Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-27 16:00:39    
Dali, Mji wa kale wenye vivutio

cri

Katika mkoa wa Yunnan, kusini mwa China, kuna mji mmoja wenye historia ya zaidi ya miaka 600 unaoitwa Dali. Mpaka sasa mji wa Dali kimsingi bado unadumisha mpangilio wake wa kale, mjini humo kuna majengo mengi yaliyojengwa zamani, na wakazi wengi wa mji huo wanafuata desturi na mila za zamani. Ingawa siku nenda siku rudi, mji huo wa kale pia umepata sura mpya, lakini sura ya kale na hali ya kisasa zinaonekana siku zote katika mji huo wa kale.

Mji wa kale Dali ulioko magharibi ya mkoa wa Yunnan una eneo la kilomita za mraba 6 hivi. Ukiangalia mji huo kutoka Mlima Cang ulioko karibu na mji wa Dali, utaona kuwa njia zilizoko mjini humo zinaonekana kama ni ubao wa kuchezea chesi; mlango mkubwa wa mji huo wa kale unasimama kidete, na njia kuu inayoanzia kwenye mlango huo inapita kwenye sehemu ya kusini hadi kaskazini ya mji huo.

Ukipita mlango mkubwa na mrefu na kuingia kwenye mji huo wa kale, utaona hali ya mjini humo ni tofauti kabisa na miji mingine ya kisasa yenye makelele. Vijito vyenye maji safi kandoni mwa njia, vijia vyembamba vya mawe vinavyoingia mbali, kuta za ua wa nyumba zilizojengwa kwa mawe madogomadogo pamoja na paa za vigae vyeusi vya majengo yote mjini, yote hayo yanaonesha mtindo wa ujenzi wa zama za kale zinazopendeza.

Mji Dali ni moja ya sehemu wanazoishi watu wengi zaidi wa makabila madogomadogo nchini China. Nyumba za makazi ya watu wa kabila la wabai zilijengwa kwa kufuata hali ya hewa ya huko, njia za maisha ya huko na upendeleo wa wakazi wa huko, kila nyumba huwa na vyumba vitatu pamoja na ukuta mmoja. Mwongozaji wa utalii Bi. Li Yi alituambia:

Nyumba za makazi ya watu wa kabila la wabai hujengwa kwa mtindo wao pekee, kila nyumba ina chumba kimoja kikuu pamoja vyumba viwili vingine, lakini chumba kikuu kinakabiliana na ukuta mmoja. Kila ikikaribia saa za jioni, jua linapiga ukuta, halafu mwangaza wake unamulika uani, hivyo ua mzima huonekana na mwangaza. Usanifu huo hasa ni kwa ajili ya kujipatia mwangaza uani.

Mbali na usanifu murua wa nyumba za makazi katika mji huo wa kale, makazi ya mji huo pia yanapambwa vizuri, takriban kila familia inapanda maua na majani, hata familia nyingi zimejenga mabustani yao makubwa na madogo. Maua na miti iliyopandwa ndani ya nyumba zinazoegemeana inashikamana na kuwa vichochoro vingi vya maua na majani, ambapo maua yanayochanua yanatoa harufu nzuri mjini. Katika majira ya mchipuko na majira ya joto, wakati maua na majani yaliyonyauka yakipukutika na kuanguka ndani ya vijito, watalii wanaopita huko wanakuwa na husuda juu ya wakazi wa Dali wanaopenda maisha ya kujistarehesha.

Katika maisha ya wakazi wa Dali, unaweza kuona dalili nyingi za mila na desturi za jadi. Kuonja chai za aina tatu ni moja kati ya desturi zisizobadilika maishani mwa wakazi wa mji huo wa kale. Inasemekana kuwa desturi ya kuonja chai za aina tatu ilikuwa desturi ya mfalme wa nchi ya Dali katika zama za kale kwa kuwakirimu wageni mashuhuri, desturi hiyo ilienea miongoni mwa raia na inaendelea mpaka sasa .

Chai za aina tatu ni chai chungu, chai tamu na chai ya kukumbusha ladha. Wageni wakija kwanza wanaonja chai chungu; halafu wanaonja chai tamu ambayo ndani kuna tangawizi, asali na vitu vingine; na mwishoni wanaonja chai iliyotiwa pilipili na nyinginezo.

Mhudumu wa baa moja la chai Bi.Wang Hongyuan alituambia kuwa, kuonja chai za aina tatu si kama tu kuna historia tangu enzi na dahari, bali pia kuna maana muhimu. Akisema:

Kuonja chai za aina tatu kuna maana muhimu, desturi hiyo inawaambia kuwa kuishi maisha si rahisi, wakionja kwanza uchungu wa maisha, wakipata maisha mazuri wangethamini utamu wa maisha, na kila baada ya kupita vipengele vya maisha, wanapaswa kujumuisha uzoefu, na kutambua wapi wako sahihi na wapi walifanya makosa.

Mbali na kuonja chai, watalii wakienda kwenye mikahawa mbalimbali mjini Dali kuonja vyakula vya aina mbalimbali pia watafahamu zaidi jinsi wakazi wa Dali wanavyoishi maisha yao katika hali ya kujistarehesha, vyakula vya mji huo ni vingi na vya aina mbalimbali, ambavyo vinawafurahisha sana watalii. Kwenye kibanda kimoja cha chakula, mtalii kutoka Beijing Bi. Zhang Qian alikuwa anakula kwa furaha, akimwambia mwandishi wetu wa habari:

Vyakula vya mjini Dali kweli ni vitamu sana, vyote ni vyenye umaalum wa sehemu hiyo. Kabla ya kuja hapa nilitaka kupunguza kula chakula ili nisinenepe, lakini nimefika hapa nikavutiwa na vyakula vitamu vya hapa, basi nakula sana, baada ya kuondoka ninapaswa kupunguza kula.

Mandhari nzuri ya Mji wa Dali, majengo ya kale na vyakula vitamu, vyote hivyo vinawavuta sana watalii kutoka nchini China na nchi za nje, wageni wanaomiminika mjini humo pia wanakuja na vitu vya kisasa. Hivi sasa mjini Dali, kwenye njia moja ya mawe yenye urefu wa mita elfu moja hivi, kando mbili imejengwa mikahawa ya chakula cha magharibi, mikahawa ya chai na baa. Watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani wenye rangi tofauti wanafanya utalii mjini humo, hata baadhi yao wanakaa huko kwa muda mrefu, njia hiyo sasa imekuwa "njia ya wazungu" inayojulikana nchini na ng'ambo.

Kwenye "njia ya wazungu", unaweza kuona mara kwa mara wageni wanaokunywa kahawa, kusoma au kuangalia mandhari ya barabarani ndani ya baa na mikahawa ya chai. Wanaonekana kuwa ni watu wanaojistarehesha sana ambao wanauchukulia mji Dali kama nyumbani kwao. Mtalii Bi. Geraldine Laurendeau kutoka Canada ni mmoja kati yao, alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, maisha ya mjini Dali yamemfanya ang'ang'anie huko hata kusahau kurudi nyumbani.

Niko hapa mjini Dali nimepata picha kubwa ambayo lugha ya mjini humo ni ya ajabu, nimejifunza kidogo, kufanya hivyo ninaweza kuelewa zaidi utamaduni wa sehemu hiyo. Naona watu wa Dali na wa mkoani Yunnan wote ni wenye ukarimu na uchangamfu, na mandhari ya Dali ni nzuri sana. Kuja Yunnan kwa utalii ni rahisi sana, pia ni rahisi kufanya mawasiliano na wakazi wa hapa.

Idhaa ya kiswahili 2006-02-27