Waziri wa habari wa Nigeria Bw. Frank Nweke tarehe 20 huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria alithibitisha kuwa baada ya kugunduliwa homa ya mafua ya ndege ya aina ya H5N1 tarehe 8 mwezi huu kwenye shamba la ufugaji wa kuku kwenye jimbo la Kaduna lililoko kaskazini mwa nchi hiyo, hivi sasa virusi vya homa ya mafua ya ndege vimeibuka katika sehemu 7 nyingine ukiwemo mji mkuu Abuja, hali ambayo inazidisha shida kwa udhibiti wa maambukizi hayo.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku hiyo Bw. Frank Nweke alisema, upimaji mpya wa maabara unaonesha kuwa a kuku waliokufa katika sehemu ya kaskazini ya Nigeria yakiwemo majimbo matatu na mji mkuu Abuja, walikufa kutokana na kuambukizwa virusi vya homa ya mafua ya ndege.
Lakini Bw. Nweke alisema, kutokana na jitihada za serikali ya Nigeria pamoja na mashirika ya utoaji misaada ya kimataifa, hivi sasa maambukizi hayo yamedhibitiwa kwenye sehemu za pembezoni mwa majimbo matatu kulikogunduliwa mapema zaidi virusi vya maradhi hayo. Alisema upimaji husika juu ya wafanyakazi walioko kwenye mashamba ya ufugaji wa kuku yaliyoambukizwa virusi vya homa ya mafua ya ndege unaendelea kufanyika, hadi hivi sasa bado hakuna mtu aliyeambukizwa virusi vya aina hiyo, lakini upimaji zaidi utaendelea kufanyika.
Maambukizi ya homa ya mafua ya ndege yaliyoibuka kwenye sehemu ya kaskazini ya Kaduna ni maambukizi ya homa ya mafua ya ndege yaliyogunduliwa kwenye bara la Afrika, yalifualitiwa mara moja na serikali ya Nigeria pamoja na nchi husika na baadhi ya mashirika ya kimataifa. Serikali ya Nigeria ilianzisha mara moja "kituo cha udhibiti wa mgogoro wa homa ya mafua ya ndege" ili kuratibu udhibiti wa maambukizi ya homa ya mafua ya ndege. Mbali na kuwachinja kuku, mabata wote wanaofugwa kwenye mashamba ya maeneo hayo, kunyunyizia dawa na kutenganisha mashamba hayo na sehemu nyingine, serikali ya Nigeria imetenga fedha nyingi ikiwa ni fidia kwa hasara wanayoingia wafugaji. Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria amehimiza mashamba ya ufugaji wa kuku na mabata yaliyoko kwenye sehemu mbalimbali yaombe kupewa ukaguzi husika, ili kuzuia maambukizi zaidi, tena aliomba watu husika waende kukagua shamba lake binafsi la ufugaji ikiwa ni mfano wa kuigwa kwa mashamba mengine.
Baadhi ya mashirika ya kimataifa na nchi husika yakiwemo shirika la afya duniani na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa yametoa misaada ya dharura ya fedha, zana na teknolojia. Mtaalamu husika amesema, kutokana na hali ya maambukizi yanayoendelea kuenea hivi sasa nchini Nigeria, maambukizi ya homa ya mafua ya ndege huenda yataendelea kwa muda fulani na yatazidisha shida kwa udhibiti wa homa ya mafua ya ndege.
Kutokana na matatizo ya kiuchumi na utamaduni, watu wa Nigeria bado hawajafahamu vizuri virusi vya homa ya mafua ya ndege pamoja na madhara yake, hususan kwenye sehemu kubwa ya vijiji yenye maambukizi ya homa ya mafua ya ndege.
Aidha katika sehemu ya kaskazini ya Nigeria ambayo imeathiriwa na homa ya mafua ya ndege, wafugaji wengi wanalalamika kuhusu fidia ndogo inayotolewa na serikali. Hivi sasa mpango wa fidia bado haujakubaliwa na wafugaji, baadhi ya wafugaji wanaendelea kuuza kuku na mabata wao ili kupunguza hasara yao, jambo ambalo limeongeza shida kwa udhibiti wa maambukizi ya homa ya mafua ya ndege.
|