Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-01 20:26:59    
Wachina wafuatilia utatuzi wa suala la mtu kukosa afya nzuri

cri

Pamoja na maendeleo ya kasi ya uchumi, wachina hususan wakazi wa mijini, wanafanya kazi kwa chapuchapu zaidi, ambapo baadhi watu wanakosa afya nzuri kutokana na shinikizo la kazi. Watu hao hawana afya nzuri, lakini wao siyo wagonjwa, hali hiyo inafuatiliwa na idara za afya na umma. Je, chanzo cha mtu kukosa afya nzuri ni nini? Na hali hii ina madhara gani kwa watu?

Bibi Peng anafanya kazi katika kampuni moja mjini Beijing, hivi karibuni kutokana na marekebisho ya kazi ya kampuni hiyo, kazi zake zimeongezeka, na hana budi kufanya kazi kwa saa nyingi zaidi kuliko kawaida yake, hivi sasa hakuna utaratibu maalum wa kula chakula na kulala usingizi, bibi Peng anasikia uchovu sana na hali yake si nzuri kama zamani. Alisema,

"Ninafanya kazi kutwa nzima, sina nafasi ya kupumzika katikati ya kazi, licha ya hayo sina saa maalumu ya kwenda kula chakula. Naona afya yangu si nzuri tena."

Ni kama watu wengi wanavyokuwa, bibi Peng hafahamu vizuri kuhusu hali yake hiyo isipokuwa anasikia uchovu, na hana uchangamfu.

"Hali ya afya isiyo nzuri sana" ilitolewa na mtaalamu mmoja wa Russia miaka 30 iliyopita. Baada ya kufanya utafiti kwa miaka mingi, ingawa hali hiyo bado haiwezi kuthibitishwa kwa kigezo kimoja, lakini madaktari wengi wanakubaliana na maoni hayo. Mkurugenzi wa kituo cha uthibitishaji wa hali ya afya ya marubani nchini China Bw. Wu Liuxin alisema,

"Maoni kuhusu hali ya afya isiyo nzuri sana ni kueleza hali ya afya kati ya mtu mzima kabisa na mgonjwa. Mtu aliye katika hali hiyo isiyo na afya nzuri, licha ya kutoweza kufikia kiwango cha kisasa kuhusu afya, ambaye katika kipindi fulani anaonekana kuzorota kwa uwezo wa mishipa na viungo vya mwili, kukosa uhamasa, kushindwa kuendana vizuri na mazingira mapya, kukosa ulingano moyoni, wala siyo kwamba hali yake imefikia kiwango cha kuweza kuthibitishwa kuwa ni mgonjwa kwa kigezo cha hivi sasa."

Bw. Wu, alisema, mtu aliyeko katika hali hiyo, kwanza anaonekana kuumwa kichwa, kusikia uchovu, kutopata usingizi mzuri, kutokuwa na furaha, tena hali hiyo inaendelea kwa muda fulani, ambao kwa kawaida ni kati ya miezi 3 na nusu mwaka; mtu anayeumwa kichwa au kusikia uchovu kwa muda mfupi siyo mtu aliyekosa afya nzuri.

Bw. Wu alisema,

"Kuna vyanzo 6 muhimu vinavyofanya mtu kutokuwa na afya nzuri. Cha kwanza, kuwa na wasiwasi na kukabiliwa na shinikizo kubwa. Pili, "saa ya mwilini" kutokuwa na majira sahihi. Tatu, mazoea mabaya ya maisha. Nne, kuchafuliwa kwa mazingira ya makazi na maisha. Tano, kukabiliwa na hali mbaya kimawazo. Na sita, mawazo mazito na matukio makubwa yanayosababisha kutokuwa na ulingano wa kimawazo."

Je, hali ya kutokuwa na afya nzuri kuna madhara gani kwa watu? Kwanza kabisa, hali hiyo ni chanzo cha maradhi mengi ya muda mrefu na yasiyo ya kuambukiza. Utafiti husika unaonesha, kuwa watu huugua saratani, maradhi ya moyo, mishipa ya damu na ugonjwa wa kisukari unafuata baada ya kukosa afya nzuri kwa kipindi fulani. Aidha, hali ya mtu kutokuwa na afya nzuri inaathiri ufanisi wa kazi, ubora wa maisha na masomo. Kwa upande mwingine hali hiyo inapunguza maisha ya mtu anayekosa afya nzuri, ambaye hata anaweza kufa akiwa kijana.

Idara za tiba za China zinazingatia sana suala la mtu kutokuwa na afya nzuri. Katika miaka ya karibuni sehemu za tiba ya watu wanaokosa afya nzuri zimeanzishwa katika baadhi ya hospitali za baadhi ya miji mikubwa na wastani.

Kwa watu wasio na afya nzuri, kwanza kutoa tathmini kwa mujibu wa matokeo ya ukaguzi wa afya yao na kubuni mipango inayoendana na hali yao halisi. Ukaguzi wa afya kwa watu wasio na afya nzuri, licha ya kufanya ukaguzi na upimaji wa kawaida kuhusu viungo na mishipa ya miili yao, upimaji mwingine unafanyika kuhusu uwezo wa kiroho na miili yao. Kwa mfano, mtu anapokagua hali ya afya yake, pengine anatakiwa kufanya mazoezi ya kukimbia kwa dakika kumi kwenye zana ya mazoezi ya ukimbiaji ili kujua uwezo na hali ya moyo na mapafu yake.

Nchini China, hivi sasa watu wasio na afya nzuri wanasaidiwa kurejeshwa afya nzuri kwa tiba za aina mbili za nchi za magharibi na ya jadi ya kichina. Tiba ya nchi za magharibi ni pamoja na lishe bora, mazoezi ya mwili, kuwa na saa za usingizi za kutosha, faraja na marekebisho ya kiroho; wakati mwingine mbinu hizo kutumika pamoja na kutumia dawa hata kutumia zana maalumu ya tiba ikiwemo hyperbaric oxygen chamber.

Tiba ya jadi ya kichina yenye historia ya miaka elfu kadhaa inapendwa zaidi na watu wasio na afya nzuri nchini China. Kuhusu hali hiyo, mkuu wa taasisi ya sayansi ya tiba ya jadi ya kichina Bw. Cao Hongxin alisema,

"tiba ya jadi ya kichina ikiwa ni pamoja na akyupancha, kukanda mwili na teknolojia ya tiba ya kupumua inatoa njia nyingi zenye ufanisi za kurejesha afya nzuri kwa watu wenye matatizo hayo.

Bw. Cao alisema, tiba ya jadi ya kichina haitegemei sana matokeo ya upimaji, bali ni kufuatilia chanzo cha matatizo ya mwili kwa kuchunguza dalili zinazoonekana katika miili ya wagonjwa pamoja na uhusiano kati ya dalili hizo na matatizo ya mgonjwa. Mbali na hayo, imani ya tiba ya jadi ya kichina inazingatia umaalum wa kila mgonjwa ukiwa ni pamoja na hali ya mwili na mazingira anayoishi mgonjwa. Hivyo, mipango ya tiba kuhusu wagonjwa wanaougua magonjwa ya aina moja huwa ni tofauti, na umaalum huo unafaa sana katika kurejesha afya kwa watu wasio na afya nzuri.

Mambo anayotaja Bw. Cao ndiyo sifa za tiba ya jadi ya kichina, ambayo inaweza kutoa tiba sahihi na yenye ufanisi zaidi kwa wagonjwa.