Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-22 18:36:07    
Mapishi ya slesi za nyama ya kuku

cri

Mahitaji

Nyama ya kuku gramu 750, ute wa yai moja, slesi zilizokaushwa za vichipukizi vya mianzi gramu 25, chumvi gramu 5, mvinyo wa kupikia gramu 20, M.S.G gramu 2, vitunguu saumu gramu 5, maji ya wanga gramu 25, mafuta gramu 100.

Njia

1? Kata nyama ya kuku iwe vipande vidogo vidogo, na koroga pamoja na ute wa yai, ukiwa umetia chumvi.

2? Chemsha maji, halafu tia slesi zilizokaushwa za vichipukizi vya mianzi kwenye maji halafu zipakue.

3? Pasha moto tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe nyuzi ya 50, tia vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga mpaka viive kwa joto la nyuzi 80, kisha vipakue.

4? Pasha moto tena, tia vipande vya vitunguu saumu korogakoroga halafu tia slesi zilizokaushwa za vichipukizi vya mianzi korogakoroga halafu tia vipande vya nyama ya kuku korogakoroga, tia chumvi, mvinyo wa kupikia, M.S.G korogakoroga halafu vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.