Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-16 15:42:25    
Wahandisi watatu wa China wauawa kwa risasi nchini Pakistan

cri

Wahandisi watatu wa China wameuawa kwa kupigwa risasi kwenye kijiji cha Hub mkoani Baluchistan nchini Pakistan. Rais Pervez Musharraf na waziri mkuu wa Pakistan walilaani vikali tukio hilo na kusema kwamba serikali ya Pakistan itachukua hatua kadiri iwezavyo kuwaadhibu kisheria.

Tarehe 15 saa 12 na nusu wahandisi sita wa China walirudi kambi yao kutoka mahali pa kazi, walipofika kwenye kijij cha Hubu ghafla walizuiliwa na watu waliokuwa wamepanda pikipiki mbili, kati ya majambazi hayo mmoja alifyatua risasi, wahandisi wawili wa China na dreva mmoja wa Pakistan walikufa papo hapo, na mhandisi mwingine alijeruhiwa vibaya ambaye alipokimbizwa hospitali alikufa njiani, wahandisi wengine watatu walisalimika. Wizara ya Biashara ya China imethibitisha kuwa waliouawa ni Long Hongbao, Wei Jianping na Zhao Bin. Muda mfupi baada ya kutokea kwa tukio hilo, kundi moja linalojiita "Baluchistan Liberation Army" lilitangaza kuhusika na tukio hilo.

Balozi mdogo wa China mjini Karachi Bw. Sun Chunye alieleza kuwa baada ya kutokea kwa tukio hilo polisi ya Pakistan imeimarisha hatua za kuwalinda Wachina nchini Pakistan. Alisema,

"Hivi sasa wahandisi wa China wako salama. Tumetuma watu kusafirisha miili ya waliouawa hadi hospitali ya Karachi na kuihifadhi."

Bw. Sun alisema, wahandisi wote 11 wakiwemo watatu walionusurika wamerudishwa mjini Karachi. Alieleza kuwa wahandisi hao walikwenda nchini Pakistan kwa ajili ya kusaidia kiteknolojia ya uzalishaji wa saruji. Licha ya kiwanda cha saruji cha mkoa wa Baluchistan, pia kuna viwanda vingine vilivyosaidiwa kiteknolojia na wahandisi wa China.

Bw. Sun Chunye alikanusha kabisa usemi wa baadhi ya vyombo vya habari vya magharibi kuwa, viwanda hivyo vilivyojengwa kwa msada wa China ni kwa ajili ya kuunga mkono bandari ya Guadal. Alisema kutokana na kuwa zana za uzalishaji wa saruji katika viwanda hivyo ni za China, ili kuhakikisha uzalishaji unaendelea kama kawaida wahandisi wa China wamekuja kusaidia kiteknolojia katika kipindi cha majaribio ya uzalishaji. Jambo hilo halina uhusiano wowote na ujenzi wa bandari ya Guadal."

 

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, rais Hu Jintao na waziri mkuu Wen Jiabao wa China mara waliziagiza wizara ya mambo ya nje ya China na ubalozi wa China nchini Pakistan ziitake Pakistan iwakamate wauaji, kuhakikisha usalama wa Wachina walioko nchini humo na kushughulikia kimamilifu mambo ya waliokufa. Waziri wa mambo ya nje wa China Li Zhaoxing alfajiri ya tarehe 16 aliwasiliana kwa simu na waziri wa mambo ya nje wa Pakistan kuhusu tukio hilo. Waziri wa mambo ya nje wa Pakistan alisema, serikali ya Pakistan itafanya kila iwezalo kuwakamata wauaji, kuchukuka hatua zote za kuhakikisha usalama wa Wachina nchini humo na kushughulikia kimamilifu mambo ya waliokufa.

Rais na waziri mkuu wa Pakistan walilaani vikali tukio hilo na kusema serikali ya Pakistan itachukua hatua zote zinazoweza kuchukuliwa, ili kuwakamata magaidi hao na kuwaadhibu kisheria. Kadhalika, walitoa rambirambi kutokana na vifo vya kwa wahandisi hao.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Pakistan Tasnim Aslam alipohojiwa na waandishi wa habari wa CRI alisema,

"Huu ni wakati wa huzuni sana. Wahandisi hawa wa China wamekuja nchini kwa ajjili ya kuisaidia Pakistan, ni marafiki zetu. Jambo hili kamwe halikubaliki, ni kitendo cha kigaidi. Sasa uchunguzi umeanzishwa kwa pande zote, na tutawagundua wauaji."

Idhaa ya kiswahili 2006-02-16