Majira ya baridi katika sehemu ya kaskazini ya dunia karibu yatapita, lakini homa ya mafua ya ndege haijatoweka, kinyume na hali hiyo ugonjwa huo unaenea kutokana na ndege wanaohama hama. Hivi karibuni, katika bara la Afrika ambalo uwezo wa kukinga na kudhibiti ugonjwa huo ni dhaifu, ghafla ilitokea homa ya mafua ya ndege, na katika nchi za Ulaya pia wamegunduliwa wagonjwa wenye virusi vya H5N1. Hivi sasa, karibu mabara yote duniani yamekumbwa na ugonjwa huo. Hali hiyo inamaanisha kuwa juhudi za kukinga na kudhibiti homa ya mafua ya ndege ni vita virefu kote duniani, na ushirikiano wa kimataifa ni wa lazima.
Mwanzoni mwa mwezi huu homa ya mafua ya ndege yenye virusi vya H5N1 ilitokea kaskazini mwa Nigeria, hii ni mara ya kwanza kwa Afrika kukumbwa na ugonjwa huo, baadaye barani Ulaya bata pori walioambukizwa na virusi vya H5N1 walikufa, na nchi kadhaa barani humo hazikuwahi kutokewa na ugonjwa huo hapo kabla.

Hali hiyo mpya imetahadharisha jumuyia ya kimataifa. Nchi za Afrika zikiwemo Nigeria, Mauritania, Senegal Ghana na Benin zimechukua hatua, na nchi za Umoja wa Ulaya pia zimeimarisha udhibiti ili kuzuia kuenea kwa homa hiyo na maambukizi kwa binadamu.
Nchi zinazoendelea na hasa nchi za Afrika hazina fedha za kutosha katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo kutokana na hali ya uchumi. Serikali ya Nigeria ilisema kuwa ingawa imechukua hatua za kuchinja na karantini, lakini ugonjwa huo unaonekana ukienea, rais wa nchi hiyo ameomba msaada mkubwa zaidi kutoka jumuyia ya kimataifa. Huu ndio wasiwasi ulipo, kwamba nchi yoyote ikikosa fedha za kutosha au hatua zisipotekelezwa, juhudi za nchi hiyo zitakuwa bure, na matokeo yatakuwa mabaya katika nchi hiyo na hata katika kanda nchi hiyo ilipo.
Mbele ya uwezekano wa kurudia tena kwa homa ya mafua ya ndege katika sehemu fulani, fikra za kujilinda kwa kila nchi kabisa hazifai, na ni vibaya zaidi kulaumiana, kwani kufanya hivyo hakusaidii kitu na kutaathiri vibaya ushirikiano. Njia sahihi ni kuwa, wenye nguvu wasaidie wadhaifu, watu matajiri wasaidie maskini, wenye fedha watoe fedha na wenye teknolojia wasaidie kwa teknolojia, ushirikiano uwe wa ukunjufu na mshikamano uwe wa muda mrefu, ili kupambana na ugonjwa huo kwa pamoja.
Tsunami iliyotokea katika bahari ya India mwishoni mwa mwaka 2004, ulionesha uokoaji uliosisimua unaostahili kukumbukwa daima, jumuyia ya kimataifa ilibadilika kuwa na umoja mkubwa. Hivi sasa mbele ya tishio la homa ya mafua ya ndege jumuyia ya kimataifa inahitajika kuendelea na moyo wa kusaidiana bila kulegea.

Ni jambo la kufurahisha kwamba, kuhusu umoja huo jumuyia ya kimataifa imeafikiana kimawazo. Waziri mkuu wa China Wen Jiabao kwenye mkutano wa kimataifa wa mawaziri uliofanyika mwezi Januari mwaka huu kwa ajili ya kukusanya fedha za kukinga na kudhibiti homa ya mafua ya ndege alitoa mapendekezo matatu: Kuanzishwa kwa mfumo wa ushirikiano duniani, ujenzi wa uwezo wa kupambana na homa hiyo uimarishwe, uongozi wa Umoja wa Mataifa ufanye kazi zaidi, na fedha zitolewe zaidi. Ofisa mmoja anayeshughulikia kazi ya kukinga na kudhibiti homa ya mafua ya ndege katika Umoja wa Mataifa hivi karibuni alionya kuwa, kati ya watu kama kukiwa na mmoja asiyewajibika vilivyo ni sawa wote hawawajibika. Msemaji wa WHO, Dick Thompson alisema, binadamu watashindwa katika mapambano hayo, kama hawataongeza fedha za mapambano hayo.
Homa ya mafua ya ndege ni tishio kwa binadamu wote. Lakini tuna uhakika kwamba mradi tu nchi zote zinasaidiana, zinafanya juhudi kwa pamoja na kufanya ushirikiano wa muda mrefu, ugonjwa huo unapokuwa mwanzoni utaangamizwa kabisa.
Idhaa ya kiswahili 2006-02-17
|