Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-20 20:59:22    
Ni vigumu kwa kundi la Hamas kupita hatua ya kushika hatamu za kiserikali

cri

Kundi la Hamas la Palestina tarehe 19 limetangaza kumteua rasmi kiongozi wake mmoja Ismail Haniyeh kuwa waziri mkuu mpya wa serikali inayojiendesha ya Palestina. Wachambuzi wanaona kuwa, Bwana haniyeh atakabiliwa na taabu nyingi za kuunda baraza la mawaziri na kushughulikia migongano ya ndani na ya nje ya Palestina.

Juu ya kuunda baraza la mawaziri, kabla ya hapo kundi la Hamas limesema litaunda serikali ya la shirikisho la kitaifa inayoundwa na wataalamu kutoka makundi mbalimbali. Hivyo kuwateua nani wajiunge na serikali hiyo ni taabu ya kwanza inayolikabili kundi la Hamas. Kwa kundi la Hamas lisilo na uzoefu wa kushika madaraka, chama cha ukombozi wa kitaifa wa Palestina Fatah kilichoshika madaraka kwa miaka mingi ni mshirika linalotaka kupata katika ushirikiano nalo, lakini mpaka sasa Fatah haijapokea rasmi mwaliko wake.

Kama serikali inayojiendesha ya Palestina ya siku zijazo haitashirikisha Fatah, Palestina itakuwa miundo miwili ya mamlaka. Moja ni Kamati ya utungaji wa sheria na serikali inayoongozwa na Kundi la Hamas, na nyingine ni mamlaka ya utawala wa Palestina chini ya uongozi wa mwenyekiti wake Mahmoud Abbas. Katika hali hiyo, migongano kati ya Baraza la mawaziri litakaloongozwa na Bwana Haniyeh na Mamlaka ya utawala wa Palestina hakika itazidi kuwa mingi. Kwa kweli, migongano kati ya kundi la Hamas na kikosi cha usalama cha Palestina kinachodhibitiwa na Fatah imeonekana kabla ya hapo. Tarehe 15 mwezi huu kamanda mkuu wa polisi wa kando ya magharibi ya Mto Jordan ya Palestina alilionya kundi la Hamas lisiingilie kati mambo ya polisi. Alisema, serikali mpya itakayoundwa na Hamas ikishirikiana na kikosi cha polisi ndipo itakapoweza kufanya kazi katika hali ya kawaida. Tarehe 18, kwenye sherehe ya kuapishwa kwa kamati ya awamu mpya ya utungaji sheria inayoongozwa na Kundi la Hamas, Bwana Abbas aliitaka bayana serikali mpya itambue makubaliano yote ya maani yaliyofikiwa kati ya Palestina na Israel hapo kabla, na kuitaka itumie mbinu za kiamani kupambana na ukaliaji wa Israel. Juu ya hiyo, msemaji wa kundi la Hamas Tarek Zeid al Masri alisema, Kundi la Hamas haliwezi kuacha mapambano ya kijeshi mpaka kutokomezwa kwa ukaliaji wa Israel. Aidha, mwenyekiti mpya wa kamati ya utungaji wa sheria ya Palestina Abdel Aziz Duaik alisema, atawaondoa madarakani maofisa waandamizi kadhaa wa Fatah walioteuliwa na Abbas hivi karibuni. Maofisa hao waliteuliwa na Abbas wakati kamati ya utungaji wa sheria iliyodhibitiwa na kundi la Fatah wataondolewa, na madhumuni ya kuwateua maofisa hao ni kubakiza madaraka ya Fatah katika kamati ya awamu mpya, kama kundi la Hamas litaamua kuwaondoa madarakani maofisa hao wa Fatah, hakika hii itaongeza zaidi migongano kati ya Abbas na kundi la Hamas.

Tatizo lingine kubwa linalolikabili kundi la Hamas kwa hivi sasa ni vikwazo vya kiuchumi vya Israel na Marekani na hali ya kutengwa katika mambo ya kidiplomasia. Baraza la mawaziri la Israel tarehe 19 lilipitisha azimio likiamua kuzuia fedha za ushuru za dola za kimarekani milioni 54 ilizokusanya ambazo ingeikabidhi Palestina. Uamuzi huo una maana kuwa, serikali ya Palestina itakuwa haina uwezo wa kutoa mishahara kwa watumishi laki moja na zaidi wa serikali na kikosi cha usalama. Aidha, Marekani pia inaitaka Palestina irudishe fedha za misaada ya dola za kimarekani milioni 50 iliyotoa mwaka jana kwa mamlaka ya utawala wa Palestina. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice tarehe 18 aliionya Iran isitoe misaada kwa kundi la Hamas. Wachambuzi wanaona kuwa, onyo lake hilo pia alilitoa kwa nchi nyingine za kiislamu. Bwana Abbas amesema, shinikizo la kimataifa linaonesha umuhimu wake, sasa Palestina iko katika mgogoro wa kifedha. Hivyo kundi la Hamas litakumbwa na taabu kubwa katika njia yake ya kushika hatamu za kiserikali.

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-20