uvumbuzi kwa kujitegemea, na kuharakisha maendeleo ya uchumi na jamii ya mkoa wa Guangdong. Hii inamaanisha kuwa, wizara ya elimu itapanga vyuo vikuu kuunga mkono mkoa wa Guangdong kuinua uwezo wa uvumbuzi, kutoa huduma kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya mkoa huo. Vyuo vikuu 72 vinavyosimamiwa moja kwa moja na wizara ya elimu vikiwemo Chuo Kikuu cha Beijing, Chuo Kikuu cha Qinghua vimeshiriki kwenye mkataba huo.

Bw. Zhao Qinping alisema, mwelekeo wa maendeleo ya elimu duniani umeonesha kuwa, kuendeleza sekta ya teknolojia mpya na ya kiwango cha juu, kwa vituo vya utafiti wa sayansi na teknolojia, vikiwemo vyuo vikuu kumekuwa mwelekeo wa kuendeleza uchumi katika nchi mbalimbali duniani. Ushirikiano huo kati ya wizara ya elimu na mkoa wa Guangdong ni kuunganisha nguvu za vyuo vikuu na mkoa wa Guangdong ambao uchumi wake ni mzuri zaidi nchini China; kuanzisha ushirikiano barabara katika utaratibu wa uvumbuzi wa teknolojia ambao sehemu yake muhimu ni mashirika, na uzalishaji, vyuo vikuu na taasisi ya utafiti kushirikiana pamoja, na utaratibu wa uvumbuzi wa kikanda wenye sifa za kipekee; kuinua uwezo wa uvumbuzi wa mkoa wa Guangdong na nchi nzima, kuvifanya vyuo vikuu kuwa uungaji mkono muhimu wa Mkoa wa Guangdong katika utatuzi wa masuala muhimu yakiwemo uchumi, sayansi na teknolojia na maendeleo ya jamii.

Naibu mkuu wa Mkoa wa Guangdong Bw. Song Hai alisema, uchumi wa mkoa huo ni mzuri zaidi nchini China, lakini uwezo wake wa uvumbuzi ni mdogo kuliko Beijing na Shanghai. Mkoa huo ukiwa ni mkoa unaosukuma mbele na kuongoza maendeleo ya uchumi wa Delta ya Mto Zhujiang, ni lazima uinue uwezo wa uvumbuzi kwa uwezo wa utafiti wa vyuo vikuu, na kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na kuwa kielelezo katika sehemu ya Delta ya Mto Zhujiang.

Habari zinasema, wizara ya elimu na serikali ya mkoa wa Guangdong itaendelea kuweka mkazo katika kuendeleza Chuo Kikuu cha Zhongshan na Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Kusini mwa China, kuanzisha kamati ya utoaji ushauri kwa sekta muhimu zikiwemo za upashanaji habari kwa njia ya elektroniki, viumbe, dawa mpya, mali ghafi mpya, utengenezaji wa kisasa, ubanaji wa matumizi ya nishati, nishati mpya, hifadhi ya mazingira, matumizi ya maliasili kwa njia mbalimbali, kuunga mkono vyuo vikuu husika kushirikiana na mashirika yenye uwezo mkubwa wa kupata maendeleo kufanya utafiti na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, na kujenga vituo vya mafunzo, utafiti na uzalishaji, na vituo vya kufanya utafiti kwa wanafunzi waliopata mashahada ya udaktari.

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-15