Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-24 14:04:04    
Nchi za Afrika zazikaribisha kampuni za China kushiriki katika uchimbaji wa madini

cri

Tarehe 7 hadi 10 Februari mwaka huu, mkutano wa Afrika kuhusu uwekezaji wa uchimbaji madini ulifanyika huko Cape Town, Afrika ya kusini. Kwenye mkutano huo, viongozi kutoka nchi 30 za Afrika wanaoshughulikia uchimbaji madini na wahusika kutoka kampuni kubwa za uchimbaji madini duniani ,walikuwa wanajadiliana kuhusu uwekezaji, biashara na uvumbuzi wa teknolojia katika sekta ya uchimbaji madini.

Bara la Afrika lina rasilmali nyingi za madini. Kiasi cha aluminium, vanadium na thorium zilizogunduliwa nchini Guinea kinachukua asilimia 24 ya kile cha duniani, kiasi cha chrome kilichogunduliwa nchini Afrika ya kusini kinachukua asilimia 80 ya duniani, ambapo Afrika kusini na Gabon ni nchi zinazozalisha madini aina ya manganese kwa wingi zaidi duniani, na kiasi cha phosphate kinachozalishwa nchini Morocco kinachukua nafasi ya kwanza duniani. Zaidi ya hayo, nchi za Afrika zinakidhi asilimia 30 ya mahitaji ya dhahabu duniani, Afrika kusini inachukua nafasi ya kwanza katika kuzalisha dhahabu dunani. Isitoshe, kiasi cha shaba, antimony, cobalt, asbestos, uranium, lithium na aina nyingine za madini kilichogunduliwa barani Afrika pia kinachukua nafasi ya mbele duniani.

Mwandishi wetu wa habari aliyeko nchini Afrika kusini aliona kuwa, japokuwa mara hii hakuna mjumbe wa China aliyehudhuria kwenye mkutano huo, lakini athari ya China bado ilionekana hapa na pale kwenye mkutano huo. Kwenye hotuba zilizotolewa na wajumbe wa nchi mbalimbali za Afrika na makampuni mbalimbali duniani, neno la "China" lilitajwa mara kwa mara, walipoitaja "China" walikuwa wanasifu maendeleo makubwa ya kiuchumi yaliyopatikana nchini China, na makadirio na tathmini ya athari zitakazoletwa na maendeleo ya China kwa soko la madini duniani.

Mjumbe mwanamke kutoka Ghana alipokutana na mwandishi wetu wa habari alisema kwa furaha kuwa, siku hiyo alikuwa amejifunza neno jipya la Kiingereza la "Chindia". Neno la "Chindia" ni neno la muungano la "China" na "India". Kutokana na kujitokeza kwa China na India kwenye soko la kimataifa la uchimbaji madini, nchi hizo mbili zilizungumzwa kwa pamoja mara kwa mara, hivyo likaundwa neno la "Chindia". Na alipozungumza na wajumbe wengine wa nchi za Afrika mwandishi wetu wa habari alikuwa amesikia mshangao wao kwa maendeleo makubwa ya kiuchumi yaliyotokea nchini China, na matarajio yao ya kushirikiana na China katika uchimbaji madini.

??

Kwenye kituo cha mkutano huo, kulikuwa na vibanda vingi vya maonesho vya nchi za Afrika na makampuni ya uchimbaji ya madini duniani. Kwenye kibanda cha Tanzania, mfanyakazi mmoja kutoka Tanzania alimpatia mwandishi wetu wa habari karatasi zote za matangazo bila kujali kama alihitaji karatasi hizo au la, na kuzungumzia reli ya TAZARA na urafiki uliopo kati ya Tanzania na China. Mfanyakazi huyo alisema, serikali ya Tanzania na wananchi wake wanakaribisha sana makampuni ya China kuwekeza katika sekta ya uchimbaji madini nchini humo.

Kwenye kibanda cha maonesho cha Zambia, mwandishi wetu wa habari pia alikaribishwa sana, na mazungumzo yao pia yalianza na reli ya TAZARA. Kutokana na mazungumzo yao, mwandishi wetu wa habari alisikia upendo mkubwa wa watu wa Zambia kwa China. Alipouliza msimamo wa Zambia kuhusu propaganda ya nchi za magharibi kuhusu "China kunyang'anya maliasili za Afrika", mfanyakazi mmoja kutoka wizara ya madini ya Zambia alijibu kuwa, usemi huo ni wa uwongo mtupu. Zambia na China zote ni nchi zilizowahi kukandamizwa na nchi za kikoloni, lakini China ilisaidia kujenga reli ya TAZARA, ambapo nchi za magharibi ziliiacha Zambia kutokana na kutokuwa na faida. Mfanyakazi huyo alisema, Zambia inazikaribisha kwa udhati kampuni za China kuwekeza nchini humo, ili kushirikiana na Zambia kuchimba rasilmali. Kwenye vibanda vingine vya Nigeria, Zimbabwe na Afrika kusini, mwandishi wetu wa habari pia aliweza kuhisia ukarimu mkubwa kutoka kwa watu wa Afrika kwa China.

Idhaa ya kiswahili 2006-02-24