Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-22 18:12:22    
Serikali ya China yafanya juhudi kuwapunguzia wananchi malipo ya matibabu

cri

Hivi sasa watu karibu wote nchini China wanafuatilia suala la kuwepo kwa malipo makubwa ya matibabu. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na wizara ya afya ya China, zaidi ya asilimia 80 ya watu wa China wanaona kuwa, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka 10 iliyopita, hivi sasa malipo ya matibabu yanachukua sehemu kubwa zaidi katika matumizi yote ya fedha kwenye familia. Lakini malipo hayo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku na kuwafanya watu wasitesite kwenda hospitali.

Laikni kwanini malipo ya matibabu nchini China yamekuwa ni makubwa? Na serikali ya China imechukua hatua gani ili kupunguza malipo ya matibabu, na je hatua hizo zimefanya kazi kwa ufanisi?

Katika mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, mtu mmoja alipatwa na saratani ya mafingofingo, na alitozwa malipo ya matibabu zaidi ya yuan za renminbi milioni 5, sawa na dola za kimarekani laki 5.2 alipolazwa hospitalini kwa muda wa miezi miwili, lakini gharama za matibabu kubwa kiasi hicho bado hazikuweza kunusuru masiha yake.

Baada ya tukio hilo kuripotiwa na vyombo vya habari nchini China, watu wengi walilifuatilia sana. Ingawa hii sio tukio la kawaida, lakini limefichua wazi tatizo la malipo makubwa za matibabu nchini China.

Watu wengi wa China wanasema, watu wa kawaida ambao kwa wastani pato lao kwa mwaka ni kati ya yuan elfu 10 hadi 20, malipo ya matibabu ya yuan milioni kumi kadhaa ni fedha nyingi sana. Wanaonesha wasiwasi kuhusu gharama za kujilipia wenyewe matibabu. Mkazi wa Beijing mzee Guo mwenye umri wa mika zaidi ya 50 alisema,

"Sina malipo makubwa, na hadi sasa nikiwa umri wa zaidi ya miaka 50, sijahifadhi fedha nyingi, lakini afya yangu sio nzuri, nina wasiwasi kwamba kama nikipatwa na ugonjwa mkubwa, siwezi kumudu malipo makubwa ya matibabu. Nafikiri hali ikiwa hivyo, ni afadhali nife."

Hivi sasa watu wa kawaida wa China wakiumwa kidogo hawaendi hospitali, wanavumilia tu; kama wakipatwa na ugonjwa mkubwa wanaacha matibabu kabisa kutokana na malipo makubwa ya matibabu. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na wizara ya afya ya China, karibu nusu ya wachina ambao wanatakiwa kwenda Hospitali kumwona daktari hawaendi hospitali, na asilimia 30 ya wachina ambao hali zao za ugonjwa zinawabidi walazwe, hawalazwi, chanzo muhimu cha kuwepo kwa hali hiyo ni gharama kubwa za matibabu.

Hospitali nchini China karibu zote ni hospitali za serikali, sababu muhimu inayofanya kuwepo kwa malipo makubwa ya matibabu ni baadhi ya hospitali kuzingatia faida za kiuchumi peke yake na kupuuza mambo mengine, na baadhi ya madaktari wanawafanyia wagonjwa upimaji wa aina mbalimbali ukiwemo upimaji ambao hauhitajiki, na kuwaandikia wagonjwa dawa za bei kubwa, ili kuongeza mapato yao wenyewe na mapato ya hospitali. Mbali na hayo, serikali haikutenga fedha za kutosha kwa hospitali hizo pia ni sababu nyingine inayozifanya hospitali zijitafutie faida ya kiuchumi.

Ili kuwatatulia wananchi matatizo ya malipo makubwa ya matibabu, serikali ya China na idara husika zimefanya juhudi kubwa katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, na zimefanya majaribio kadha wa kadha. Kwa mfano, sehemu za Beijing, Xinjiang na Zhejiang zimeanza kujaribu kuanzisha hospitali za kutoza malipo ya kawaida, hospitali hizo zinazoungwa mkono kiuchumi na serikali, zinawapunguzia wagonjwa malipo ya matibabu.

Mkuu wa hospitali ya kwanza ya bei nafuu ya hapa Beijing, Hospitali ya Shangdi Bi. Wang Ling alisema, katika hospitali yake ni malipo ya matumizi ya dawa ndiyo yanayochukua sehemu kubwa ya gharama zote za matibabu, ndiyo maana hospitali yake inatilia maanani sana kuwaandikia wagonjwa dawa za bei nafuu.

"Katika dawa halali zinazofanana, tunachagua dawa za bei nafuu zaidi kwa wagonjwa, ili kuwapunguzia mizigo yao ya kiuchumi."

Hospitali hiyo ambayo inawajali wagonjwa kihalisi inasifiwa na wagonjwa wengi. Mgonjwa mmoja anayepatwa na ugonjwa nyungunyungu aliambiwa kwamba malipo ya matibau yaliyotozwa na hospitali ya Shangdi sio makubwa, akaenda kwenye hospitali hiyo, alisema:

"Katika hospitali ya Shangdi, nililipa yuan elfu moja tu?lakini kama ningetibiwa katika hospitali nyingine, ningelipa yuan elfu 2 au 3."

Katika mikoa ya Hennan, Zhejiang na Shandong, baadhi ya hospitali zinajaribu kupunguza gharama za matibabu kwa kuweka kikomo cha malipo ya matibabu ya ungonjwa fulani peke yake, yaani mgonjwa anayepatwa na ugonjwa mmoja peke yake ambao hausababishi ugonjwa mwingine, basi jumla ya gharama za matibabu inatakiwa kuwa chini ya kiasi fulani. Hatua hiyo imetekelezwa katika hospitali moja mjini Jining, ambapo kwa wastani malipo ya matibabu ya hospitali hiyo yamepungua kwa asilimia 33.

Kutokana na kutoza malipo ya chini ya matibabu, hospitali hiyo inajulikana, na watu wengi wanapenda kwenda kwenye hospitali hiyo.

Bw. Liu ni mkulima, mtoto wake alizaliwa na ugonjwa wa moyo, lakini malipo makubwa ya matibabu yanamzuia kumpeleka mtoto huyo kufanyiwa operesheni. Bw. Liu aliambiwa kuhusu hospitali ya huko Jining ambayo malipo ya matibabu ni asilimia 60 tu ya malipo yanayotozwa na hospitali nyingine, akasafiri mamia ya maili kumpeleka mtoto wake katika hospitali hiyo, alisema:

"Niliambiwa kwamba nahitaji yuan elfu kumi kumtibu mtoto wangu, habari hii imeniletea matumaini. "

Ofisa wa wizara ya afya ya China Bw. Gao Qiang alidokeza kuwa, wakati serikali inapochukua hatua mbalimbali zilizotajwa, China inafanya maandalizi kwa kutoa mpango wa mageuzi ya utaratibu wa matibabu, ili kutatua kimsingi tatizo la kuwepo kwa malipo makubwa ya matibabu.

"Tumefanya utafiti juu ya suala la kufanya kwa kina mageuzi ya utaratibu wa matibabu mijini, na tumethibitisha kanuni za kimsingi, lakini mpango mzima unahitaji kuthibitishwa."

Bw. Gao Qiang aliongeza kuwa, kabla ya kutolewa kwa mpango huo, sehemu mbalimbali nchini China zinapaswa kutafuta ufumbuzi wa kupunguza malipo ya matibabu kwa wagonjwa.