Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-01 20:40:45    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe na tangawizi

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe gramu 300, tangawizi gramu 150, mvinyo wa kupikia gramu 40, mchuzi wa sosi gramu 20, sukari gramu 10, maji ya wanga gramu 20, pilipili manga gramu 1, vipande vya vitunguu maji na vituanguu saumu gramu 20, mafuta gramu 200.

Njia

1. kata tangawizi iwe vipande, na kata nyama ya ng'ombe iwe vipande vipande, koroga pamoja na mchuzi wa sosi, pilipili manga, wanga, mvinyo wa kupikia, mafuta na maji.

2. pasha moto, tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi ya 60, tia vipande vya nyama ya ng'ombe korogakoroga kwa haraka halafu vipakue.

3?pasha moto tena, tia vipande vya vitunguu maji na vitunguu saumu, sukari, mchuzi wa sosi, M.S.G na maji, baada ya kuchemka, tia maji ya wanga korogakoroga halafu tia vipande vya nyama ya ng'ombe na vipande vya tangawizi korogakoroga, vipakue. Kitoweo hiki sasa kiko tayari kuliwa.