Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-23 19:43:18    
Hamas na Fatah zaitisha mkutano kuhusu uundaji wa serikali

cri

Kundi la kiislamu la Palestina, HAMAS na kundi la chama cha ukombozi wa taifa cha Palestina, FATAH tarehe 22 ziliitisha mkutano wa kwanza kuhusu uundaji wa serikali ya umoja, jambo hilo linafuatiliwa na watu wengi duniani.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina mwezi uliopita, uundaji wa serikali mpya umekuwa ukifuatiliwa sana na pande mbalimbali husika. Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw Mahmoud Abbas tarehe 21 alimteua Bw. Haniyeh, kiongozi wa HAMAS kuwa waziri mkuu wa serikali mpya. Baada ya hapo HAMAS ilizindua rasmi mchakato wa mazungumzo na vyama mbalimbali kuhusu uundaji wa serikali.

Tarehe 22, mazungumzo kati ya viongozi wa HAMAS na FATAH yalifanyika kwenye ukanda wa Gaza. Ingawa HAMAS na FATAH havikudokeza mambo halisi yaliyozungumzwa, lakini wachambuzi walisema, usawazishaji wa miongozo ya utawala ya vyama hivyo viwili na mgawanyo wa madaraka ya serikali lilikuwa suala lisiloepukika katika mazungumzo yao. Hivi karibuni Bw. Abbas alipoapishwa katika kamati mpya ya utungaji sheria, alitaka serikali mpya inayoongozwa na HAMAS ifuate mikataba iliyosainiwa na Palestina na Israel pamoja na mpango wa "ramani" ya amani wa mashariki ya kati ili kuleta amani pamoja na Israel kwa njia ya mazungumzo. Kiongozi mmoja wa FATAH tarehe 21 alisema, endapo 60% ya mwongozo wa utawala wa HAMAS unaendana na ule wa FATAH, basi FATAH itafikiria kushiriki katika serikali mpya. Aidha, katika masuala ya mgawanyo wa madaraka ya serikali, hususan yale muhimu ya udhibiti wa idara muhimu za usalama na mambo ya kidiplomasia, vyama viwili vitakuwa na mvutano mkubwa.

Kikanuni, HAMAS yenye viti vingi katika kamati ya utungaji wa sheria ya Palestina, linaweza kuunda serikali peke yake. Lakini kiongozi wa HAMAS katika siku ya kwanza tangu ilipopata ushiriki katika uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria, alieleza wazi kuwa anatarajia kuunda serikali pamoja na FATAH, ambayo ilishindwa katika uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria. Wachambuzi wa huko walisema, kuhusu suala la utawala, HAMAS inafahamu vizuri hali yake, kwanza, ikiunda serikali pake yake itakuwa vigumu kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa; Pili, HAMAS haina uzoefu wa utawala na haina makada; Tatu, udhaifu wa Palestina kutokana na kukaliwa kwa muda mrefu ni shida kubwa kukabiliana peke yake changamoto ya migongano ya kisiasa ya makundi mbalimbali nchini na misukosuko ya kijamii ya nchi hiyo. Endapo FATAHA itashiriki kwenye serikali mpya, kwa upande mmoja HAMAS inaweza kuitumia FATAH, ambayo imekuwa na athari kubwa duniani, kupunguza matatizo hayo, ili kupunguza shinikizo duniani dhidi ya serikali mpya ya Palestina; Kwa upande mwingine uzoefu wa utawala wa FATAH katika miaka zaidi ya kumi iliyopita utaweza kujaza pengo la upungufu wa uzoefu wa HAMAS katika uendeshaji wa shughuli za kiserikali.

Kuna maoni tofauti ndani ya FATAH kuhusu kuunda serikali pamoja na HAMAS. Baadhi ya watu wanaona, sera za vyama hivyo ni tofauti sana, hivyo hakuna msingi wa kufanya ushirikiano. Kuna watu wanaosema, kazi ya haraka kwa FATAH ni kujibadilisha kuwa chama cha upinzani, kukusanya nguvu zake na kuwania ushindi katika kipindi kijacho cha utawala. Lakini, viongozi wa ngazi ya juu wa FATAH akiwemo Bw. Abbas, mwenyekiti wa mamlaka ya taifa ya Palestina, wanataka kushiriki katika serikali mpya. Wachambuzi walisema, kwa upande mmoja, katika mazungumzo ya uundaji wa serikali, FATAH inaweza kuibana HAMAS kujibadilisha kutokana na haraka yake ya kutaka FATAH ishiriki kwenye serikali mpya, kuilazimisha HAMAS kujisogeza na msimamo wa Bw. Abbas wa kujenga nchi kwa njia ya amani. Kwa upande mwingine, FATAH baada ya kushiriki kwenye serikali mpya, itaweza kuathiri HAMAS ili kunufaisha mamlaka ya taifa ya Palestina kuendelea kutekeleza mwongozo wake wa kisiasa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-02-23