Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-02-28 16:00:43    
Wastani wa ongezeko la mwaka la mikopo kwa kazi ya kilimo wafikia yuan zaidi ya bilioni 149

cri
Shughuli za kilimo, vijiji na wakulima zimekuwa zikipata misaada mingi zaidi ya fedha kutoka kwa mashirika ya fedha nchini China. Mwishoni mwa mwaka jana, mikopo ya kilimo iliyobaki kwenye mashirika ya fedha ya ushirikiano ya sehemu za vijijini China iliongezeka kwa RMB Yuan bilioni 449.2 kuliko mwaka 2002, na wastani wa ongezeko ulizidi RMB Yuan bilioni 149 kwa mwaka likiwa ni ongezeko la asilimia 80, kiasi ambacho kimeongezeka kwa asilimia 22.6 kuliko wastani wa ongezeko la mikopo mingine.

Kwenye Mkutano wa usimamizi na mageuzi ya mashirika ya fedha uliofanyika tarehe 20 mwezi Februari, naibu mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa shughuli za benki ya China Bw. Tang Shuangning alisema, tangu kuanzishwa kwa majaribio ya mageuzi ya mashirika ya fedha vijijini, mashirika ya fedha ya ushirikiano ya vijiji yametoa huduma mbalimbali katika kuendeleza shughuli za kilimo, na mikopo inayotolewa kwa kusaidia kazi ya kilimo, vijiji na wakulima imepata ongezeko dhahiri.

Mwishoni mwa mwaka jana, mikopo ya kilimo iliyobaki kwenye mashirika yote ya fedha ya vijiji yakiwa ni pamoja na mashirika ya fedha vijijini, Benki za biashara za vijiji, na Benki za ushirikiano za vijiji, ilichukua asilimia 45.8 ya mabaki ya mikopo yote, na mikopo hiyo iliwahudumia wakulima zaidi ya milioni 70, kiasi ambacho kinachukua asilimia 50 ya watu wote wanaohitaji mikopo vijijini.

Mashirika ya fedha ya ushirikiano ya sehemu ya vijiji ni nguzo ya shughuli za fedha vijijini nchini China. Mwishoni mwa mwaka jana, thamani ya jumla ya raslimali za mashirika hayo nchini China ilizidi RMB Yuan trilioni 3.7. Bw. Tang Shuangning alisema, kadiri sera na hatua mbalimbali zinavyotekelezwa hatua kwa hatua katika miaka miwili iliyopita tangu majaribio ya mageuzi ya mashirika ya fedha vijijini yaanzishwe mwaka 2003, ndivyo mazingira ya uendeshaji na usimamizi wa mashirika ya fedha vijijini yanavyoboreshwa, shughuli mbalimbali za fedha zimepata maendeleo ya haraka, na mageuzi kuhusu majaribio ya mashirika ya fedha vijijini yamepata maendeleo makubwa.

Serikali za mikoa mbalimbali nchini China zinashughulikia kazi ya usimamizi wa mashirika ya fedha ya vijiji na kubeba jukumu la kukabiliana na mgogoro wa mambo ya fedha. Hadi sasa mashirika ya fedha ya mikoa 25 yameanzisha ushirikiano, na benki za biashara za vijiji zimeanzishwa Beijing, Shanghai na Tianjin, aidha, mashirika ya fedha vijijini yataanzishwa katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, na mageuzi ya mashirika ya fedha vijijini yanafanyika mkoani Hainan.

Baada ya hatua za kuunganisha mashirika na kufanya majaribio kuanzisha mashirika ya shughuli za benki vijijini, utaratibu wa umilikaji na uendeshaji umepata maendeleo kwa hatua madhubuti. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, China ilianzisha mashirika 72 ya shughuli za benki, zikiwemo benki 12 za biashara za vijiji, benki 60 ya ushirikiano za vijiji, na mashirika mengine 9 ya benki ya ushirikiano vijijini yako tayari kuidhinishwa na kuanzishwa.

Kutokana na misaada ya fedha ya Benki kuu ya China na serikali za mikoa mbalimbali, pamoja na ongezeko la fedha na hisa kwenye mashirika ya fedha vijijini, tatizo la upungufu wa fedha na migogoro ya mambo ya fedha ya mashirika ya fedha ya ushirikiano vijijini zimepungua.

Mwishoni mwa mwaka jana, mikopo mibaya iliyobaki kwenye mashirika ya fedha ya ushirikiano vijiji nchini China ilikuwa Yuan bilioni 325.5, kiasi ambacho kilipungua kwa Yuan bilioni 125.9 kuliko mwanzoni mwa mwaka jana, na kupungua kwa RMB Yuan bilioni 189.2 kuliko mwishoni mwa mwaka 2002 kabla ya kufanyika kwa mageuzi. Kwa ujumla sifa ya raslimali ya mashirika ya fedha ya ushirikiano ya vijiji nchini China inaongezeka siku hadi siku.